Zanzibar itapojitenga na Tanganyika: Itaendelea kuliko Singapore au Dubai

LUKAZA

Senior Member
Nov 30, 2010
140
225
ZBR KUWA MBALI NA TZ,BARA MAENDELEO FASTA PROFESA H. SEMBOJA

Kweli Zanzibar
kuipiku Dubai
*Kuiacha kwa mbali ‘Dar'. Ila iende kivyake
*Lakini matusi haya ya nini. Akina Samia Suluhu, Fatma Abdulhabib Fereji, Amina Salum Ali, Zahara Ali Hamad, Fatma Maghimbi, Fatma Said Ali, Naila Jidawi hamuwaoni?

*Akina Ana Makinda, Ana Abdalla, Mary Nagu, Ananeliya Nkiya, Gertrude; wameleta maendeleo gani Tanzania Bara?

Imeelezwa kwamba katika kipindi cha miaka mitano hadi kumi, Zanzibar inaweza kupaa kiuchumi na kuiacha kwa mbali Tanzania Bara.

Hayo yamelezwa na Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr. Haji Semboja katika mahojiano yake na baadhi ya vyombo vya habari nchini.
Kwa mujibu wa taarifa za baadhi ya vyombo vya habari, Profesa Semboja amesema kwamba, siasa za chuki, farka na utengano zilizokuwa zikitawala Zanzibar, zilisababisha nguvu kazi kubwa kutokutumika na hivyo kudumaza maendeleo.
Akasema kwamba, maadhali sasa kuna serikali ya umoja wa kitaifa na zile chuki na farka zimezikwa, anachotegemea ni kuwa Wazanzibari watachapa kazi kwa vile wana imani na serikali.

Hata hivyo akaonya kuwa ili Zanzibar ipate mafanikio na ipige hatua, ni lazima ipange na kutekeleza mipango yake ya kiuchumi yenyewe, bila ya kusubiri maelekezo kutoka Bara.
"Lazima sasa Serikali ifanye kazi zake kwa kujitenga na Bara, kwa maana kwamba yapo baadhi ya mambo ya kimaendeleo ambayo wanatakiwa wayafanye wao kama wao, kwa manufaa yao wenyewe, lakini kama wakisema wanatenda kwa kuitazama Tanzania Bara, basi uchumi wake utaendelea kudumaa kila kukicha." Amenukuliwa Profesa Semboja akisema.

"Kwa sasa, sera na siasa za Zanzibar zinabidi zijikite zaidi katika kutilia mkazo matumizi mazuri ya rasilimali kisiwa ili ziweze kuwapunguzia umasikini. Taifa lolote lenye rasilimali kisiwa, hakuna sababu ya kuwa masikini kama hakuna kitu chochote kibaya kinachohatarisha usalama wa mazingira. Kwa hiyo ipo haja ya kuziangalia upya sera na mikakati iliyopo katika kukuza uchumi wa Zanzibar. Usimamiaji na utekelezaji wa sera na mikakati hiyo, utoke katika mtazamo wa Tanzania nzima, na badala yake ujikite zaidi katika utendaji wa kisiwani pekee." Ameongeza Prof. Haji Semboja.

Katika kuhitmisha mahojiano yake Profesa huyo mchumi amenukuliwa akisema mkuwa Zanzibar ikiwa kituo kikubwa cha bidhaa kutoka nchi za Asia, utaona kwamba hata wafanyabiashara wa nchi jirani watakuwa hawaendi tena Dubai, bali watakuja Zanzibar. Na kwamba "mwelekeo wa sasa wa Zanzibar unatakiwa uwe na malengo ya kuufikia uchumi wa Singapore, nchi ambayo huko nyuma uchumi wake ulikuwa unalingana na wa Zanzibar pamoja na nchi nyingine za Afrika Mashariki."
"Kama kweli viongozi wa Zanzibar wataamua kufanya kazi na kuacha maneno, naamini ndani ya miaka 10 ijayo uchumi wa Zanzibar utaufikia uchumi wa Singapore. Hilo linawezekana kama wataenda kwa ‘speed' kubwa, na kama…wafanye kazi zao kwa kujitenga na Tanzania Bara, wasikubali kuambukizwa ugonjwa wa huku (Bara) ambao umejaa maneno matupu bila vitendo." Alimalizia Prof. Semboja kama alivyonukuliwa na baadhi ya magazeti.

Baada ya kuyanukuu maelezo haya, gazeti moja ambalo ndilo lililofanya mahojiano na Profesa Haji Semboja, gazeti hilo liliandika pia tahariri ambapo pamoja na kuunga mkono maoni ya Profesa Semboja, Mhariri alionya juu ya kile alichokiita "kasumba."
Katika ujumla wake Mhariri huyo anasema kwamba, Zanzibar haitapiga hatua katika maendeleo kama haitaachana na "kasumba na utamaduni uliopitwa na wakati."
"Ile kasumba na utamaduni uliopitwa na wakati, unaotoa visingizio vya kulinda utamaduni wa Zanzibar, utamaduni unaomfungia mwanamke ndani, ni muhimu vikaanza kuondolewa pole pole." Anasema Mhariri huyo.

Haihitaji mtu kuwa razini sana kugundua alichokusudia kusema Mhariri huyu. Lakini pengine kwa kuwa naye hakuwa na ujasiri wa kukisema wazi wazi tusiende sana huko.
Lakini tuseme yafuatayo. Tanzania Bara tunao akina Mary, Anna, Ananelya, Jenifa, Margareth, Kate, Gertrude Mongella, Thabitha Siwale na wengine kama hao ambao wamekuwa serikalini na katika sekta binafisi toka nchi hii imepata uhuru.
Labda sasa tuulize, hivi hali ya mwananchi wa Ukerewe, Iramba na Peramiho, inatofautiana vipi kiuchumi na hawa wa Unguja na Pemba wanaodaiwa kuwa na "kasumba na utamaduni uliopitwa na wakati?"
Kwa kuwa na akina Margaret na Gertrude wake toka nchi hii ipate uhuru, Tanzania Bara yaweza kudai kwamba imeendelea sana kiuchumi ikilinganishwa na Zanzibar?

Pengine tukiacha maswali hayo ambayo Mhariri yule anaweza kutumia muda wake kujijibu yeye mwenyewe, hivi sasa katika serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania yupo Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Labda tumuulize Mhariri wetu, huyu Samia ni Mgogo, Mhehe, Mngoni au Mzanzibari?

Yupo pia yule mwanadiplomasia Amina Salum Ali anayetuwakilisha kule Umoja wa Mataifa. Awali mwana mama huyu alikuwa Waziri wa Fedha kule Zanzibar. Huyu naye vipi? Ni Mchagga?
Kama "ile kasumba na utamaduni anaodai Mhariri kuwa umepitwa na wakati, unaotoa visingizio vya kulinda utamaduni wa Zanzibar, utamaduni wa unaomfungia mwanamke ndani" umeweza kuwatoa watu kama Mheshimiwa Amina Salum Ali, basi utakuwa unafaa na Wazanzibari wanapaswa kuuenzi!
Mbali ya hayo tuliwahi kuwa na Waziri Fatma Saidi Ali katika serikali ya Tanzania. Tunao pia hivi sasa Waziri Fatma Fereji na Zahara Ali Hamad katika serikali ya Dr. Shein. Hii kasumba inayowafungia wanawake ndani Zanzibar, imewezaje kuwapata Mawaziri hawa?

Lakini wapo pia wasomi na wanasiasa machachari kama Fatma Maghimbi na Nalaila Jidawi, hawa Mhariri wetu hawaoni?
Hivi Dar es Salaam na Pemba, ni wapi wanawake wana mwamko mkubwa zaidi wa kisiasa na wanashiriki hasa katika siasa, tena kwa gharama zao, sio kwa kutaraji malipo au kupewa posho na kanga?
Utasemaje Zanzibar inaficha wanawake ndani wakati unawaona wanawake wa Kizanzibari wamejaa vyuo vikuu, ndani ya serikali, katika siasa na sekta mbalimbali za kijamii.
Labda Mhariri huyu atuambie, pale Tunguu, Chukwani na SUZA, wanafunzi Wazanzibari wanawake ni wangapi na wanaume wangapi? Hakuna wanafunzi wanawake wa Kizanzibari katika Vyuo Vikuu hivyo?

Pengine tuseme kuwa, ukiyatizama yote haya utakubaliana na Profesa Semboja kwamba kama Zanzibar inataka kupiga hatua katika maendeleo, basi iachane na ‘longolongo' za Bara.
Kinachojidhirisha katika kinachoonekana kuwa nasaha katika kauli hii ya Mhariri ni kejeli na matusi ‘kwa Waswahili'. Ni chuki zisizo na sababu. Sasa ukimsikiliza mtu mwenye chuki, kamwe hatakusaidia maana muda wote, furaha yake yeye ni kukuona unapata shida, ukineemeka anakasirika.
Qur'an imesema kweli, yaliyojificha katika vifua vyao ni makubwa mno. Ni mazito. Na si ajabu wanachukia hata kuwepo kwa hii serikali ya umoja wa kitaifa. Wangependa kuona ‘Waswahili' wa Unguja na Pemba wakiendelea kuparurana. Vita vya panzi furaha ya kunguru.
"Kama kweli viongozi wa Zanzibar wataamua kufanya kazi na kuacha maneno, ndani ya miaka 10 ijayo uchumi wa Zanzibar utaufikia uchumi wa Singapore."
"Hilo linawezekana kama wataenda kwa ‘speed' kubwa, na kama…watafanya kazi zao kwa kujitenga na

Tanzania Bara. Wasikubali kuambukizwa ugonjwa wa huku (Bara) ambao umejaa maneno matupu bila vitendo."

Hili ndilo la kushika. Hizi kejeli ni kuzipuuzilia kwa mbali na kuwapuuza pia wanaozisema.
 
X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,631
1,250
ZBR KUWA MBALI NA TZ,BARA MAENDELEO FASTA PROFESA H. SEMBOJA

Kweli Zanzibar
kuipiku Dubai
*Kuiacha kwa mbali ‘Dar'. Ila iende kivyake
*Lakini matusi haya ya nini. Akina Samia Suluhu, Fatma Abdulhabib Fereji, Amina Salum Ali, Zahara Ali Hamad, Fatma Maghimbi, Fatma Said Ali, Naila Jidawi hamuwaoni?

*Akina Ana Makinda, Ana Abdalla, Mary Nagu, Ananeliya Nkiya, Gertrude; wameleta maendeleo gani Tanzania Bara?

Imeelezwa kwamba katika kipindi cha miaka mitano hadi kumi, Zanzibar inaweza kupaa kiuchumi na kuiacha kwa mbali Tanzania Bara.

Hayo yamelezwa na Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr. Haji Semboja katika mahojiano yake na baadhi ya vyombo vya habari nchini.
Kwa mujibu wa taarifa za baadhi ya vyombo vya habari, Profesa Semboja amesema kwamba, siasa za chuki, farka na utengano zilizokuwa zikitawala Zanzibar, zilisababisha nguvu kazi kubwa kutokutumika na hivyo kudumaza maendeleo...
Hayo maendeleo ya kuipiku Dubai... Kwa rasilimali zipi...!? Unaweza kufafanua hapa.
 
Mo-TOWN

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,723
1,250
nakubaliana na mtoa hoja. X-PASTER Dubai Singapore au tiger economies zimeendelea kwa rasilimali zipi?

Kwa kukuelimisha tu rasilimali uendelezwa! Jifunze toka nchi kama Swiss hata malawi kwa upande wa Kilimo.
 
X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,631
1,250
nakubaliana na mtoa hoja. X-PASTER Dubai Singapore au tiger economies zimeendelea kwa rasilimali zipi?

Kwa kukuelimisha tu rasilimali uendelezwa! Jifunze toka nchi kama Swiss hata malawi kwa upande wa Kilimo.
Mimi sielewi ndio maana nikauliza, je wewe unaweza jibu ilo swali langu!?
 
papason

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
4,124
2,000
Hayo maendeleo ya kuipiku Dubai... Kwa rasilimali zipi...!? Unaweza kufafanua hapa.

Hawa jamaa si wanajinadi kuwa wana reservoirs kubwa sana za mafuta? sijui ni kwa nini hawayachimbi au ni ya mdomono tuuu??
 
mgen

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
20,201
2,000
Hayo maendeleo ya kuipiku Dubai... Kwa rasilimali zipi...!? Unaweza kufafanua hapa.

wauze nini na wanunuzi kina nani ahaaa watauza nguo na tv toka dubai na watawauzia koloni lao la Tanganyika ndio soko lao kubwa.....
 
Mo-TOWN

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
1,723
1,250
X-PASTER nchi nilizotaja hapo juu zimeendelea kutokana na rasilimali watu. Watu hao waliweka mipango mizuri ya keuneleza nchi zao ikiwa ni pamoja na kuexploit resources chache walizo nazo kama land.

For that matter nchi yeyote ile inaweza kuendelea (ikitaka tu)as long as ina rasimali watu.
 
Mallaba

JF-Expert Member
Jan 30, 2008
2,555
1,170
Province(zanzibar) yenyewe inategemea kila kitu kutoka bara, watakimbilia wapi? huo ni upofu tu usiozingatia ukweli na uhalisia, waulize bajeti yao ni kiasi gani? na inatoka wapi? halafu bila hata aibu wanajifanya kutaka kujitenga,wakiulizwa wanatoka wapi wanasema zanzibar wakikana kwa makusudi Utanzania hali halisi ndio unaowaweka hapo walipo...
 
The Khoisan

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
13,488

Sasa mbona tunawang'ang'ania na kuwachagulia viongozi kila kukicha??
 
Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,807
2,000
Tatizo kubwa ni elimu ya chini kama Zanzibar haitatilia mkazo elimu haiwezi kuendelea.Zanzibar sijui hata kama wana university??
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,062
0
Hayo maendeleo ya kuipiku Dubai... Kwa rasilimali zipi...!? Unaweza kufafanua hapa.

Kwanza uelewe kuwa Dubai haina Rasilmali yeyote ya kuizidi Zanzibar.

Haina hata mafuta ambayo nchi nyingi za kiarabu ndio yaliyowasaidia/yanayowasaidia kiuchumi.

Dubai iliendelzwa kibiashara na kufanywa kitovu cha biashara kati Yuropa, Asia, Afrika. Hakuna zaidi ya hilo.

Zanzibar, historically ndio iliokuwa kitovu cha biashara baina ya Yuropa, Asia, Amerika na Afrika.

Zanzibar ndio ilikuwa makao makuu ya biashara/uchumi ya Oman, Abudhabi, Baluchistan na nchi za karibu ya huko na karibu ya Zanzibar, zama hizo nyingi kati ya hizo nchi zilikuwa si nchi kamili na zilikuwa zikitaliwa na Sultan wa Oman ambae makao yake Makuu yalikuwa Zanzibar. Mpka alipoingia mkoloni, Mjerumani na Muingereza na kabla yao Mreno, ndio wakaziparaganyisha na kuanza kuzitawala kimabavu himaya za Zanzibar.

Sipo hapa kutowa somo la historia, lakini nimeona ni kubrief, kukubaisnishia kuwa Zanzibar inaweza kujitengenezea rasilmali biashara ki ulaini kabisa na kuipiku kimaendeleo Tanganyika kwa haraka zaidi, kwani Zanzibar kwa sasa ni nchi ndogo na inaweza kujiwekea na kujiletea maendeleo ya haraka zaidi ya Tanganyika. Seuse, kwa sasa inajulikana kuwa ukanda wa bahari inyoizunguka Zanzibar una rasilmali kubwa ya mafuta na gesi asilia.

Zanzibar ina wasomi wengi waliozagaa karibu dunia nzima wanaoweza kuwatosheleza, iwapo tu watawawekea mikakati ya kuwalipa na kuwaenzi vizuri. Wana wafanya biashra waliozagaa dunia nzima na iwapo watawawekea mazingira mazuri, wapo tayari kurudi na kuiendeleza Zanzibar.

Kwa kifupi, Zanzibar inaweza ikawa Singapore ya Afrika within a very short period. Let's say between 10 and 20 years. Provided, hakuna siasa za majungu na hakuna kuingiliwa kiuchumi na Tanganyika.
 
Jasusi

JF-Expert Member
May 5, 2006
11,522

Nikuulize. Hivi Zanzibar inaweza kuuza bidhaa zake Rwanda na Burundi bila kupitia Tanzania bara? Au watapitishia Mombasa? Ninachosema ni kwamba Zanzibar haiwezi kuendelea bila kuitegemea Tanzania bara
 
Mdondoaji

JF-Expert Member
Mar 17, 2009
5,108
1,225
Nikuulize. Hivi Zanzibar inaweza kuuza bidhaa zake Rwanda na Burundi bila kupitia Tanzania bara? Au watapitishia Mombasa? Ninachosema ni kwamba Zanzibar haiwezi kuendelea bila kuitegemea Tanzania bara

Jasusi acha mawazo ya mgando hayo. Zanzibar inaweza kuwa na maendeleo sana kuliko Tanzania Bara. Kuhusu swali lako jibu rahisi sana Zanzibar wanaweza kuuza bidhaa zao mombasa na malindi (which by the way wakifungua kesi kuidai mombasa na malindi nadhani kenya wana kesi nzito ya kuwajibu wazanzibari). Pili zanzibar wana mafuta ambayo wakiyatumia vizuri wanaweza kukwamuka kiuchumi. Sisi watanganyika tuna gesi nyingi kuliko mafuta na hata hiyo gesi mafisadi wanaifaidi kuliko wazawa tunashindwa na kanchi kadogo kama Qatar kanachojua namna ya kufaidika na gesi hiyo. Tatu population wise. Wakiweza kupanuka kibiashara tu achilia mbali rasilimali za nishati zanzibar inaweza kujimudu kimiundo mbinu. Hili litasaidia nchi kuweza kufanya shughuli mbali mbali za maendeleo.

Naungana na Professa Semboja wazanzibari amkeni na chakalikeni nchi inyanyuke sie huku Tanganyika ndio hivyo tena R.A na nduguye Lowassa wameshika kila kitu hadi tutakapoamka ndio tutajua nini cha kufanya sasa hivi mafisadi ndio wameshika uchumi.
 
zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,062
0
Nikuulize. Hivi Zanzibar inaweza kuuza bidhaa zake Rwanda na Burundi bila kupitia Tanzania bara? Au watapitishia Mombasa? Ninachosema ni kwamba Zanzibar haiwezi kuendelea bila kuitegemea Tanzania bara

Ukimuuzia mtu bidhaa, kuifikisha kwake si tatizo inapitia wapi, kwani Zanzibar ikiuza bidhaa nchi hizo unazozitaja ni wazi kuwa njia rahisi ni kuzipitisha Tanganyika, ya ana kupitia bandari zake au kupitia mawingu yake. Na kwa hilo, Tanganyika itafaidika ikiwa hizo bidhaa zitapitia huko, kwani anaelipia usafiri wa bidhaa na transit charges ni mnunuzi na si muuzaji.
 
Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,694
2,000
Zenji rafiki zangu Zenji. Ndoto zenu hazijaweza kutimia bila bara. Bara Ndio tumeshika usukani nyie mnafuata. La hakika ni kwamba bila Sisi bara kuwakubalia hamna namna. Msijidanganye kwamba mnaweza kwenda popote bila kutegemea bara kibiashara. Ni uongo. Hata mungekuwa na laslimali za mafuta kiasi gani.
Kwanza mpende msipende lazima hayo mafuta tuyafaidi pamoja.
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
24,067
2,000
..Zenj waache siasa.

..wanasiasa wakae pembeni na usukani ushikwe na TECHNOCRATS wenye mapenzi na uzalendo na Zenj.

..Zenj pia inapaswa kupunguza ukubwa wa serikali yake.

..uhusiano mzuri na majirani zake haswa TANGANYIKA na KENYA ni muhimu kwa maendeleo ya ZENJ.

..kama Mauritius na Seychelles wameweza kupiga hatua nzuri bila hata kuwa na mafuta, kwanini Zenj ishindwe?
 
mtemiwao

JF-Expert Member
Sep 5, 2010
384
0
Go zenj go achana na sisi bado hatujui rasilimali tuzifanyeje,ufisadi ndo hivo hadi madam spika hajui maana yake,yaani ni utata wazenj tangulieni mtakuja kutusuruhisha tutakapochoka na kuamua kuchukua hatua
 
BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,521
2,000
Tukubali tukatae zanzibar imekosa maendeleo kutokana na muungano uliopo sasa, ni -ve ktk economy.wamefanywa mazoba kila kitu kutegemea bara na kukosa muelekeo wa maendeleo na kukuza uchumi
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,952
2,000
Zanzibar, kama ilivyo Tanganyika, kama kukiwa na sera nzuri na utawala sahihi wa kusimamia hizo sera inaweza kuendelea kwa muda mfupi ila kuifikia Singapore ndani ya miaka 10, too ambitious. Na kama Zanzibar inataka kuendelea inatakiwa iige Singapore, ambayo mazingira yake ya kijiografia yanakaribiana - vyote ni visiwa. Wasijifananishe na Dubai maana mwanzo wa maendeleo ya Dubai yalisababishwa na bandari. Zanzibar kwa kuwa ni kisiwa bado itategemea Tanganyika na Kenya.

Kuweza kuiiga Singapore, Wazanzibari watakuwa na kazi kubwa ya ku-transform culture zao. Wasingapore ni kama Wachina, ni watu wanaojituma sana kufanya kazi kwa masaa mengi, kitu ambacho sijakiona kwa Wazanzibar wa Zanzibar ingawa ni kweli kuwa Wazanzibari wa asili ya Pemba ni wafanyabiashara wazuri.

Kwa Zanzibar kuwa sehemu ya Tanzania na sehemu ya EAC hawatakuwa na uwezo wa kuwa na kodi zao tofauti na zile za wanachama wengine, hicho kitakuwa ni kipingamizi mojawapo cha kuifanya Zanzibar kuwa kitovu cha biashara. Kwa Zanzibar kuwa sehemu ya Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania, sioni ni kwa namna gani itaweza kuwa Singapore au Dubai ya Afrika.

Mafuta yanayotajwa kuwepo Zanzibar ni ya kinadharia kuliko uwepo halisi. Kuna indication ya mafuta na favourable geology lakini hakuna economic potential iliyokuwa determined. Ni kama tunavyosema kwa bara kuwa kuna indications/occurrences za dhahabu Mkoa wa Pwani, Morogoro, Mpanda, Iringa, Ruvuma, Kagera, n.k. lakini mpaka leo hii hakuna economic potential ambayo inajulikana. Kwa kufanya utafiti zaidi kunaweza kuja kupatikana mgodi au usipatikane kabisa. Suala siyo kuwepo kwa mafuta bali kuwepo kwa mafuta yanayoweza kuchimbika kwa faida. Aheri Wazanzibari waendelee kufanya kazi kwa bidii kuliko kufikiria kuwa kuna mafuta yanakuja, yanaweza yasije kabisa, wakaishia kukata tamaa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom