Sr. Magdalena
JF-Expert Member
- Aug 10, 2011
- 803
- 472
- Thread starter
- #21
Sr.
Uhuru ni hali ambayo kwayo wenyeji wa Taifa, Nchi ausehemu yake wana madaraka ya kujichagulia dira na viongozi wawatakao, uwezo wakuwaondoa kwa mujibu wa sheria zilizo pitishwa na vyombo halali vya kitaifa; nakwa hiyo kuwa na sovereignty juu ya Taifa au nchi yao na mstakali wake. Uhuruni tofauti na mapinduzi, kwani mapinduzi yanauondosha utawala ulopo kwa nguvuau amani; ingawa aidha mapinduzi yanaweza kuleta uhuru kutegemea mfumo, dira nauongozi uliopinduliwa. Lakini mapinduzi yanaweza kuwa na dhaira ya kuletauwiano katika kushiriki katika usimamizi wa utawala, kugawana mali n.k.Mapinduzi ya Urusi yalilenga hili, lakini vita vya mapinduzi vya Marekanivililenga kuleta uhuru. Kuhusu Zanzibar inategemea mtazamo wako; Uhuru chini ya himaya ya Sultani uliwakilisha maono ya kitaifa au la?
Kaka Kasesela heshima mbele sana.
Kwa kesi ya Zanzibar Mapinduzi ya 12, January 1964 yalifanywa na John Okello Kijana wa Kiganda aliyekuwa akiishi Pemba kwa muda mchache, huyu jamaa alikuwa na ushawishi mkubwa kwa vijana na nia yake ya kuipindua serikali ya Znz ilifanikiwa, Aliingia unguja na usiku huo wa Jan, 12, 1964 alikiteka kisiwa hicho na ikumbukwe kuwa kipindi hicho bunge la Zanzibar lilifuata mfumo wa bunge la Kiingereza, Sultani akiwa kama ni mtawala tu lakini sio mtawala mwenye maamuzi ya mwisho, kulikuwa na wanzanzibar wengi tu kwenye bunge hili waliokuwa na sauti na maamuzi, kwa kifupi wa Znz waliipindua serikali yao halali.
Swali hapa kwa nini tunakumbatia historia ya Mapinduzi ya Mganda Okello na si nguvu zetu za kudai uhuru kutoka kwa mkoloni Mwingereza?..