Kalunguine
JF-Expert Member
- Jul 27, 2010
- 2,543
- 134
Zanzibar au Tanzania Visiwani kama inavyojulikana inachangia kiasi gani cha bajeti ya Serikali ya Muungano? Kwa mfano tunaona wabunge wengi wa kutoka Zanzibar na pemba kuingia kwenye bunge la muungano ingawa idadi ya watu ni ndogo ukilinganisha na Tanzania bara. Lakini hatufahamu mchango wa kila sehemu ya muungano kwenye uendeshaji wa serikali ya muungano. Wananchi wa ardhi zote mbili bara na visiwani tuna haki ya kujua isije ikawa kuna upande unaoelemewa zaidi.