X-PASTER
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 11,605
- 1,843
Usifikirie kuwa sihifahamu Historia ya Zanzibar, naifahamu sana...! Na kama kujivunia maendeleo ya karne zilizo pita basi Kilwa ndio ilikuwa inaongoza maana utawala wake ulikuwa kuanzia Pwani ya Somalia mpaka Msumbiji sofara, utawala ulioanzia mwaka 957 CE. Na visiwa vilivyokuwemo kati yake, Mombassa, Pemba, Zanzibar, Mafia, Comoro na Mozambique. Biashara zilishamili na ilifikia mpaka kujitengenezea sarafu yake...! Mambo yalikuja kuharibika walipovamiwa na Wareno mwishoni mwa karne ya 14...!Kwanza uelewe kuwa Dubai haina Rasilmali yeyote ya kuizidi Zanzibar.
Haina hata mafuta ambayo nchi nyingi za kiarabu ndio yaliyowasaidia/yanayowasaidia kiuchumi.
Dubai iliendelzwa kibiashara na kufanywa kitovu cha biashara kati Yuropa, Asia, Afrika. Hakuna zaidi ya hilo.
Zanzibar, historically ndio iliokuwa kitovu cha biashara baina ya Yuropa, Asia, Amerika na Afrika.
Zanzibar ndio ilikuwa makao makuu ya biashara/uchumi ya Oman, Abudhabi, Baluchistan na nchi za karibu ya huko na karibu ya Zanzibar, zama hizo nyingi kati ya hizo nchi zilikuwa si nchi kamili na zilikuwa zikitaliwa na Sultan wa Oman ambae makao yake Makuu yalikuwa Zanzibar. Mpka alipoingia mkoloni, Mjerumani na Muingereza na kabla yao Mreno, ndio wakaziparaganyisha na kuanza kuzitawala kimabavu himaya za Zanzibar.
Sipo hapa kutowa somo la historia, lakini nimeona ni kubrief, kukubaisnishia kuwa Zanzibar inaweza kujitengenezea rasilmali biashara ki ulaini kabisa na kuipiku kimaendeleo Tanganyika kwa haraka zaidi, kwani Zanzibar kwa sasa ni nchi ndogo na inaweza kujiwekea na kujiletea maendeleo ya haraka zaidi ya Tanganyika. Seuse, kwa sasa inajulikana kuwa ukanda wa bahari inyoizunguka Zanzibar una rasilmali kubwa ya mafuta na gesi asilia.
Zanzibar ina wasomi wengi waliozagaa karibu dunia nzima wanaoweza kuwatosheleza, iwapo tu watawawekea mikakati ya kuwalipa na kuwaenzi vizuri. Wana wafanya biashra waliozagaa dunia nzima na iwapo watawawekea mazingira mazuri, wapo tayari kurudi na kuiendeleza Zanzibar.
Kwa kifupi, Zanzibar inaweza ikawa Singapore ya Afrika within a very short period. Let's say between 10 and 20 years. Provided, hakuna siasa za majungu na hakuna kuingiliwa kiuchumi na Tanganyika.
Haya ni mambo ambayo yeshapita, hizi ni zama tofauti na za zamani...! Unguja ilikuwa muuzaji mzuri wa Karafuu na mbata, soko ambaro hivi sasa limekamatwa na Singapore na kuna nchi zingine kama Guiana, Brazil na West Indies, hawa pia ni walimaji wazuri wa karafuu tena zenye ubora mkubwa.
Haya yote Zanzibar yamepotea na mchawi si Tanganyika ila Wazanzibar wenyewe. Kila kukicha tunasikia jinsi askari wa KMKM wakikamata wasafirishaji wa karafuu, wanao peleka nchi jirani... Kumbuka kuwa KMKM ni mali ya serikali ya mapinduzi Zanzibar.
Tuzungumzie rasilimali zilizokuwepo Zanzibar kwa sasa, je kuna mkakati gani ambao serikali ya mapinduzi ZNZ inayo ili kujikwamua na lindi la umaskini uliokithiri hivi sasa. kumbuka kuwa wale waliokuwa kwenye serikali iliyo pinduliwa January 1964, wengine bado wapo hai. mauwaji ambayo wengi wenye asili ya Arabs na Indians waliuwawa katika mtindo wa genocide... Wapo na wana machungu na kile wanacho kiamini kuwa ni nchi yao halal kabisa, nchi ambayo wamenyang'anywa na machinja chija wa mauwaji ya halaiki (Kimbali). Rejea kitabu cha UKWELI NI HUU KUUSUTA UWONGO kilicho andikwa na Aman Thani Fairooz, vile vile maelezo ya Sheikh Ali Muhsin Al-Barwani ambaye naye aliwekwa jela kwa muda wa zaidi ya miaka kumi bila ya kushitakiwa...!
Kwa maoni yangu mimi, ile dhambi ya mauwaji yaliotokea Mwaka 1964, ndio inaila Zanzibar hivi sasa, na itaendelea kwa karne nyingi sana.

Kilwa Coin, c. 1315, Fitzwilliam Museum