Zanzibar : kulibariki Azimio la Arusha si kuitusi kauli ya Karume

Baraghash

JF-Expert Member
Dec 18, 2012
2,713
1,789
"Rais Karume ameuwawa na kuzikwa ... , kilichozikwa ni kiwiwili chake tu....mawazo ...hekima ......busara........zitaendelea kubaki palepale.....", ni slogan katika miaka '70 ambayo utaikuta kila chumba kwenye kwenye ofisi zote za Zanzibar.

Nyerere alipolibuni Azimio la Arusha alilitaka kutapakaa nchi nzima. Hivyo alimwita Sheikh Karume muasisi mwenzake, kuiuza ndoto yake hiyo. Karume alimkubalia kama kawaida yake kwa " kauli" huku akibaki kutafakari. Karume aliitisha mkutano wa hadhara kutueleza wananchi kuhusu Azimio la Arusha na akatutaka kuliunga mkono.

Baada kuona utekelezaji wake na kuona maudhui ya Azimio linakwenda kinyume na maadili, imani na desturi za wazanzibar aliitisha mkutano mwengine wa hadhara

Katika mkutano huo Karume aliwaeleza "wana wa nchi" kama anavyo penda kuwaita na kutanabahisha ubaya wa Azimio la Arusha na kulipiga marufuku kuingia Zanzibar, na kama atatokea mtu ataiunga mkono falsafa hiyo ya Azimio, basi iwe MWISHO CHUMBE. Na akatuusia kuwa wazanzibari lazima wawe na KHATIMA....KHATIMA ...KHATIMA. Kauli hiyo ambayo inapaswa kuendelea kuheshimiwa na kila mpenda Mapinduzi na muadilifu.

Hivi sasa wamejitokeza baadhi ya watu , hususan, " wakuja" wa CCM na kuitumia hotuba yake ya kwanza kuhusu AZimio kujenga hoja ya kulitaka kulirejesha Azimio la Arusha Zanzibar Je, wazanzibari mnakubali kutia ulimi puani mwenu? ????
 
Mwingiliano wa Azimio la Arusha ni kwamba lilifia na kuzikwa Zbar! Sasa kuna Azimio la Zbar ambalo ni kinyume na Azimio la Arusha!
 
Tukiwataja wapenda mapinduzi na Marehem Karume anaingia kweli!!?

Field Marshal John Okello ndie mwana Mapinduzi hasaa.

Mzee Karume alikua ni kiongozi tu wa chama, hapo nyuma kuna mambo chungu tele ambayo ukiyaweka hapa itakua shida...
 
Back
Top Bottom