Zanzibar kutoka nchi hadi mkoa.

Nonda

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
13,358
4,304
Zanzibar from a sovereign nation to a region of Grand Tanganyika(Tanzania)- a step back-ward.

Baada ya kutembelea hizi sites, kwa hakika sasa ninaelewa kwa nini ndugu zetu wazanzibari wanapiga kelele ya kuwa hatuwatendei haki.

Kama sisi Tanganyika tungeungana na Kenya halafu wakatuambia "ninyi muwe mkoa wa Kenya!" Tungefanya nini?

Jamani tunawaumiza ndugu zetu wa zenj, mimi naona wana madai ya msingi.

Pitia hizi pages uone, jinsi tulivyowarudisha nyuma hawa jamaa. Tunawatawala. Na hivi tunataka kuifuta serikali yao. Tuwaonee huruma, tuwatendee haki.

Tembelea hii page, halafu sikiliza siku wanajoin UN in 1963 halafu leo tunawaambia kuwa wao sio nchi bali ni ”kasehemu kadogo tu kama jimbo la Kawe”

Hapa unapata sauti

http://www.mzalendo.net/sauti/sheikh-mohammed-shamte-akihutubia-un

na hapa unapata transcript

http://www.zanzinet.org/journal/shamte_speech.html

Tuisome historia ya nchi yetu,jamani, hawa watawala wetu wanaturushia mchanga wa macho tu. Halafu tunaishia kwenye ushabiki. Tuipitie historia ya Tanzania, halafu turekebishe palipo na makosa.

Mimi ninachotaka tukitilie maanani ni kuwatendea haki na usawa Wazenj na sisi tuifufue Tanganyika ndani ya Muungano.

Mkataa asili yake…………….Mimi nataka niwe Mtanzania, Mtanganyika kama wao wanavyojiita Mtanzania, Mzanzibari

Nawasilisha.
 
Wewe unge suggest mfumo upi wa muungano mkuu? Inge kuwa vizuri ungetoa alternative yako kisha tuichambue.
 
hao ma yakhe wa zenj na wao ni wajanja wanaona mbali mwanangu!!!!utakuja kush tukizia hafla wamerejesha kiti chao ndani ya United Nation kama ilivyokuwa hapo awali baada ya kupata uhuru wao December 10/ 1963......wameshajitangaza tayari kama wao ni Taifa huru kamili la Zanzibar na mipaka yake...wamekula ngombe mzima bado kumalizia mkia tu ndio wanaougombania:A S-alert1:
 
Zanzibar from a sovereign nation to a region of Grand Tanganyika(Tanzania)- a step back-ward.

Baada ya kutembelea hizi sites, kwa hakika sasa ninaelewa kwa nini ndugu zetu wazanzibari wanapiga kelele ya kuwa hatuwatendei haki.

Kama sisi Tanganyika tungeungana na Kenya halafu wakatuambia "ninyi muwe mkoa wa Kenya!" Tungefanya nini?

Jamani tunawaumiza ndugu zetu wa zenj, mimi naona wana madai ya msingi.

Pitia hizi pages uone, jinsi tulivyowarudisha nyuma hawa jamaa. Tunawatawala. Na hivi tunataka kuifuta serikali yao. Tuwaonee huruma, tuwatendee haki.

Tembelea hii page, halafu sikiliza siku wanajoin UN in 1963 halafu leo tunawaambia kuwa wao sio nchi bali ni ”kasehemu kadogo tu kama jimbo la Kawe”

Hapa unapata sauti

http://www.mzalendo.net/sauti/sheikh-mohammed-shamte-akihutubia-un

na hapa unapata transcript

http://www.zanzinet.org/journal/shamte_speech.html

Tuisome historia ya nchi yetu,jamani, hawa watawala wetu wanaturushia mchanga wa macho tu. Halafu tunaishia kwenye ushabiki. Tuipitie historia ya Tanzania, halafu turekebishe palipo na makosa.

Mimi ninachotaka tukitilie maanani ni kuwatendea haki na usawa Wazenj na sisi tuifufue Tanganyika ndani ya Muungano.

Mkataa asili yake…………….Mimi nataka niwe Mtanzania, Mtanganyika kama wao wanavyojiita Mtanzania, Mzanzibari

Nawasilisha.

Mwanangu jionee huruma wewe na kizazi cha Tanganyika wazenj ingekuwa hawafaidi wangecheua angalia wanavyo faidika mawaziri wizara nyeti wabunge madiwani wauza nyanya masalo....wamejazana Tanganyika wakati wewe mtanganyika huna haki hiyo zenj
 
..Muungano unawabeba wa-Zenj kwa kuwapatia subsidies kibao at the expense ya wa-Tanganyika.

..hivi unajua kwamba mkazi wa Dar analipia umeme kwa gharama kubwa kuliko yule wa Zenj kwasababu Tanesco na Ewura wamelazimishwa na serikali iwe hivyo?

..kama wa-Zenj wana matatizo basi wayapeleke kwa viongozi wao ni siyo kutu-demonize wa-Tanganyika.

..Maalim Seif aliyekuwa kinara wa kushutumu wa-Tanganyika na muungano ndiyo huyo sasa katulia kama maji mtungini.

..kuna wengine walikuwa wakiita CCM kuwa ni "Catholic Church Movement" sasa leo wameungana nayo kuunda serikali ya mseto.
 
Hii asili inaanzia wapi? wakati wa mkoloni...au kabla ya mkoloni? Maana kabla ya mkoloni hapakuwapo 'nchi' inaitwa Tanganyika! Na kama unataka tuanzie kipindi cha mkoloni....unataka kutuambia hiyo ndio asili yetu?

Mimi ninachotaka tukitilie maanani ni kuwatendea haki na usawa Wazenj na sisi tuifufue Tanganyika ndani ya Muungano.

Mkataa asili yake…………….Mimi nataka niwe Mtanzania, Mtanganyika kama wao wanavyojiita Mtanzania, Mzanzibari
 
Hii asili inaanzia wapi? wakati wa mkoloni...au kabla ya mkoloni? Maana kabla ya mkoloni hapakuwapo 'nchi' inaitwa Tanganyika! Na kama unataka tuanzie kipindi cha mkoloni....unataka kutuambia hiyo ndio asili yetu?

Mkuu,

Utakapolijibu hili suali ,ndio pia utakuwa umepata jibu lako...uko tayari?

Juzi,tarehe 09.Disember.. tulisherehekea uhuru wa nchi gani?

Kama umefikiria Tanzania, Urudi tena darasani, ukajikumbushe historia na somo la uzalendo.

Jengine, Zanzibar iliungana na nchi gani kufanya Jamhuri ya muungano?

Vyenginevyo, nifundishe mkuu, jee asili yetu ni ipi? usinitajie kabila,,no.no..no...nchi yetu.
 
Jamani Tanganyika yetu ndiyo tuipiganie kwa sasa kwani haina serikali hivyo mambo yetu yanaongozwa na Wazenji. Kwa mfano waziri wa mambo ya ndani ni mzenji ! Pia tulikuwa na Rais Mzenji (MWINYI) ambaye alijali maslahi ya kizenji zaidi. Serikali ya Tanganyika ni muhimu kwa sasa!
 
Vyenginevyo, nifundishe mkuu, jee asili yetu ni ipi? usinitajie kabila,,no.no..no...nchi yetu.

Tanganyika ndio jibu la maswali yako yote mawili! Mtoa mada amegusia suala la asili...ndio nikawa najiuliza kama asili yetu kweli ni Tanganyika ya mkoloni?

Kabla ya mkoloni tulikuwa na makabila/koo na kila moja ilijua mipaka yao na kulikuwa na utaratibu wa kuongoza makabila hayo. Wakoloni 'waliunganisha' makabila na koo na maeneo ya ardhi mbalimbali kwa manufaa yao...na ndio hapo ukapata nchi inaitwa Tanganyika. Nyerere na Karume wao 'wakaunganisha' Tanganyika na ZnZ na kupata Tanzania.

Kwa kutambua hili ndo maana Nyerere alikuwa anasema dhambi ya ubaguzi itatutafuna....kwa sababu hii ishu ya asili ikiitizama sana haiishi!
 
Zanzibar from a sovereign nation to a region of Grand Tanganyika(Tanzania)- a step back-ward.

Baada ya kutembelea hizi sites, kwa hakika sasa ninaelewa kwa nini ndugu zetu wazanzibari wanapiga kelele ya kuwa hatuwatendei haki.

Kama sisi Tanganyika tungeungana na Kenya halafu wakatuambia "ninyi muwe mkoa wa Kenya!" Tungefanya nini?

Jamani tunawaumiza ndugu zetu wa zenj, mimi naona wana madai ya msingi.

Pitia hizi pages uone, jinsi tulivyowarudisha nyuma hawa jamaa. Tunawatawala. Na hivi tunataka kuifuta serikali yao. Tuwaonee huruma, tuwatendee haki.

Tembelea hii page, halafu sikiliza siku wanajoin UN in 1963 halafu leo tunawaambia kuwa wao sio nchi bali ni "kasehemu kadogo tu kama jimbo la Kawe"

Hapa unapata sauti

http://www.mzalendo.net/sauti/sheikh-mohammed-shamte-akihutubia-un

na hapa unapata transcript

http://www.zanzinet.org/journal/shamte_speech.html

Tuisome historia ya nchi yetu,jamani, hawa watawala wetu wanaturushia mchanga wa macho tu. Halafu tunaishia kwenye ushabiki. Tuipitie historia ya Tanzania, halafu turekebishe palipo na makosa.

Mimi ninachotaka tukitilie maanani ni kuwatendea haki na usawa Wazenj na sisi tuifufue Tanganyika ndani ya Muungano.

Mkataa asili yake…………….Mimi nataka niwe Mtanzania, Mtanganyika kama wao wanavyojiita Mtanzania, Mzanzibari

Nawasilisha.
mh! tehe! tehe! basi na mimi nataka niwe mhehe(Lilinga nchi aliyoongoza MKWAWA),mtanganyika, mtanzania. pia nahisi tanganyika ni muungano wa nchi kadhaa kama nchi ya wahehe iliyoongozwa na mkwawa,hivyo basi chi zote zilizounganishwa na mjerumani na kuifanya tanganyika nazo zinaumuhimu wa kutambuliwa kikatiba.
 
..Muungano unawabeba wa-Zenj kwa kuwapatia subsidies kibao at the expense ya wa-Tanganyika.

..hivi unajua kwamba mkazi wa Dar analipia umeme kwa gharama kubwa kuliko yule wa Zenj kwasababu Tanesco na Ewura wamelazimishwa na serikali iwe hivyo?

'Min fadhlaka huwa pundaka' Musisahau nyinyi wakati mulipofungiwa na IMF katika miaka ya 1978 onwards iliyowasave ni Zanzibar. Uchumi wa Tanganyika ulikuwa zero kama siyo minus, wakati uchumi wa Zanzibar ulikuwa very strong.

Mzee weenu kila alipokuwa anakwenda kukopa alikuwa akitoka kapa kwa kukataa sera za IMF.........
 
haya mawazo kwa zama hizi yamepitwa na wakati

mtu mwenye akili yake iliotulia kamwe hawezi kuwaza haya
 
Juzijuzi walidai kupitia mabadiliko ya 10 ya katiba ya zenj kuwa Zanzibar ni nchi, sasa kelele zote za nini?
 
Tanganyika ndio jibu la maswali yako yote mawili! Mtoa mada amegusia suala la asili...ndio nikawa najiuliza kama asili yetu kweli ni Tanganyika ya mkoloni?

Kabla ya mkoloni tulikuwa na makabila/koo na kila moja ilijua mipaka yao na kulikuwa na utaratibu wa kuongoza makabila hayo. Wakoloni 'waliunganisha' makabila na koo na maeneo ya ardhi mbalimbali kwa manufaa yao...na ndio hapo ukapata nchi inaitwa Tanganyika. Nyerere na Karume wao 'wakaunganisha' Tanganyika na ZnZ na kupata Tanzania.

Kwa kutambua hili ndo maana Nyerere alikuwa anasema dhambi ya ubaguzi itatutafuna....kwa sababu hii ishu ya asili ikiitizama sana haiishi!

Mkuu,

Mleta mada kaleta mada na kuonesha Zanzibar imerudi nyuma kihatua,kutoka nchi hadi mkoa. Katika hali ya kawaida , huikomboi nchi yako halafu unayeungana naye akwambie wewe si nchi.

Rudia kauli ya Pinda, bungeni na hadi hii leo kama alifanya kosa basi hajalisahihisha. Rudia kauli tunazozitoa humu JF, kuwa "kasehemu kadogo, kama jimbo la Kawe" hata hakifai kuitwa Mkoa ,wilaya tu"

Unaposema kuwa Nyerere na karume waliunganisha Tanganyika na Zanzibar kupata Tanzania, hiyo ni kweli na uongo.

Kama kumbukumbu zako ni sahihi jina halisi la nchi yetu ni Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Full stop.
Kilichofanyika baada ya hapo ndio huo tunaouita usanii, usanii haukuanza leo.

Kuna member hapa JF amesema jina Tanzania limetungwa na muhindi mmoja wa Tanga, Maana yake nini?
Kutunga au kuunda maana yake nini?
Muhindi alitutungia jina TANZAN na akasema hii IA ni nahau tu!

Kero ya jina refu, Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ndio iliyozaa ufupisho,Tanzania, Kwa hiyo ,mtoto wako akikuuliza, Mzee, Tanzania maana yake nini?
Jawabu sahihi ni ufupisho wa jina la nchi inayoitwa Jamhuri ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

Vyenginevyo, utakuwa unamdanganya kijana wako. Na hivyo ndio sisi, watanganyika ndivyo tunavyojidanganya na tunataka kuwadanganya na wengine. Mimi ni kama Rev. Mtikila katika hili sidanganyiki! Tanganyika ipo….. Na Zanzibar ipo na Muungano upo.

Still tuchukuwe hivyo utakavyo wewe, Tanzania ndio nchi yetu. Tuisahau Tanganyika yetu, kwa nini tukatae au tuone ni tishio Wazanzibari wanaposema ile ni nchi yao. Zanzibar ni nchi yao. Na ndio hapo hiyo mada inapogusia, Zanzibar kutoka nchi hadi mkoa. Au hulioni hilo.

Ukiniuliza mimi, mbona sisi hatuitaji Tanganyika? Au Tanganyika iko wapi?
Hapo ndio nitakujibu, sisi tunataka kujifanya kuwa ni watu tusio na asili. Kama tuliutafuta uhuru wa nchi yetu, tukaipata nchi yetu, ikawa na jina la Tanganyika, sasa kwa nini tuisahau? Iwe ni dhambi, uhaini kuitaja na kujifaharisha nayo?

Kwani hatuwezi kujafaharisha,kujivunia kwa kusema mimi ni mtanzania, mtanganyika?
Wazungu husema," I am European but Irish, or I am European but French"
Mtu anajivuna kwa yote.Inawezekana!

Mimi sijazungumzia ubaguzi, wala sijasema tuuvunje Muungano. Nimesema tuwatendee haki wazenj na nikisema hivi nakusudia kuwa.
Tuchukulie kuwa Tanganyika tuliungana na Kenya badala ya Zanzibar. Vipi sisi tungependa Wakenya wahusiane na sisi katika muungano huo?
Tukapata jina letu. Tankenia. Tungeliacha jina letu la Tanganyika kama sehemu ya muungano huo? Kama unanifahamu hapa, mkuu basi utangundua mimi sipiganii ,wala sitilii nguvu ubaguzi ila haki na usawa.

Lakini katika historia ya miungano, ulikuwepo muungano wa sovieti, Yugoslavia,
Senegambia. Unataka kuniambia hujuwi kilichotokea kwa miungano hii? Ilichukuwa miaka mingapi hadi kusambaratika? Misingi yake haikuwa imara, mbona US kwa kuazima mfano wa Mzee Mwanakijiji mbona bado upo? Jawabu, Misingi yake imara.!

Mungu aepushe hili la kuvunjika muungano na sisi wenyewe tufanye juhudi tusiwe kichocheo wa kutokea hili,tutende haki.
Lakini tuchukuwe mfano kwa mantiki ya hoja tu, jee likitokea utaniambia kuwa tutaliita pande letu la ardhi Tanzania bara?

Ombi kwako na wanaJF

Kama una habari za kutosha naomba unifungue macho.

Jee Tanganyika ilipata kuomba na kukubaliwa kuwa mwanachama wa UN ?
Kama ni yes, kuna yeyote aliye na hutuba ya mwakilishi wa sovereign Tanganyika, akilishukuru baraza la UN kwa kupatiwa kiti ? kama ipo tuingizie humu ili tufunguane macho.
Pia kwa nini, Kenya na Zanzibar waliomba wakati mmoja na kukubaliwa kwa wakati mmoja ?
Kilitokea nini kwa nchi yetu, Tanganyika?

Tafadhali, kwa yeyote aliye na mwenge, tochi, atumulikie, tupate mwanga, tupate kuona.
Kama hakuna mwenye mwenge basi japo wa kuazima,ule mwenge wa uhuru.

Nilijiunga JF ili kujifunza.!
 
Last edited by a moderator:
mzalendo.net? MMhm!

Mkuu,

Nimesoma uhuru na mzalendo sana (propaganda tupu), sasa naangaza kila sehemu, kila kona, kipembe, huo ndio utandawazi aliosema Mzee Ben. Elimu huchotwa popote, Mkuu.

Huko ….net pia nachambua, nachakuwa, sibwagii tu! simezi bila kutafuna! Ndio nimesema nimegundua kuwa jamaa wana madai ya msingi wakati mwengine wanapolalamika.
Nchi zipapoungana si kweli kuwa zina-cease to exist. They join with a purpose, bigger purpose siyo kutoka nchi kuwa mkoa.. Au vipi?
 
Juzijuzi walidai kupitia mabadiliko ya 10 ya katiba ya zenj kuwa Zanzibar ni nchi, sasa kelele zote za nini?

Mkuu

Habari zako? Habari za mapumziko?

Sasa mkuu, wewe saa zote unakuwa umekasirika,umenuna? pia huwa una majibu ya mkato mkato tu?
Tuelimishe! Usifanye uchoyo kwenye kutoa elimu.

Kweli wamefanya hayo, lakini ni sisi huku Tanzania bara(Tanganyika) ndio tunaopiga kelele, mayowe na kupaza sauti kuwa wamevunja katiba yetu!!

Punguza ukali, mzee.

Jee utanzania umetusaidia vipi kuondosha ujinga, ufisadi na umasikini? Hata tuukatae utanganyika wetu?
Bado ninasubiri majibu, Mkuu.
 
Zanzibar from a sovereign nation to a region of Grand Tanganyika(Tanzania)- a step back-ward.

Baada ya kutembelea hizi sites, kwa hakika sasa ninaelewa kwa nini ndugu zetu wazanzibari wanapiga kelele ya kuwa hatuwatendei haki.

Kama sisi Tanganyika tungeungana na Kenya halafu wakatuambia "ninyi muwe mkoa wa Kenya!" Tungefanya nini?

Jamani tunawaumiza ndugu zetu wa zenj, mimi naona wana madai ya msingi.

Pitia hizi pages uone, jinsi tulivyowarudisha nyuma hawa jamaa. Tunawatawala. Na hivi tunataka kuifuta serikali yao. Tuwaonee huruma, tuwatendee haki.

Tembelea hii page, halafu sikiliza siku wanajoin UN in 1963 halafu leo tunawaambia kuwa wao sio nchi bali ni "kasehemu kadogo tu kama jimbo la Kawe"

Hapa unapata sauti

http://www.mzalendo.net/sauti/sheikh-mohammed-shamte-akihutubia-un

na hapa unapata transcript

http://www.zanzinet.org/journal/shamte_speech.html

Tuisome historia ya nchi yetu,jamani, hawa watawala wetu wanaturushia mchanga wa macho tu. Halafu tunaishia kwenye ushabiki. Tuipitie historia ya Tanzania, halafu turekebishe palipo na makosa.

Mimi ninachotaka tukitilie maanani ni kuwatendea haki na usawa Wazenj na sisi tuifufue Tanganyika ndani ya Muungano.

Mkataa asili yake…………….Mimi nataka niwe Mtanzania, Mtanganyika kama wao wanavyojiita Mtanzania, Mzanzibari

Nawasilisha.

Inamaana MBUNGE wao ni Hon. Mdee?

Kweli hili JIMBO ni kubwa ni wakati wa kulimega maana aiwezekani hii!
Inamaaan NEC hawaoni?
 
Back
Top Bottom