Zanzibar kupiga marufuku ndizi toka Tanzania bara

RANCO TZ

Member
Aug 26, 2014
23
11
Leo zimezuiwa ndizi zenye thamani ya Tzs 5,000/= Maafisa wamesema serikali imezuia uingizwaji wa ndizi toka bara sababu kuwa zina wadudu wanaosababisha maradhi. Hajafafanua maradhi hayo aina gani.

Hivyo nimelazimika kuziacha bandarini chakula changu pendwa ndizi Bukoba. Naishauri Serikali ya Zanzibar kutoa taarifa na kubandika taarifa hizo katika kuta za matangazo bandarini Dar es Salaam and Zanzibar.

Ajabu ni kuwa wakati natoka nje ya bandari naona kuna Wazanzibar wameshikilia ndizi mzuzu kutoka bara na hawajazuiliwa. Nilitaka kuwauliza walikuwa wakali sana.

Naomba kama kuna wataalam wa afya au mwenye taatifa hizi za kiafya anipe faida nami na familia yangu tupate kuzifaham
 
Bara nayo ijibu mapigo kwa kuzuia ubuyu, hiriki, karafuu, mwani, na mdalasini kutoka Zanzibar, vina fungus.
 
Ikimaliza ihamie kwenye malashi na vipodozi vinavyopitia Zanzibar kuja bara, vina viambata vya sumu.
 
Back
Top Bottom