Zanzibar itatawaliwa na Wazanzibari - Seif Sharrif | Page 2 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar itatawaliwa na Wazanzibari - Seif Sharrif

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 23, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 23, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Niliuliza hili swali huko nyuma kuwa Mzanzibari ni nani? sikupata jibu zuri la kiakili. Baada ya kumsikia Seif akiapa kuwa "hatatoka mtu mahali popote duniani kuja kutawala Zanzibar na kuwa Zanzibar itatawaliwa na Wazanzibari" nimeshindwa kuelewa anaposema "Wazanzibari" anamaanisha watu gani?

  a. Wananchi wanaoishi Zanzibar na ambao wametimiza masharti ya ukazi ya Zanzibar hata kama kinasaba hawana asili ya Zanzibar?

  b. Wananchi wa Zanzibar ambao wanahistoria ya muda mrefu huko Zanzibar hata kama wako nje ya eneo la jiografia la Zanzibar?

  c. Wazanzibari kama watu wenye kuamini na kuitamani nchi iliyokuwepo kabla ya Uhuru wa Mwingereza?

  d. Wazanzibari waliokuwa chini ya uongozi wa Serikali ya kwanza ya Shamte kabla ya Mapinduzi?

  e. Wazanzibari chini ya Serikali ya Mapinduzi?

  f. Wazanzibari kama watu wote wenye kujitambua kuwa wana asili ya Zanzibar hata kama hawaishi Zanzibar au hawajawahi kuishi Zanzibar hivi karibuni?

  Kwa mfano, Mmakonde aliyezaliwa na kukulia Zanzibar atatambulika kama Mzanzibari? Je mmshirazi ambaye wazazi wake wametokea Zanzibar lakini amekulia Tanga na ana familia Zanzibar huyo naye ni Mzanzibari?

  Bado najiuliza Mzanzibari ni nani hasa?
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #21
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Watu nadhani wanashindwa au hawataki kuangalia tu tunachosema ni kitu gani.. je mwarabu wa Zanzibar anaweza kutawala Zanzibar kwa sababu naye ni Mzanzibari?
   
 3. Mtu wa Pwani

  Mtu wa Pwani JF-Expert Member

  #22
  Oct 24, 2010
  Joined: Dec 26, 2006
  Messages: 4,108
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145

  hilo nalo la kuuliza mbona wapo wanatawala huyu mheshimiwa karume ana damu ya kinyasa (baba yake) na ya kiarabu (mama yake) madam ametimiza masharti ya katiba sisi hatuna pingamizi

  ww una lako hutaki kuliweka wazi hebu liweke uchi tulione
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #23
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Mtu wa Pwani, wala sina miye nasikiliza maneno tu. Naamini kwa haki kabisa Zanzibar lazima itawaliwe na Wazanzibari kisheria. Kitu ambacho sikukielewa ni kwanini Maalim anawahakikishia watu kuwa Zanzibar haitotawaliwa na watu wasio Wazanzibari. Aidha, kuna tetesi kuwa kuna Watu wasio Wazanzibari wanataka kutawala au Baadhi ya wagombea siyo Wazanzibari wanataka kutawala. Yote mawili yana matatizo.

  Sijasikia kama kuna mtu kutoka nje ya Zanzibar anataka kuitawala Zanzibar na sijui kama kuna mgombea yoyote sasa hivi ambaye si Mzanzibari. Kama yote haya mawili ni kweli, kwanini kuwahikishia watu kuwa Zanzibar haitotawaliwa na watu wasio Wazanzibari, au ni kile kinachoitwa ni redundancy?
   
 5. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #24
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Na mke wake ni mwarabu.
  yULE MFALME WA MWISHO WA ZANZIBAR ALIKUWA NI MZANZIBARI,kafanana sana na mzee Mwanakijiji.
  Nini wewe mwanakijiji ! kuleta upuuzi huu.Unapenda sana wazanzibari wagombane kwa choko choko zako.
   
 6. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #25
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Maalilm Seif ni mgombea na ni mwanasiasa wa miaka mingi.Anajuwa mengi na anapelekewa taarifa kila aina nyingine za umbea tu.
  Kwa namna yoyote ile yeye ni mtu wa kusikilizwa zaidi kuliko wewe mwanakijiji.Kwa sababu hata ikiwa ni umbeya basi utakaoupata wewe utakuwa ni ujinga zaidi na fitna.
  Unaposema SIJASIKIA,nani akuletee wewe taarifa,na wewe ni nani?.


   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #26
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  hapana Ami sipendi kweli Wazanzibari wagombane au mtu mwingine yoyote; ila sipendi zitafutwe sababu za kuwaganywa na kuwagombanisha. Mchagga ambaye amehamia Zanzibar na kutimiza masharti ya ukazi ya Zanzibar atakuwa ni Mzanzibari na atakuwa na haki ya kutawala Zanzibar, au hili haliwezekani?
   
 8. Ami

  Ami JF-Expert Member

  #27
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2010
  Messages: 1,858
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Hivyo ndivyo ilivyo.Kama unavyoshangaa kwamba hakukuwa na sababu ya Seif kusema vile,pamoja na kwamba kuna mantiki kutokana na vionjo alivyonavyo vya kuwa mgombea uraisi.
  Kwa upande wako hukukuwa na haja ya kuonesha hisia hizo wakati hilo ndilo linaloendelea kwa sasa huko Zanzibar.Kila mwenye kufikia vigezo vya kuwa mzanzibari hakuna anayepinga kuwa mtawala.Kwani wangapi wenye asili ya kichagga wameshatawala Zanzibar katika nafasi mbali mbali.Tatizo la kwako nahisi mara nyingi hujisikii vizuri akitawala mwengine mwenye asili tuseme ya Arabuni au Msumbiji.
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #28
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  absolutely wrong, mimi kwa Zanzibar nataka Seif ashinde, lakini siyo ashinde halafu watu waanze kelele za kuwa tunabaguliwa kwa Uunguja na Upemba kwani huko nyuma watawala wote wa Zanzibar baada ya uhuru wametokea Unguja na watu wa Pemba wakajikuta wanalalamika kama kutengwa hivi japo nao ni Wazanzibari.. Ni muhimu ukubaliane nami kuwa wananchi wote wenye haki ya Zanzibar bila kujali asili yao, rangi zao, dini zao au makabila yao wana haki sawa ya kuifurahia na kuitumikia Zanzibar, unakubaliana nami?
   
 10. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #29
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Mkandara!
  Seif amehusishwa mara nyingi na wapinzani wake ktk kumbandika Tag ya kwamba waki
  mchagua Seif atarudisha utawala wa kisultani Zanzibar hivyo anawaambia wapiga kura wa Zanzibar kwamba Zanzibar itatawaliwa na wazanzibari .
   
 11. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #30
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  KNKU.. welcome back buddy! swali langu ndilo liko hapo, kwani Sultani wa Zanzibar aliacha lini kuwa Mzanzibari?
   
 12. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #31
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Thanks!
  Na arudi kama naye ni MZANZIBAR!
   
 13. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #32
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Mwanakijiji!
  Kwani Historia inatueleza nini kuhusu Sultan?Pili Katiba ya Zanzibar imeainisha vipi kuhusu ni nani Mzazinzibari?
   
 14. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #33
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  si lazima yeye mwenyewe arudi, uzao wake unaweza kurudi au hata watu wengine ambao waliondoka Zanzibar baada ya Mapinduzi ambao hata toka ugenini bado wanatambua Zanzibar ya Sultani siyo ya haya mapinduzi. Ndio maana kwangu mimi Seif akisema kuwa "Sultani na uzao wake hawana haki ya kutawala Zanzibar" atakuwa amesema kitu ambacho ni kizito sana. Hawezi kusema hili hata hivyo. Si kwa sababu anataka Sultani arudi bali kuappease wale wengine ambao wanamuunga mkono kwa sababu he is more tolerant na Sultani labda kuliko mahafidhina wa CCM.
   
 15. K

  Kazi Ndiyo Kipimo Cha Utu JF-Expert Member

  #34
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 1,221
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Ndiyo maana nimeuliza katiba ya wazanzibari inasemaje kuhusu ili?Kama Inamtambua kama naye ni Mzanzibari kwa mujibu wa katiba basi bado kauli ya Seif haina utata na kama haimtambui pia kauli yake haina utata kwani alichosema yeye ni kwamba kila mzanzibari kwa mujibu wa katiba yao anahaki ya kuchaguliwa kuongoza zanzibar.
   
 16. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #35
  Oct 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,737
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Hapana hakusema hivyo.. angesema hivyo wala kusingekuwa na tatizo.
   
 17. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #36
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Ndio maana nasema definition of who is Zanzibari is decided by Seif Sharif Hamad, not by the isles constitution. Hakuwa na maana yoyote ya kusema Zanzibar itatawaliwa na wazanzibar kwa kuwa katiba imesema wazi nani ni mzanzibar na nani anatakiwa kutawala Zanzibar. Yeye amezungumzia mzanzibari (akimtenga mzanzibara) unless aje na ufafanuzi mwingine.
   
 18. S

  Saracen Senior Member

  #37
  Jan 12, 2018
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 148
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  TULIKOTOKA

  WAKAJA JUUU

  WAKO WAPI?
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...