Zanzibar Itaendelea Kushirikiana na Sweden Kukuza Uhusiano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar Itaendelea Kushirikiana na Sweden Kukuza Uhusiano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kakke, Jun 7, 2012.

 1. Kakke

  Kakke JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 4, 2010
  Messages: 1,797
  Likes Received: 389
  Trophy Points: 180
  [h=3][/h]

  [​IMG]

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akizungumza na Balozi wa Sweeden nchini Tanzania bwana Jennerth Hjelmaker, alipofika Ofisini kwake Migombani kwa ajili ya kubadilishana mawazo. Kushoto ni mshauri wa balozi huyo bibi Margareta Brisman.
  [​IMG]

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Sweeden nchini Tanzania bwana Jennerth Hjelmaker, huko ofisini kwake Migombani. Kulia ni mshauri wa balozi huyo bibi Margareta Brisman. (Picha zote na, Salmin Said, OMKR)

  Na Hassan Hamad OMKR

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema Zanzibar itaendelea kushirikiana na Sweeden katika kukuza uhusiano wake ikizingatiwa kuwa nchi hiyo imekuwa mshirika wa karibu wa maendeleo kwa Zanzibar.

  Maalim Seif ameeleza hayo huko ofisini kwake Migombani alipokuwa na mazungumzo na balozi wa Sheeden nchini Tanzania bwana Jennerth Hjelmaker.  Amesema Zanzibar inathamini sana mchango unaotolewa na nchi hiyo hasa katika sekta za elimu na afya, na kwamba itaendelea kushirikiana na nchi hiyo katika sekta mbali mbali kwa maslahi ya pande hizo mbili.

  Makamu wa Kwanza wa Rais amefahamisha kuwa Zanzibar imeweza kupiga hatua kubwa katika sekta ya elimu na kupelekea kuvuka malengo ya uandikishaji wa wanafunzi wenye sifa ya kuanza kwenda skuli.

  Hata hivyo Maalim Seif amesema licha ya mafanikio hayo, bado Zanzibar inakabiliwa na tatizo la upungufu wa walimu wa Sayansi pamoja na vikalio katika skuli mbali mbali Unguja na Pemba.

  “Tumepata mafanikio mazuri katika sekta hii lakini bado tuna upungufu wa walimu wa sayansi pamoja na vikalio. Hii ni kutokana na kuwa vijana wengi wanasoma masomo ya sanaa na kutojishughulisha na masomo ya sayansi pamoja na yale ya lugha za kigeni”, alibainisha Maalim Seif.

  Amesema kwa sasa serikali imeweka mkakati wa kuwashajiisha wanafunzi kusoma masomo ya sayansi, sambamba na kurahisisha upatikanaji wa vifaa kwa ajili ya masomo hayo, ili kuweza kupunguza au kuondosha kabisa tatizo hili katika siku zijazo.

  Kwa upande mwengine Maalim Seif amesema ipo haja kwa nchi hizo mbili kukaa pamoja ili kutathmini mchango unaotolewa na Sweeden kwa Tanzania, na kuhakikisha kuwa unawafikia walengwa na kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

  Nae balozi wa Sweeden nchini Tanzania bwana Jennerth Hjelmaker amesema nchi yake inafurahia uhusiano mwema uliopo kati yake na Tanzania na kutaka uendelezwe zaidi kwa maslahi ya nchi hizo mbili.

  Balozi Jennerth amefahamisha kuwa Sweden ambayo imekuwa ikishiriana kwa karibu na Tanzania hasa katika masuala ya watoto na haki za binadamu kwa ujumla, itaendelea kutoa ushirikiano wake katika maeneo tofauti, ili kuendeleza uhusiano huo.


  Imewekwa na MAPARA at 7:47 PM
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Jun 7, 2012
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280
  hii nayo thread?
   
Loading...