Zanzibar: Katibu wa ACT-Wazalendo mbaroni kwa tuhuma za kuwashambulia kwa mapanga wanachama wa CCM

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,644
2,000
Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linamshikilia Katibu wa Chama Cha ACT Wazalendo Tawi la Kosovo Shehia ya Kangani Hassan Hamad Hassan mwenye umri wa miaka 56, kwa tuhuma ya kuwashambulia kwa kuwakata mapanga wanachama wa Chama Cha Mapinduzi akiwemo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Wete.

Kamishna wa Polisi Zanzibar Mohammed Haji Hassan ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya polisi mkoa wa Kaskazini Pemba ambapo amesema inadaiwa kuwa mtuhimiwa huyo baada ya kutekeleza kitendo hicho alikimbia na kujificha na kwamba amelazimika kujisalimisha kituoni baada ya kutafutwa kwa siku kadhaa.

Aidha amesema baada ya Jeshi la Polisi kufanya upekuzi kwenye nyumba ya mtuhumiwa walikuta baadhi nyaraka zinazoonyesha kwamba huyo ni mwanachama halali wa chama Cha ACT Wazalendo nyaraka hizo ni pamoja na kadi yake ya uanachama yenye namba 438052 iliyotolewa ya tarehe 20/3/2019 wadi ya kiuyu Jimbo la Kojani.
 

mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
3,745
2,000
Si walisema kijana aliingia msikitini kukatakata hao wasaliti?
Leo wanakamata mzee wa 56 yrs,kuweni seriaz basi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom