Zanzibar - Kodi na Mapato VS Muungano. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar - Kodi na Mapato VS Muungano.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Sikonge, Nov 21, 2008.

 1. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #1
  Nov 21, 2008
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wachangiaji,
  Nimekuwa napita na kusoma kuwa Tanganyika imekuwa ikiibia pesa Zerikali ya Zanzibar. Misaada ikija kwa Tanzania, inapelekwa Tanganyika tu. Pesa za kodi zikikusanywa na Wazanzibar, zinapelekwa Wizara ya fedha ya Muungano na wao hawapati kitu. Pesa za utalii, karafuu nk zinakusanywa na zinapelekwa Tanganyika na kuwa za Muungano. Hapo wao hawapati kitu kwani serikali ya Muungano ni kwa Tanganyika tu na serikali ya Zanzibar inabaki kujihangaikia kutafuta visenti vyake vyenyewe. Kama ni kweli basi kweli Zanzibar wameonewa na kuibiwa kwa miaka 40. Na kweli inasikitisha.
  Maswali yangu hapa ni kama ifuatavyo:-
  1: Hivi tunachangia wizara ngapi?
  2: Hizi wizara ambazo hazimo katika Muungano, je wanagawana vipi majukumu? Tuseme wizara ya Utalii, ipo ya Zanzibar na Muungano. Hawa jamaa kazi zao zikoje?
  3: Kama wizara ya fedha tunachangia, kwa maana hiyo hata TRA tunachangia sasa Zanzibar wakikusanya pesa zao kodi zinakwenda wapi?
  4: Wizara zisizo katika Muungano yaani zipo Zenji tu, je wanapata wapi fedha kujiendesha?
  5: Wizara za Muungano, zinalipiwa na Watu wote au ni Watanganyika tu (ukiacha ya fedha). Hapa tuseme Wanajeshi, Polisi, magereza, Mabalozi nk.
  6: Mgawanyiko wa fedha ukoje? Hapa ni hii wizara ya fedha.

  Naomba kama mchangiaji atakuwa na ya kuongeza basi ntashukuru sana. Nataka kujua kwa nini tugawane mafuta. Kama hii itakuwa ni pato la taifa basi si kuwa pesa zinakwenda Wizara ya fedha na huko tunagawana wote? Kama fedha za Madini, Gas, Utalii nk zinakwenda TRA na huko tunagawana wote, kwa nini Wazenji wanasema wao hawapati? Wizi huo hutokea wapi? Pia kama Gas ikishaanza kutumika majumbani, Tanzania bara wananchi si watauziwa? Mafuta hata kama yakipatikana Zanzibar, sisi wananchi wa kawaida si tutauziwa? Fedha zote zinakwenda katika kapu moja. Naomba ufafanuo wa hayo maana naona naelewa vitu nusunusu au sielewi kabisa.

  MODS: Naomba muiache kwa muda na baadaye ichanganye kwenye ile ya Mtaalam aliyedai ZNZ hakuna mafuta akabidhi ripoti kwa SMZ!!
   
 2. F

  Fundi Mchundo JF-Expert Member

  #2
  Nov 21, 2008
  Joined: Nov 9, 2007
  Messages: 4,706
  Likes Received: 61
  Trophy Points: 145
  Hivi mpaka kati ya Jamhuri ya Muungano na Zanzibar uko wapi? Mpaka kati ya mkoa wa Pwani na Zanzibar, Mkoa wa Tanga na Zanzibar uko wapi? Tutajuaje hayo mafuta ya off-shore yako Zanzibar au kwenye JMT? Na jurisdiction ya Zanzibar katika international water iko wapi? Je hao pirates wakisomali wakivamia meli nje ya zanzibar ni nani mwenye wajibu wa kupambana nao? KMKM au JWTZ?

  Sasa kama kuna mpaka kati ya JMT ( ambamo Zanzibar imo) na Zanzibar, huo Muungano uko wapi?
   
Loading...