ZANZIBAR;Ina Watu Milion 1 lkn Mawaziri 25!

Malafyale

JF-Expert Member
Aug 11, 2008
13,813
11,123
Ndoa ya CCM na CUF ya kugawana madaraka ilihitimishwa jana kwa Rais wa ZNZ Dr Shein kutangaza baraza lake KUBWA la mawaziri lenye mawaziri kamili 19 na manaibu wake 6 na kufanya idadi kamIli ya watendaji wakuu wa Wizara kisiwani ZNZ kufikia 25!

ZNZ yenye wakazi milion moJa na ushehe ina uchumi ulioyumba mno kwa sasa;Uchumi wa ZNZ unategemea sana biashara za utalii na imeripotiwa kuwa kwa sasa biashara hiyo imedorora kufuatia kuanguka kwa uchumi wa dunia;lkn bila kujali hali hiyo Rais Shein akateua baraza KUBWA sana la Mawaziri tena akiwaweka hata mawaziri 3 wasio na wizara maalum!

CCM hata baada ya kupata misukosuko ya kukataliwa kwenye sanduku la kura kulikopolekea kupoteza majimbo mengi ya uchaguzi bado haijajifunza?CCM imepoteza majimbo 3 zaidi Unguja na huku ikishindwa kupata hata jimbo moja Pemba kwa sababu ya umaskini wa ZNZ ulikokithiri lknbado haijajifunza kitu?CCM imepoteza kiti cha Ubunge hadi Lindi na Singida sehemu ambazo ilikuwa ndiyo ngome yao kubwa lkn bado haijajifunza?Kwa nini watu Milion 1 wawe na Baraza la Mawaziri la watu 25 wakiwemo 3 wasio na viti maalum?Ndiyo yale yale ya kugawana madaraka kirafiki au?

Tuwafanye nini watu hawa wanaotumia makusanyao makubwa ya kodi zetu kulipana mishahara badala ya kuwekeza hela hizo kwenye mambo ya maendeleo?
 
Na bado, mawaziri 25, Makatibu wakuu 25, manaibu waziri 25, wakurugenzi 100, manaibu wakurugenzi 100 na kila mmoja kati ya hao 275 atakuwa na wapambe wake angalau 4.
Heko Dkt. Shein kwa ahadi yako ya kuinua uchumi za ZNZ.
 
Maana yake ni kila watu 40,000 wana waziri wao, kwa bara hiyo ni waziri kila tarafa!!!!!!!!! or else 25 x 42 = 1050, yaani equivalently and proportionally serikali ya muungano inatakiwa iwe na mawaziri 1050.
 
DK Shein ni mkuu wa wilaya ya Zanzibar. Zanzibar ni wilaya tu katika Tanzania.
 
katika majuha wewe nimuheshimiwa wao. Zumbukuku ulimwengu ukohuku.

Mwera nashukuru kwa hekima zako ulizoonyesha hapa juu. Nimekugongea senksi.

Narudia tena hapa....DK Shein ni mkuu wa wilaya ya Zanzibar ambayo ina kata mbili za Unguja na Pemba. Yaani hata Jimbo la uchaguzi Ilemela Mwanza ni kubwa kuliko Zanzibar nzima.
 
mkuu
ukubwa wapua sio wingi wamakamasi.
 
what a waste.... ashakum si matusi, jinsi huu muungano unavyoendeshwa ni sawa na nyumba ndogo inavyopendelewa
 
Duh watu mnawaonea sana Wazenj, kuna nchi inaitwa Sychelles (cabinet) ina watu wapatao 10 na population ya around 90,000. Angalieni Cyprus na Equatorial Guinea wao cabinet zikoje? Lakini kuna vinchi vidogo zaidi ya Zanzibar ni zaidi ya hapo. Pia hivi basis ya size ya cabinet ni serikali ya Muungano?
 
Anfaal;

Do we need to follow what Sychellians does?Sidhani kama ina manufaa kwetu kwa ukubwa kama huu wa Baraza la Mawaziri la Dr Shein akiteua hadi Mawaziri 3 wa viti maalum!

Ahadi yake kwetu kama ataimarisha uchumi wa ZNZ kweli itatimia kwa ukubwa huu wa serikali?
 
Duh watu mnawaonea sana Wazenj, kuna nchi inaitwa Sychelles (cabinet) ina watu wapatao 10 na population ya around 90,000. Angalieni Cyprus na Equatorial Guinea wao cabinet zikoje? Lakini kuna vinchi vidogo zaidi ya Zanzibar ni zaidi ya hapo. Pia hivi basis ya size ya cabinet ni serikali ya Muungano?

Hizo 'size' ni hatari sana kwa usalama wa nchi. Hivi nikijenga uwanja wa kisasa wa michezo wenye uwezo wa kubeba watu 90,000. Siku kukiwa na tukio la muhimu na wakahudhuria hata watu 75,000 halafu alqaeda wakafanya vitu vyao unategemea nini hapo????

Huo si mfano wa kuigwa, population is power in this world. China power? Euro Power? USA Power??? sasa wazanzibar milioni 1 wenye purchasing power ya kimama wa nyumbani ni Taifa hilo???
 
Muungano wa watu Milion 1 na Milion 45 ni sawa kweli?
ikiwa ni hivyo itabidi Watu wa Tanzania Bara waiachie Huru Serikali ya Watu wa Tanzania Visiwani kuna Serikali 2 Serikali ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa hiyo bora sisi wa bara tuiache hiyo serikali ya visiwani ijitawale wenyewe mnasemaje Wenzangu?
 
Jamani kiachieni kisiwa hiki nikinunue, nataka nikirudishe kwenye asili yake halisi- SHAMBA LA KARAFUU.
 
This thing does not make any sense at all. Is there any people with BRAINS in our society? How can you have 25 ministers/ministries in a such small country?

To my opinion, Zanzibar needs only one ministry, finance ministry. Every other affairs need to be departments under finance. Downsize the government and direct all money and other resources to public services.
 
Tatizo la thithiem ni 'kusaidiana', 'mwenzetu', n.k. Hawaangalii mantiki imekaaje. Wanachoangalia ni ku-accomodate interest za kichama, basi. Katika hali ya kawaida, utawezaje kuunda baraza la mawaziri lenye wajumbe 25 kwa ajili ya kuongoza watu wasiozidi milioni 1!!!!! Ama kweli ukishangaa ya Musa, subiri ya Firauni, kama hujafa kwa mshangao.
 
Back
Top Bottom