Zanzibar 2020 Zanzibar ina wakazi laki 8, wabunge 75 wa nini?

USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
9,886
22,633
Nimeshtushwa na idadi ya wabunge 75 kuwakilisha wakazi wasiofika million huko Zanzibar wakazi wanaozidiwa na mbunge mmoja tu Arusha,Temeke,Ubungo,Mbeya mjini, Kigoma mjini nk ikiwa ni sawa na uwakilishi wa mbunge kwa wakazi 106669 huku ni kuchezea pesa wa walipa kodi.

Kinachoumiza zaidi ni vyama vya siasa vimeweka viwango vya mabilion kufanya kampain eneo ambalo hata mguu au baiskeli unafika hapa naona kunavichwa haviko sawa kabisa hapa ilifaa kuwa na wabunge watano au watatu .

Kuna haja ZEC kuwa makini na uchezeaji wa pesa huu

USSR
 
Tanganyika tunaihitaji Zanzibar kuliko Zanzibar inavyoihitaji Tanganyika..

Hatuna jinsi inabidi tuwape wa Zanzibar nafasi ya kula cake ya taifa sana.. ili wasiupinge Muungano

Pia kumbuka Zanzibar sio mkoa ama wilaya kama Kinondoni na Temeke, Zanzibar ni taifa kamili ambalo lina Rais wake na lina native land yake...lazima tuwape nafasi nyingi maana bila Zanzibar hakuna Tanzania.. ila bila Temeke ama Kinondoni Tanzania bado inakuwepo
 
USSR takwimu za kwamba zanzibar ina wakaazi laki nane umezitoa wapi?

Una uhakika zanzibar ina wakaazi hao?
Je wewe ni Mzanzibari hata utake wabunge wawe idadi unayotaka?

Pilipili usiyo ila inakuwashia nini?

Zanzibar tumekubali kuungana nao na kutengeneza muungano wa nchi ya Tanzania wakiwa ni nchi kamili yenye mamlaka yake hivyo huwezi kuilinganisha na mkoa wowote wa Tanzania Bara.
 
Tanganyika tunaihitaji Zanzibar kuliko Zanzibar inavyoihitaji Tanganyika..

Hatuna jinsi inabidi tuwape wa Zanzibar nafasi ya kula cake ya taifa sana.. ili wasiupinge Muungano

Pia kumbuka Zanzibar sio mkoa ama wilaya kama Kinondoni na Temeke, Zanzibar ni taifa kamili ambalo lina Rais wake na lina native land yake...lazima tuwape nafasi nyingi maana bila Zanzibar hakuna Tanzania.. ila bila Temeke ama Kinondoni Tanzania bado inakuwepo
ni kweli, ikiwemo kuwapa chaguo la NEC Bara! 129 Vs 33 . Ilikuwa zamu ya Vuai, kwa bahati mbaya hajatoka koo za Urais. Zipo mbili
 
Watu wenye fikra kama USSR wanazidi kuongezeka Tanzania. Dawa ya kuweza kutambulika ni kurudi tuakuangalia upya huu Muungano. Sisi wazanzibari asilia hatupendi fujo. Ni watu wastaarabu na wakuheshimika duniani.

Tunaitaka nchi yetu na utaifa wake. Kama alivosema kiongozi wa kizanzibari , Ukhanithi wenu huko huko, sisi hatutaki ukhanithi hapa". Mzanzibari akitamka hivo ujue ameshachoka na upuuzi. Kwa hiyo bora kila mtu kukaa kwake. Kutawaliwa miaka 57 inatosha. Tunaweza kuwa kaji nchi kadogo lakini tunajitambua.
 
Yaani miaka yote hiyo hamkuona kwamba ZNZ ina wabunge wengi?
Kwa kuwa mwaka huu Jecha hatokuwemo kwenye mapinduzi ndio mmeanza chokochoko?
Ebu waacheni wazanzibari waamue wenyewe kwa maslahi yao.
 
Wanaogopa ACT inatoa KUB kupitia kura chahche za ZNZ.

Kiongozi naona kama umewapunguzia hadhi ACT wazalendo. Maana upepo unaonyesha kwamba ACT wazalendo ndio watakao unda serikali ya mapinduzi ya Zanzibar ili watuonyeshe taifa na serikali ya Tanganyika iliyo jificha nyuma ya JMT.

Ama una maanisha watatoa KUB katika bunge la Tanganyika?
 
Nimeshtushwa na idadi ya wabunge 75 kuwakilisha wakazi wasiofika million huko Zanzibar wakazi wanaozidiwa na mbunge mmoja tu Arusha,Temeke,Ubungo,Mbeya mjini, Kigoma mjini nk ikiwa ni sawa na uwakilishi wa mbunge kwa wakazi 106669 huku ni kuchezea pesa wa walipa kodi.

Kinachoumiza zaidi ni vyama vya siasa vimeweka viwango vya mabilion kufanya kampain eneo ambalo hata mguu au baiskeli unafika hapa naona kunavichwa haviko sawa kabisa hapa ilifaa kuwa na wabunge watano au watatu .

Kuna haja ZEC kuwa makini na uchezeaji wa pesa huu

USSR

Ni kweli kabisa. Ukipiga filimbi tu, watu wote wanakusanyika Zanzibar yote.
 
Nimeshtushwa na idadi ya wabunge 75 kuwakilisha wakazi wasiofika million huko Zanzibar wakazi wanaozidiwa na mbunge mmoja tu Arusha,Temeke,Ubungo,Mbeya mjini, Kigoma mjini nk ikiwa ni sawa na uwakilishi wa mbunge kwa wakazi 106669 huku ni kuchezea pesa wa walipa kodi.

Kinachoumiza zaidi ni vyama vya siasa vimeweka viwango vya mabilion kufanya kampain eneo ambalo hata mguu au baiskeli unafika hapa naona kunavichwa haviko sawa kabisa hapa ilifaa kuwa na wabunge watano au watatu .

Kuna haja ZEC kuwa makini na uchezeaji wa pesa huu

USSR
Hili swali ni sawa na kuuliza Comoro kuna wabunge wangapi ? Zanzibar ni nchi yenye mipaka na raisi wake ambae anaamua kugawa majimbo, sijuwi nini kinachokusumbua. Kama ni fedha Zanzibar inachangia, kama ni mzigo tugawane mbawa yaishe!
 
hakuna kitu kinanikera na kunichefua kama Muungano na Zanzibar.

kama kuna kitu namlaani Nyerere mpaka kufa ni kutumezesha li-muungano na Zanzibar

Nyerere alituuza wazima wazima kwa kutaka sifa za kuwa unifying agent wa Waafrika...
Mimi kinachonikera wazanzibar ni kama wake wenza yaani kutwa kulalamika japo naumia kuipoteza Tanzania lakini wanakera sana hao watu
 
Back
Top Bottom