Zanzibar iungwe na Bara kwa Daraja - Wazo Jipya

Mzee Mwanakijiji, nimeipenda sana hii na Mungu ashushe baraka zake iwe kweli (my wishful thinking). Wana JF wamechangia mengi ya kisiasa bila kuangalia upande wa uchumi. Tukiwa na daraja hatutosubiri meli kupeleka viazi, nyanya, vitunguu, nk kwenda Znz tutakuwa tunatumia pikipiki za TOYO au pickup, na kwa namna hiyo maisha yanakwenda.
Ila, hilo daraja itakuwaje ikitokea Tsunami?
 
Mimi nawaambia tungekuwa na viongozi kweli wenye maono ya kuthubutu, uthabiti wa vitendo na siyo "tutafikiria na kupanga mchakato" tungeweza kujenga Kigamboni (miaka kumi iliyopita) na la Zanzibar lingekuwa tayari; tungekuwa tayari tumejenga Stielger's Gorge dam badala ya hivi vya 20MW na 100MW plants! Stielger's ilipokaridiwa wakati ule ingegharimu dola bilioni kama 2 hivi! kiasi ambacho tunakipoteza kwa ufisadi every two years or so.

Hivi, mmesahau mambo ya opportunity cost? Gharama ya kweli ukiangalia siyo ya vile ambavyo tunafikiria tumevifanya!!
 
yakhe unataka daraja la znz hadi OMAN nini...?! maana nyie wa znz Diaspora mnatamani muarabu arudi kama kesho awatawale ... haha! mnamawazo ya kitumwa sana seriously! hadi kichefuchefu mnavyowaona miungu waarabu.. tanganyika tunamlinda muungano hautovunjika wa znz bar weusi hawapo radhi kuwa watumwa waarabu
WEWE pimbi kweli,hivi njaa mulio nayo mujenge daraja kwa maantiki gani ? 1Trilion mutazirejesha vipi ? Kwa business gani tuliyonayo baina ya tanganyika na zanzibar ? Kama muungano huu basi hauko mbali kuuvunja kwa sababu ile misingi ya muungano imeshavunjika.

Tanganyika haipo ambaye ndio mshirika wa muungano.
Rais wa zanzibar sio tena makamo wa muungano wa kwanza.

Hivyo ndivyo vizingiti au nguzo za muungano,na huyu makamo aliopo sasa anaiwakilisha vipi zanzbar ? Wakati wananchi wa zanzbar hawajampigia kura,ispokuwa kateuliwa tu kichama na kikwete,kwa vile kamuonea huruma alikosa nafasi ya kugombea usrais ?

Nafikiri mtoa mada angeleta hoja kuwa hilo daraja lijengwe kutoka pemba kuelekea unguja kwa vile ni taifa moja la wazanzbari basi ingeleta maana, lakini sio tanganyika.

Muungano soon bye byee .
 
Kujitambulisha muhimu hapa duniani mkuu... no footprint, no recognition! Simple as that. Hebu jiulize kwanini Mh. Rais wetu alienda kujitambulisha kwa Bush na Obama mara baada ya kuchaguliwa?? Au kwanini kuchwa kuta anapiga misele akipishana angani kwa ajili ya kuwafata huko huko na bakuri letu... pangelikuwa na makubwa hapa si wangelikuja wenyewe!! Au nchi zinazojijengea man-made wonders zimeanza kukosa soko la watalii siku hizi??! Kitu kinaweza kujengwa sasa hivi lakini manufaa yake yakawa miaka 50 ijayo... hata hivyo hii si hoja sana; hoja iliyopo hapa kwa maoni yangu ni kule kuweza kuwaza/kufanya makubwa kwa ajili ya manufaa ya vizazi vijavyo... siyo kila jambo liwe kwa ajili ya miaka mitano mitano tu na kushinda chaguzi ndani ya miaka hiyo!! Maana ahadi na mipango mingi ya CCM kwa miaka mingi sasa imekuwa ya aina hii!!! Marekani na Urusi walianza kwa kujitambulisha kwa kurusha vifaa angani, leo hii faida za kujitambulisha huko twaziona kila kona na kwa kila mtu mwenye kimobiteli!!!

Narejea tena kuwa binaadamu anapenda raha na anaikosa kwa kutokuwa na uwezo> Hivyo unakuita alikofanya Kikwete ni kujitambulisha au kujieleza kuwa tuna shida. Huko kote alikokwenda wanajuwa kuwa sisi tuna shida sasa anamtambulisha nani?

Kwa upande wapili hawa ndugu zetu wa China ndio wanajitambulisha na ukifatilia vyombo vya habari vya Magharibi utafahamu nini nazungumza!
 
We cant Even Walk..... Now you want us to RUN...?

Lack of maintenance, wizi, uchakachuaji this might end up falling down and causing a catastrophe.. Please Boats will do fine for now
And that Money itengeneze barabara za kawaida mpaka vijijini ili nafaka ziweze kutufikia mijini kwa bei nafuu
 
Yaani nimependa jibu lako hadi nimecheka moyoni; kwa hiyo mtaanza kujenga daraja mkisha kuwa na tatizo na usafiri wa majini na wa ndege. Hadi msongamano wa magari utokee ndio mnafikiria kupanua barabara, hadi kina mama walale sakafuni baada ya kujifungua ndio mnafikiria kuongeza vyumba na huduma Temeke? Hadi watoto walundikane kwenye mashule ndio shule za kata zinapokuja, na hizo shule hadi hivi sasa zijae matatizo ndio watu wataanza kutafuta suluhisho. Hadi majumba yajengwe ovyo bila kufuata taratibu ndio magenius wetu waanze kuja na kampeni ya bomoa bomoa. Of course hakuna tatizo la usafiri sasa hivi katika ya Zanzibar na Dar si yapo maboti yaendayo kwa kasi? Hivi ikijengwa barabara kati ya bara na visiwani volumu na speed ya watu na vitu inaweza hata kulinganishwa na hali iliyopo sasa? Kweli mnafikiria Uchumi wa Zanzibar utakuwa ulivyo tena?


Jibu lako kwa kweli linawakilisha fikra za watawala wetu walioshindwa.
Niamini kabisa kuwa nimepigwa butaa na unachokisema. Wewe ulijichekea moyoni lakini mimi nimeanza kupunguza kile nilichokifikiria juu yako.
Hivyo binaadamu hufanya kitu tu bila kupima umuhimu wake? Hivyo huu usafiri uliopo sasa hauna maana? Na kwa akili yako inayoona mbali fikira zako zinakutuma kuwa huu usafiri wa sasa hauwezi kukua kulingana na mahitaji kila yakiendelea? Hivyo usafiri wa sasa sio suluhisho la tatizo la usafiri isipokuwa iweko daraja ndio utakuwa usafiri ?

Mbona mfano wa Hospitali na kitu chengine chochote ulichojaribu kukileta haviowani? Tatizo la Hospitali litamalizika kwa kuongezwa kwa Hospitali kila panapohitajika na wala hakuna kitu mbadala Zaidi ya Hospitali lakini usafiri kwa hili la Zanzibar na Bara lina mbadala na iwapo kimoja wapo kama ilivyo sasa kwa Boti na Ndege vinatosheleza kuna haja gani ya Daraja? Tatizo lako mwenzangu ni kuwa uko selfright kwamba unachoona wewe ni bora basi ni ultimate.
 
yakhe unataka daraja la znz hadi OMAN nini...?! maana nyie wa znz Diaspora mnatamani muarabu arudi kama kesho awatawale ... haha! mnamawazo ya kitumwa sana seriously! hadi kichefuchefu mnavyowaona miungu waarabu.. tanganyika tunamlinda muungano hautovunjika wa znz bar weusi hawapo radhi kuwa watumwa waarabu

Unajuwa ule msemo wa domo kubwa kula kwa jirani? Si mgeanza kujenga madaraja ya kwenu kwanza ndio muingilie kwa ndugu.
Kwani wewe kama wewe unaumwa na nini iwapo Wazanzibari wameamuwa mabwana tofauti na wenu nyie? Ndio tunapenda vya Waarabu bahati mbaya hatupendi vya Wazungu kama nyinyi.
 
Ni wazo zuri lililochambuliwa kwa makini lakini nadhani siyo la lazima sana katika mazingira ya leo. Kwa maoni yangu nadhani tungejenga tunnels pana za kuunganisha visiwa hivi badala ya madaraja hasa kwa vile madaraja yanaweza kukatizwa na majambazi wa majini (pirates) na kusababisha usumbufu kwa watumiaji.

Hili la wachina ni kwa sababu tu ya kutaka kuwapiku wabaya wao wa asili, yaani wajapani, amabo wanajulikana kwa kuunganisha visiwa vyao kwa madaraja. Walifanya hivyo kwenye bullet train, na sasa wamekamilisha kwenye madaraja. Bado wanashughulikia kwenye utengenezaji wa magari kusudi waje waipiku Honda na Toyota pia

Great thickers think alike!
 
Nadhani unajua kabisa kuwa kujengwa kwa daraja la kuunganisha bara na visiwani (by the way visiwa vya Zanzibar vilikuwa vimeunganishwa na bara katika zama hizoooo) kutakuwa ni kurudisha muungano wa asili wa maeneo hayo. Lakini zaidi itaondoa na kufuta wazo la kujificha kama visiwa "Zanzibar yetu" kwani hatimaye Zanzibar itaunganishwa na bara ambayo ni asili yake. Hili linakuogopesha, kwani Muungano utakuwa siyo tu wa kisiasa bali physically! what a pyschological blow to the separists of Zanzibar.


Illussions zako zisikufikishe mbali usikoweza kurudi. Kama kuichukuwa Zanzibar kwa nguvu hakuna haja ya hilo daraja kwani hata kama mtaamuwa nyote muwe Waislamu na mfunge kwa mwaka mzima hamtokuwa na uwezo wa kulijenga hilo darajka. Jeshi mnalo kwanini hamvamii tu?
 
Kama akili za watanzania ni hizi basi maendeleo yako mbali.

Mwanakijiji hongera kwa wazo hili zuri kwani lina moyo wa uzalendo na mie leo nilipokuwa naaangalia taarifa ya habari nilipoliona hilo daraja likifunguliwa nilikuwa na wazo kama lako. Kuhusu muungano usiwapo au ukiwepo daraja lina umuhimu kwa nchi mbili hizi. Mfano zanzibar wakichimba mafuta usafirishaji wa mafuta kuja Tanzania bara kwa barabara ni rahisi zaidi kuliko kutengeneza bomba la kupita chini ya bahari kupeleka mafuta bara. Pia gharama za usafiri zitapungua. Qatar wana daraja linawaunganisha wao na Saudi Arabia wakati nchi hizo ni nchi mbili tofauti (Tuache mawazo ya mgando!!!!).

Hofu yangu ipo katika gharama za ujenzi na umakini wa ujenzi wenyewe. Kumbuka Tanzania iko katikati ya pande la ardhi ya africa na bahari ya hindi kukitokea tetemeko la ardhi usalama wake ukoje? Pia sote tunafahamu jinsi ufisadi ulivyoenea Tanzania daraja la $1 million utakuja kukuta linafika $100 million je watadhibiti vipi gharama za ujenzi ziwe hiyo $1.5 Billion.

Mie naona kama wazanzibari wanaweza kujenga hili daraja na sio sisi wadanganyika. Maana wao kidogo wana uzalendo kama unavyoona walivyoshughulikia suala la posho bungeni angalau unapata matumai kuna moyo wa uzalendo bungeni. Sio kwetu tanganyika.

Naona unajigongagonga! Hayo unayoyafikiria ndio yanayofanya kuwa hili daraja halina umuhimu wowote. Hao waliojenga daraja wako tofauti na sie kwa kila upande na ndio maana kuwa Hili wazo la Mwanakijiji halina maana kwetu. Sababu kubwa kuwa hatuna uwezo na tuna mambo yaliyo muhimu ambayo mwenyewe ameyaeleza alipokuwa akijaribu kujitetea huko juu.
 
Back
Top Bottom