Zanzibar iwe kitovu cha Kiswahili kwa Afrika Mashariki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar iwe kitovu cha Kiswahili kwa Afrika Mashariki

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by GHIBUU, Mar 17, 2011.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  MWISHONI mwa wiki Waziri wa Elimu wa Zanzibar Ramadhan Abdullah Shaaban alikuwa mgeni rasmi katika shughuli ambayo imepewa jina la Siku ya Kiswahili ambayo kwa hakika ilifana sana.


  Hii ilikuwa ni siku ya kuwaenzi na kuwakumbuka waandishi na wasanii wa Zanzibar na ambao ktika kazi zao kwa njia moja au nyengine wamesaidia katika kuikuza lugha ya Kiswahili katika mawanda yake yote.


  Hii ni shughuli ambayo iliandaliwa na Baraza la Kiswahili la Zanzibar (BAKIZA) katika kutimiza jukumu lake la msingi la kuhimiza makuzi ya lugha ya Kiswahili, lugha ya taifa ya Zanzibar na Tanzania.


  Hii ni mara ya pili Siku ya Kiswahili kufanyika na tayari mipango
  imekamilika kuifanya siku hiyo kuwa ya kudumu kwa maana ya kufanyika kila mwaka na kuenea katika jamii.
  Wataalamu wa Kiswahili na wasanii walioenziwa katika hafla hiyo
  walikuwa ni Seif Salim Saleh aliyekuwa mshairi, mchoraji na pia mtunzi wa muziki wa taarab na aliyekuwa na kipaji cha juu kabisa cha kuimba.


  Mwengine alikuwa ni Maalim Ameir Issa ambaye alikuwa ni mtaalamu wa fasihi na mwandishi aliyebobea na sehemu kubwa ya maisha yake ilikuwa ni kwenye utafiti wa fasishi ya Kiswahili na alitoa mchango wake katika kazi kadhaa ambazo zimechapishwa na Taasisi ya Kiswahili na Lugha za Kigeni.


  Halafu ikawa zmu ya maehemu Maalim Haji Chum ambaye alibobea katika utafiti na mchango wake mkubwa ulikuwa kwenye kutengeza kamusi ya lahaja ya Kimakunduchi na huku akifanya tfiti kadhaa za utamaduni unaombatana na Mswahili na lugha yake ya Kiswahili.


  Kisha ikawa ni zamu ya msanii Ali Omar Baramia ambaye fani zake ziilikuwa ni uimbaji wa taarab lakini sehemu kubwa ya maisha yake yeye alistaaladhi katika utunzi wa mashairi ingawa yeye kama Seif Salim Saleh na Maalim Ameir Issa hawakubahatika kuacha machapisho yoyote yao wao moja kwa moja.


  Lakini msanii aliyepewa heshima kubwa kwa siku hiyo alikuwa ni
  Muhammed Said Abdullah maarufu kama Bwana Msa, jina ambalo alilibuni kuwa muhusika wake mkuu katika hadithi zake kadhaa ambazo karibu zote zilikuwa ni za kiupelelezi lakini kama kawaida ya watunzi wa Zanzibar zilishiba na hata kurishai lugha bora na fasaha.


  Waziri Shaaban alizindua kitabu kilichokusanya kazi mbali mbali za uchambuzi wa vitabu na falsafa za mwandishi huyo kutokana na juhudi iliyofanywa na BAKIZA katika mchango wake wa kujivunia machapisho yanayoendeleza Kiswahili ambapo mwaka jana tu ilichapisha Kamusi ya Kiswahili Fasaha.


  Waziri pia siku hiyo alizindua kitabu kingine cha mashairi
  kinachokwenda kwa jina la NENO ambacho kimeandikwa na mwandishi wa habari wa Zanzibar Ally Saleh.


  Katibu Mtendaji wa BAKIZA Khadija Bakar alitoa wito wa kazi za wasanii wa Zanzibar kukubalika katika kutumika kwenye mitaala ya kiwango cha Kidato cha Nne na Kidato cha Sita na kwa hivyo kutahaniwa kinyume na ilivyo hivi sasa, na wito huo pia kuelekezwa kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuthamini kazi za waandishi na wasanii wake.


  Waziri Shaaban alilalamikia kushuka kwa matumizi ya lugha ya Kiswahili kwa vile utafiti wa lugha hiyo umepungua sambamba na kuwepo na uhaba wa kazi za kifasihi zinazochapishwa kila mwaka.
  Alisema kwa fikra zake kuna haja ya kuongeza mashirikiano ya nchi za Afrika Mashariki katika kukuza na kusukuma matumizi ya lugha hiyo ambayo ni kiungo kizuri cha kuunganisha nchi hizo.
  Lakini pia alisema nchi za Afrika Mashariki lazima ziwe na mikakati mikubwa zaidi ya kutumia lugha ya Kiswahili katika kujiletea maendeleo kama vile nchi za Asia ya mbali zilivyofanya.


  Alitaja mifano ya China, Kora, Japani na nyenginezo ambazo zimepiga hatua na kubadilisha nchi zao baada ya kufanya maamuzi ya makusudi ya kutumia lugha zao mama katika kuendesha mafunzo hata ya kisayansi.


  Utajiri wa lugha ya Kiswahili ukikusanywa kwa pamoja na kupewa nguvu ya pamoja baina ya nchi tano za Afrika Mashariki zenye watu millioni 120, basi ni wazi ukubwa wa soko hilo utaimarika maana maendeleo ya eneo lolote lile idadi ya watu ina umuhimu mkubwa kama dhana za uchumi zinavyoelekeza.


  Lakini hili la kukuza Kiswahili na kuwa lugha ya kufundishia hata
  sayansi na masomo yote, Tanzania ina wajibu wa kushika nafasi ya uongozi kwa vile nchi yake ina wasemaji wengi zaidi na pia ina miundo mbinu mingi zaidi ingawa Kenya nayo haiko mbali.
  Historia ya Tanzania inaonyesha inaweza kuchukua uongozi huo hata leo na kwa hivyo ni muhimu Tanzania ikajitayarisha.


  Ni lazima wana Afrika Mashariki wakubali na wajenge nia ya kisiasa ya kujivua katika minyororo miwili ya na mgando wa mawazo. Kwanza ni kuona lugha za kigeni kama Kifaransa na Kiingereza ndio suluhisho ya mfumo wetu wa ufundishaji na kwa hivyo pole pole kusoma lugha hizo kama lugha lakini sio kufanywa lugha za kusomeshea.
  Pili ni muhimu kuweka pembeni utumwa usio wa lazima wa kuendekeza lugha zetu za asili kwa hasara ya kuwa na lugha moja itayoweza kutuunganisha Afrika Mashariki nzima. Kama kila nchi itaendeleza mgawiko wa lugha ziliomo ndani ya nchi yake na kuuleta mgawiko huo katika picha kubwa ya Afrika Mashariki lugha ya Kiswahili haitapata nafasi hata siku moja.


  Kwa hivyo sisi tunaouona wito wa Waziri Shaaban ni muhimu lakini unaofaa kupita maneno na ufanyiwe vitendo na hata kuwekewa muda wa kufikiwa lengo kuu lake, hata iwapo muda huo utakuwa mrefu lakini muhimu uwe unaoweza kufikiwa tena kwa mafanikio.
  Misingi tayari imeshawekwa na viongozi wa Afrika Mashariki na sasa kama Waziri Shaaban ameliona hili basi pia naamini anajua ni wajibu wa viongozi wa kiwango chake katika kanda hii kutekeleza misingi hiyo iliotandikwa kwa kuwapanga watendaji wao.
  Kwa mfano Zanzibar inaweza kuandaa mkutano wa mabraza yote ya Kiswahili ya Afrika Mashariki na kuitandika mezani hoja hiyo ya Waziri Shaaban na kuisikilizia mlio. La sivyo kama Zanzibar haitochukua nafasi hiyo kwa niaba ya Tanzania kila siku itakuwa ngoja ngoja na Waswahili walisema zamani kuwa huumiza matumbo.
  Zanzibar imeshakuwa mfano wa mambo mengi na katika medani mbali mbali katika Afrika Mashariki na kwa hili pia inaweza kuwa mfano, lakini kwa Tanzania na Afrika Mashariki kuiwezesha.


  Tangu awali Kiswahili cha Zanzibar killichaguliwa kuwa ndio kitumike Afrika Mashariki na umefika wakati kwamba Tanzania isilionee haya hili na ilisimamie kwa nguvu zote.
  Wakati umefika wa Zanzibar kutangazwa kuwa ni kituo kikuu cha Kiswahili cha Afrika Mashariki ( Centre of Excellence for Kiswahili Language) na hilo liwe kwa vitendo na sio maneno. Hilo liwe ni jukumu muhimu kwa Tanzania, maana Zanzibar kama Zanzibar haina sauti katika Jumuiya ya Afrika Mashariki
   

  Attached Files:

 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Apr 2, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Sio iwe, Zanzibar ni kitovu cha kiswahili duniani.
   
Loading...