Zanzibar Inafanya Mauaji Yanguvu Leo!!

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,187
670
Zanzibar Heroes, Rwanda leoNa Sophia Ashery

TIMU ya taifa ya Zanzibar 'Zanzibar Heroes', leo inavaana na Rwanda 'Amavubi' katika mchezo wa robo fainali ya michuano ya Kombe la Chalenji kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Zanzibar Heroes imetinga hatua ya robo fainali hiyo baada ya kuibuka vinara katika kundi lake la C, ikiwa na pointi nne ikiwa imetoka sare ya mabao 2-2 na Sudani kabla ya kuichapa mabao Ethiopia 3-1.
Kwa upande wake Rwanda ilishika nafasi ya pili katika Kundi B ikiwa na pointi sita sawa na Uganda, ina mabao 11 ya kufunga, imefungwa matatu, imepoteza mchezo mmoja, imetoka sare mmoja na imeshinda michezo miwili kati ya mitatu iliyocheza.

Rwanda ilivuna pointi hizo baada ya kuanza vizuri michuano hiyo kwa kuichapa Eritrea mabao 3-0 kabla ya kuifanyia mauaji timu dhaifu ya Jibuti kwa kuibanjua mabao 9-0.

Zanzibar inayoongozwa na Kocha Abdulghani Msoma inatarajiwa kuteremka kwenye uwanja huo kwa nguvu na bila shaka itacheza kufa au kupona kuhakikisha inatinga nusu fainali ya michuano hiyo kwa kishindo.

Katika mchezo huo Zanzibar Heroes itaongozwa na mpachika mabao wake hodari, Abdallah Juma anayecheza timu ya Mtibwa Sugar inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ambaye atashirikiana na kiungo wa pembeni, Abdi Kassim na beki mwenye nguvu, Nadir Haroub 'Cannavaro' wanaocheza Yanga.

Kipa mzoefu katika michuano ya kimataifa, Farouk Ramadhani anatarajiwa kuwepo katika lango kuhakikisha wapinzani wao hawaleti madhara. Mchezo mwingine unaotarajiwa kufanyika leo ni kati ya Kenya 'Harambee Starsa' na Uganda 'The Cranes'.

majira

l e o hapendwi mtu tunataka wazenji wale eid kwa kujinafasi
 
Kili Stars nje
2007-12-18 09:27:53
By Somoe Ng\'itu

La kuvunda halina ubani, timu ya taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, jana iliyaaga mashindano ya Kombe la Chalenji mbele ya mashabiki wake baada ya kupokea kichapo cha bao 2-1 katika mchezo wa robo fainali ya pili uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mchezaji Abdelhamid Amarria ndiye alikuwa mwiba mchungu kwa Kili Stars inayofundishwa na Mbrazil Marcio Maximo baada ya kufunga mabao mawili katika dakika ya tisa na 35 na kupandisha hasira ya mashabiki ambao walionyesha wazi kukerwa na kibano hicho.

Sudan ambayo imeleta wachezaji wengi Yosso, iliandika bao la kwanza baada ya muuaji wao kufunga kwa tiktak kufuatia kujichanganya kwa mabeki wa Kili Stars na kutoa mwanya kwa mfungaji kufanya vitu vyake.

Kili Stars ilisawazisha katika dakika ya 26 kwa bao lililofungwa na Mrwanda, huku Sudan wakijihakikishia ushindi kwa bao lililofungwa tena na Amarria baada ya mabeki wa Stars kumsahau na mfungaji kupata nafasi ya kufunga.

Stars ilishindwa kusawazisha katika dakika ya 82 baada ya Nizar Khalfan aliyepwaya katika nafasi ya kiungo kukosa penati baada ya kupiga mpira uliopanguliwa na kipa wa Sudan Ziriab Hussein.

Baada ya Kili Stars kutolewa mashabiki walimzomea Maximo huku wakisisitiza kuwa hana uwezo wa kuiwezesha timu hiyo kufanya vizuri katika mashindano yoyote.

Naye akizungumza na waandishi wa habari kocha huyo alisema kuwa mchezo ulikuwa mgumu lakini hatupi lawama kwa mchezaji yoyote, ila yeye (kocha) ndiye wa kubeba lawama zote.

``Simlaumu yeyote, mchezo ulikuwa mgumu na mimi ndiye ninabeba lawama kwa Tanzania kutolewa katika robo fainali, ``alisema Maximo.

Katika robo fainali ya kwanza, Burundi ilisonga mbele baada ya kuifunga Eritrea kwa mabao 2-1, ambapo sasa itakumbana na Sudan katika nusu fainali.

Wakati huohuo, timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes, jana ilizuiwa kuingia uwanjani kushuhudia mechi hizo wakidaiwa kuwa hawakuwa na pasi za kuingilia, huku viongozi wa TFF wakiwaangalia bila kutoa msaada wowote.

source.....http://www.ippmedia.com/ipp/nipashe/2007/12/18/104515.htmlmtu wa pwani.......

unawaona hao TFF?
 
HAWA NDUGU ZETU HAWATUPENDI, NA HILO TUNALIJUA MUDA MREFU TU.

LKN LEO TUTATOA FUNZO HALAFU HAYA MASUALA YA MUNGANO TUTAYAENDELEZA ILA KILA ISHARA INAONYESHA KILA MTU AWE NA NCHI YAKE.

HAWA WENZETU TUKIWA NACHO AU KWA MASLAHI YAO TU.

NA UNAONA WAMEILETA HUKU WAKATI ILE NYENGINE INAYOWAHUSU WAO WAMEIACHA KULE?

ACHENI HIZO
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom