Zanzibar ikijitenga na tz bara itakuwa kiuchumi haraka sana kuipita dubai/singapore

LUKAZA

Senior Member
Nov 30, 2010
140
225
ZNZ Kuipiku Dubai?Soma Utoe Maoni Yako

Kweli Zanzibar
kuipiku Dubai
*Kuiacha kwa mbali ‘Dar’. Ila iende kivyake
*Lakini matusi haya ya nini. Akina Samia Suluhu, Fatma Abdulhabib Fereji, Amina Salum Ali, Zahara Ali Hamad, Fatma Maghimbi, Fatma Said Ali, Naila Jidawi hamuwaoni?
*Akina Ana Makinda, Ana Abdalla, Mary Nagu, Ananeliya Nkiya, Gertrude; wameleta maendeleo gani Tanzania Bara?

Imeelezwa kwamba katika kipindi cha miaka mitano hadi kumi, Zanzibar inaweza kupaa kiuchumi na kuiacha kwa mbali Tanzania Bara.
Hayo yamelezwa na Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr. Haji Semboja katika mahojiano yake na baadhi ya vyombo vya habari nchini.
Kwa mujibu wa taarifa za baadhi ya vyombo vya habari, Profesa Semboja amesema kwamba, siasa za chuki, farka na utengano zilizokuwa zikitawala Zanzibar, zilisababisha nguvu kazi kubwa kutokutumika na hivyo kudumaza maendeleo.
Akasema kwamba, maadhali sasa kuna serikali ya umoja wa kitaifa na zile chuki na farka zimezikwa, anachotegemea ni kuwa Wazanzibari watachapa kazi kwa vile wana imani na serikali.

Hata hivyo akaonya kuwa ili Zanzibar ipate mafanikio na ipige hatua, ni lazima ipange na kutekeleza mipango yake ya kiuchumi yenyewe, bila ya kusubiri maelekezo kutoka Bara.
“Lazima sasa Serikali ifanye kazi zake kwa kujitenga na Bara, kwa maana kwamba yapo baadhi ya mambo ya kimaendeleo ambayo wanatakiwa wayafanye wao kama wao, kwa manufaa yao wenyewe, lakini kama wakisema wanatenda kwa kuitazama Tanzania Bara, basi uchumi wake utaendelea kudumaa kila kukicha.” Amenukuliwa Profesa Semboja akisema.

“Kwa sasa, sera na siasa za Zanzibar zinabidi zijikite zaidi katika kutilia mkazo matumizi mazuri ya rasilimali kisiwa ili ziweze kuwapunguzia umasikini. Taifa lolote lenye rasilimali kisiwa, hakuna sababu ya kuwa masikini kama hakuna kitu chochote kibaya kinachohatarisha usalama wa mazingira. Kwa hiyo ipo haja ya kuziangalia upya sera na mikakati iliyopo katika kukuza uchumi wa Zanzibar. Usimamiaji na utekelezaji wa sera na mikakati hiyo, utoke katika mtazamo wa Tanzania nzima, na badala yake ujikite zaidi katika utendaji wa kisiwani pekee.” Ameongeza Prof. Haji Semboja.
Katika kuhitmisha mahojiano yake Profesa huyo mchumi amenukuliwa akisema mkuwa

Zanzibar ikiwa kituo kikubwa cha bidhaa kutoka nchi za Asia, utaona kwamba hata wafanyabiashara wa nchi jirani watakuwa hawaendi tena Dubai, bali watakuja Zanzibar. Na kwamba “mwelekeo wa sasa wa Zanzibar unatakiwa uwe na malengo ya kuufikia uchumi wa Singapore, nchi ambayo huko nyuma uchumi wake ulikuwa unalingana na wa Zanzibar pamoja na nchi nyingine za Afrika Mashariki.”
“Kama kweli viongozi wa Zanzibar wataamua kufanya kazi na kuacha maneno, naamini ndani ya miaka 10 ijayo uchumi wa Zanzibar utaufikia uchumi wa Singapore. Hilo linawezekana kama wataenda kwa ‘speed’ kubwa, na kama…wafanye kazi zao kwa kujitenga na Tanzania Bara, wasikubali kuambukizwa ugonjwa wa huku (Bara) ambao umejaa maneno matupu bila vitendo.” Alimalizia Prof. Semboja kama alivyonukuliwa na baadhi ya magazeti.

Baada ya kuyanukuu maelezo haya, gazeti moja ambalo ndilo lililofanya mahojiano na Profesa Haji Semboja, gazeti hilo liliandika pia tahariri ambapo pamoja na kuunga mkono maoni ya Profesa Semboja, Mhariri alionya juu ya kile alichokiita “kasumba.”
Katika ujumla wake Mhariri huyo anasema kwamba, Zanzibar haitapiga hatua katika maendeleo kama haitaachana na “kasumba na utamaduni uliopitwa na wakati.”
“Ile kasumba na utamaduni uliopitwa na wakati, unaotoa visingizio vya kulinda utamaduni wa Zanzibar, utamaduni unaomfungia mwanamke ndani, ni muhimu vikaanza kuondolewa pole pole.” Anasema Mhariri huyo.

Haihitaji mtu kuwa razini sana kugundua alichokusudia kusema Mhariri huyu. Lakini pengine kwa kuwa naye hakuwa na ujasiri wa kukisema wazi wazi tusiende sana huko.
Lakini tuseme yafuatayo. Tanzania Bara tunao akina Mary, Anna, Ananelya, Jenifa, Margareth, Kate, Gertrude Mongella, Thabitha Siwale na wengine kama hao ambao wamekuwa serikalini na katika sekta binafisi toka nchi hii imepata uhuru.
Labda sasa tuulize, hivi hali ya mwananchi wa Ukerewe, Iramba na Peramiho, inatofautiana vipi kiuchumi na hawa wa Unguja na Pemba wanaodaiwa kuwa na “kasumba na utamaduni uliopitwa na wakati?”

Kwa kuwa na akina Margaret na Gertrude wake toka nchi hii ipate uhuru, Tanzania Bara yaweza kudai kwamba imeendelea sana kiuchumi ikilinganishwa na Zanzibar?
Pengine tukiacha maswali hayo ambayo Mhariri yule anaweza kutumia muda wake kujijibu yeye mwenyewe, hivi sasa katika serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania yupo Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Labda tumuulize Mhariri wetu, huyu Samia ni Mgogo, Mhehe, Mngoni au Mzanzibari?
Yupo pia yule mwanadiplomasia Amina Salum Ali anayetuwakilisha kule Umoja wa Mataifa. Awali mwana mama huyu alikuwa Waziri wa Fedha kule Zanzibar. Huyu naye vipi? Ni Mchagga?

Kama “ile kasumba na utamaduni anaodai Mhariri kuwa umepitwa na wakati, unaotoa visingizio vya kulinda utamaduni wa Zanzibar, utamaduni wa unaomfungia mwanamke ndani” umeweza kuwatoa watu kama Mheshimiwa Amina Salum Ali, basi utakuwa unafaa na Wazanzibari wanapaswa kuuenzi!
Mbali ya hayo tuliwahi kuwa na Waziri Fatma Saidi Ali katika serikali ya Tanzania. Tunao pia hivi sasa Waziri Fatma Fereji na Zahara Ali Hamad katika serikali ya Dr. Shein. Hii kasumba inayowafungia wanawake ndani Zanzibar, imewezaje kuwapata Mawaziri hawa?
Lakini wapo pia wasomi na wanasiasa machachari kama Fatma Maghimbi na Nalaila Jidawi, hawa Mhariri wetu hawaoni?

Hivi Dar es Salaam na Pemba, ni wapi wanawake wana mwamko mkubwa zaidi wa kisiasa na wanashiriki hasa katika siasa, tena kwa gharama zao, sio kwa kutaraji malipo au kupewa posho na kanga?
Utasemaje Zanzibar inaficha wanawake ndani wakati unawaona wanawake wa Kizanzibari wamejaa vyuo vikuu, ndani ya serikali, katika siasa na sekta mbalimbali za kijamii.
Labda Mhariri huyu atuambie, pale Tunguu, Chukwani na SUZA, wanafunzi Wazanzibari wanawake ni wangapi na wanaume wangapi? Hakuna wanafunzi wanawake wa Kizanzibari katika Vyuo Vikuu hivyo?

Pengine tuseme kuwa, ukiyatizama yote haya utakubaliana na Profesa Semboja kwamba kama Zanzibar inataka kupiga hatua katika maendeleo, basi iachane na ‘longolongo’ za Bara.
Kinachojidhirisha katika kinachoonekana kuwa nasaha katika kauli hii ya Mhariri ni kejeli na matusi ‘kwa Waswahili’. Ni chuki zisizo na sababu. Sasa ukimsikiliza mtu mwenye chuki, kamwe hatakusaidia maana muda wote, furaha yake yeye ni kukuona unapata shida, ukineemeka anakasirika.
Qur’an imesema kweli, yaliyojificha katika vifua vyao ni makubwa mno. Ni mazito. Na si ajabu wanachukia hata kuwepo kwa hii serikali ya umoja wa kitaifa. Wangependa kuona ‘Waswahili’ wa Unguja na Pemba wakiendelea kuparurana. Vita vya panzi furaha ya kunguru.

“Kama kweli viongozi wa Zanzibar wataamua kufanya kazi na kuacha maneno, ndani ya miaka 10 ijayo uchumi wa Zanzibar utaufikia uchumi wa Singapore.”
“Hilo linawezekana kama wataenda kwa ‘speed’ kubwa, na kama…watafanya kazi zao kwa kujitenga na Tanzania Bara. Wasikubali kuambukizwa ugonjwa wa huku (Bara) ambao umejaa maneno matupu bila vitendo.”

Hili ndilo la kushika. Hizi kejeli ni kuzipuuzilia kwa mbali na kuwapuuza pia wanaozisema.
 
Newvision

JF-Expert Member
Nov 9, 2010
446
0
Hapo profesa unachemsha kweli kweli? Watauza nazi na karafuu ndiyo wapandishe uchumi? Usiwadanganye wenzio mazingira ya Zanzibar na Singapore ni tofauti sana prof. kubaliana nami
 
MadameX

JF-Expert Member
Dec 27, 2009
7,812
2,000
The above only possible, if below is implemented:-

-Waache uvivu na kucheza bao au karata while everyone is sweating his butf off
-Misaada ya arabuni isikatishwe
-Mambo ya ndugundugu yafe

Sorry, I have little hope for that place.
 
MwanaFalsafa1

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
5,566
1,195
Like mkuu Maxshimba said it is wishful thinking. This is just another strategy to blame Tanzania bara and the Union.
 
Edward Teller

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
3,893
2,000
kama huyo prof.anaona ni bora zanzibar ifanye mambo yenyewe,fine,sisi watanganyika pia tunaweza fanya mambo kivyetu,na ajue kuwa kuwa prof,si kujua mengi au kua wise than others-so hayo ni mawazo yake tu as an individual citizen
 
Geza Ulole

JF-Expert Member
Oct 31, 2009
44,118
2,000
Endeleeni kujidanganya na ubaguzi mlio nao haki ya Mungu the most you can be is Comoro islands and least you can be is Madagascar! Mark my words...tena hata muandishi wa hii article naona amekaa kisharishari na kimipasho zaidi sijui alisomea wapi uhandishi? sasa sijui anawezaje kufananisha Zanzibar town na jimbo lets say Hanang village na cha ajabu kuna uwezekano wa kipato cha mtu wa Hanang (average) kikawa kikubwa kuliko cha wa Zanzibar town kutegemea na shughuli za kiuchumi zilizopo...
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,978
2,000
Nadhani Zanzibar wangeachwa wajitenge tu. Muungano wa sasa hauna tija na kimsingi ni kama tunawabania
 
Kinyasi

Member
Nov 22, 2010
72
125
Hapo profesa unachemsha kweli kweli? Watauza nazi na karafuu ndiyo wapandishe uchumi? Usiwadanganye wenzio mazingira ya Zanzibar na Singapore ni tofauti sana prof. kubaliana nami

Newvision,
Umesahau kwamba ni mazao hayo hayo ndiyo yaliipandisha sana Zanzibar kiuchumi enzi zile za Mzee Karume I? Hadi kufikia miaka ya 70`s kabla ya kifo cha Karume I, Zanzibar ni nchi pekee ukanda wa Africa mashariki iliyokuwa na akiba ya fedha nyingi za kigeni hadi kufikia kulipa madeni yote. Je unadhani Karume alipata wapi ujarisi wa kuutangazia ulimwengu kwamba kama kuna nchi yoyote inayoidai pesa ijitokeze iliwe? kama siyo biashara ya karafuu na nazi? je unafahamu kwamba Zanzibar ilikuwa inachangia pato kubwa kuizidi Bara kwenye ilitokuwa Benki ya Afrika Mashariki? Na ukiongezea vyanzo vipya kama vile Biashara ya utalii Bandari, Zanzibar kupaa kiuchumi si ni sawa na kumsukuma mlevi tu? Zanzibar kupiga hatua kiuchumi ni rahisi sana hata kama si kutegemea shares zake kwenye serikali ya muungano. Mimi ni M-bara ila kwa uzoefu wangu wa kuishi kule takribani mwaka mmoja na jinsi ya hali yasasa ya maridhiano iliyopo huko, sina shaka yoyote na Zenji kuipiga Bara GAP la kiuchumi.
 
mazungumzo ya baraza haya naona mnadanganyana saaana wakati data zipo unaweza fuatilia ukaona ni kiasi gani mlichangia ila hamna hata siku moja mlichangia zaidi ya Bara
 
Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,627
2,000
sasa si waachgeni wajitenge!......kwanza mbona tayari wameshajitenga......mnataka watamke vinywani ndipo mtaelewa?,.....mbona katiba yao iko wazi,na ieleweke pia kuwa kikwete ni rais wa tanganyika tu...........
NNACHOTEGEMEA KUONA BAADAYE NI UUNGUJA NA UPEMBA
 
Papa Mopao

JF-Expert Member
Oct 7, 2009
3,780
2,000
Hao washajitenga zamaaaani, we angalia Maridhiano, angalia walivyoanzisha timu yao ya taifa na mambo mengine mengi yataibuka! mtaona...
 
TUKUTUKU

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
11,775
2,000
Wajitenge tu ,maana wamekuwa kero sana katika miaka ya hivi karibuni.
 
Mkeshahoi

JF-Expert Member
Jan 4, 2009
2,471
1,225
ZNZ Kuipiku Dubai?Soma Utoe Maoni Yako

Kweli Zanzibar
kuipiku Dubai
*Kuiacha kwa mbali ‘Dar'. Ila iende kivyake
*Lakini matusi haya ya nini. Akina Samia Suluhu, Fatma Abdulhabib Fereji, Amina Salum Ali, Zahara Ali Hamad, Fatma Maghimbi, Fatma Said Ali, Naila Jidawi hamuwaoni?
*Akina Ana Makinda, Ana Abdalla, Mary Nagu, Ananeliya Nkiya, Gertrude; wameleta maendeleo gani Tanzania Bara?

Imeelezwa kwamba katika kipindi cha miaka mitano hadi kumi, Zanzibar inaweza kupaa kiuchumi na kuiacha kwa mbali Tanzania Bara.
Hayo yamelezwa na Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dr. Haji Semboja katika mahojiano yake na baadhi ya vyombo vya habari nchini.
Kwa mujibu wa taarifa za baadhi ya vyombo vya habari, Profesa Semboja amesema kwamba, siasa za chuki, farka na utengano zilizokuwa zikitawala Zanzibar, zilisababisha nguvu kazi kubwa kutokutumika na hivyo kudumaza maendeleo.
Akasema kwamba, maadhali sasa kuna serikali ya umoja wa kitaifa na zile chuki na farka zimezikwa, anachotegemea ni kuwa Wazanzibari watachapa kazi kwa vile wana imani na serikali.

Hata hivyo akaonya kuwa ili Zanzibar ipate mafanikio na ipige hatua, ni lazima ipange na kutekeleza mipango yake ya kiuchumi yenyewe, bila ya kusubiri maelekezo kutoka Bara.
"Lazima sasa Serikali ifanye kazi zake kwa kujitenga na Bara, kwa maana kwamba yapo baadhi ya mambo ya kimaendeleo ambayo wanatakiwa wayafanye wao kama wao, kwa manufaa yao wenyewe, lakini kama wakisema wanatenda kwa kuitazama Tanzania Bara, basi uchumi wake utaendelea kudumaa kila kukicha." Amenukuliwa Profesa Semboja akisema.

"Kwa sasa, sera na siasa za Zanzibar zinabidi zijikite zaidi katika kutilia mkazo matumizi mazuri ya rasilimali kisiwa ili ziweze kuwapunguzia umasikini. Taifa lolote lenye rasilimali kisiwa, hakuna sababu ya kuwa masikini kama hakuna kitu chochote kibaya kinachohatarisha usalama wa mazingira. Kwa hiyo ipo haja ya kuziangalia upya sera na mikakati iliyopo katika kukuza uchumi wa Zanzibar. Usimamiaji na utekelezaji wa sera na mikakati hiyo, utoke katika mtazamo wa Tanzania nzima, na badala yake ujikite zaidi katika utendaji wa kisiwani pekee." Ameongeza Prof. Haji Semboja.
Katika kuhitmisha mahojiano yake Profesa huyo mchumi amenukuliwa akisema mkuwa

Zanzibar ikiwa kituo kikubwa cha bidhaa kutoka nchi za Asia, utaona kwamba hata wafanyabiashara wa nchi jirani watakuwa hawaendi tena Dubai, bali watakuja Zanzibar. Na kwamba "mwelekeo wa sasa wa Zanzibar unatakiwa uwe na malengo ya kuufikia uchumi wa Singapore, nchi ambayo huko nyuma uchumi wake ulikuwa unalingana na wa Zanzibar pamoja na nchi nyingine za Afrika Mashariki."
"Kama kweli viongozi wa Zanzibar wataamua kufanya kazi na kuacha maneno, naamini ndani ya miaka 10 ijayo uchumi wa Zanzibar utaufikia uchumi wa Singapore. Hilo linawezekana kama wataenda kwa ‘speed' kubwa, na kama…wafanye kazi zao kwa kujitenga na Tanzania Bara, wasikubali kuambukizwa ugonjwa wa huku (Bara) ambao umejaa maneno matupu bila vitendo." Alimalizia Prof. Semboja kama alivyonukuliwa na baadhi ya magazeti.

Baada ya kuyanukuu maelezo haya, gazeti moja ambalo ndilo lililofanya mahojiano na Profesa Haji Semboja, gazeti hilo liliandika pia tahariri ambapo pamoja na kuunga mkono maoni ya Profesa Semboja, Mhariri alionya juu ya kile alichokiita "kasumba."
Katika ujumla wake Mhariri huyo anasema kwamba, Zanzibar haitapiga hatua katika maendeleo kama haitaachana na "kasumba na utamaduni uliopitwa na wakati."
"Ile kasumba na utamaduni uliopitwa na wakati, unaotoa visingizio vya kulinda utamaduni wa Zanzibar, utamaduni unaomfungia mwanamke ndani, ni muhimu vikaanza kuondolewa pole pole." Anasema Mhariri huyo.

Haihitaji mtu kuwa razini sana kugundua alichokusudia kusema Mhariri huyu. Lakini pengine kwa kuwa naye hakuwa na ujasiri wa kukisema wazi wazi tusiende sana huko.
Lakini tuseme yafuatayo. Tanzania Bara tunao akina Mary, Anna, Ananelya, Jenifa, Margareth, Kate, Gertrude Mongella, Thabitha Siwale na wengine kama hao ambao wamekuwa serikalini na katika sekta binafisi toka nchi hii imepata uhuru.
Labda sasa tuulize, hivi hali ya mwananchi wa Ukerewe, Iramba na Peramiho, inatofautiana vipi kiuchumi na hawa wa Unguja na Pemba wanaodaiwa kuwa na "kasumba na utamaduni uliopitwa na wakati?"

Kwa kuwa na akina Margaret na Gertrude wake toka nchi hii ipate uhuru, Tanzania Bara yaweza kudai kwamba imeendelea sana kiuchumi ikilinganishwa na Zanzibar?
Pengine tukiacha maswali hayo ambayo Mhariri yule anaweza kutumia muda wake kujijibu yeye mwenyewe, hivi sasa katika serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania yupo Waziri katika Ofisi ya Makamu wa Rais, ambaye ni Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan. Labda tumuulize Mhariri wetu, huyu Samia ni Mgogo, Mhehe, Mngoni au Mzanzibari?
Yupo pia yule mwanadiplomasia Amina Salum Ali anayetuwakilisha kule Umoja wa Mataifa. Awali mwana mama huyu alikuwa Waziri wa Fedha kule Zanzibar. Huyu naye vipi? Ni Mchagga?

Kama "ile kasumba na utamaduni anaodai Mhariri kuwa umepitwa na wakati, unaotoa visingizio vya kulinda utamaduni wa Zanzibar, utamaduni wa unaomfungia mwanamke ndani" umeweza kuwatoa watu kama Mheshimiwa Amina Salum Ali, basi utakuwa unafaa na Wazanzibari wanapaswa kuuenzi!
Mbali ya hayo tuliwahi kuwa na Waziri Fatma Saidi Ali katika serikali ya Tanzania. Tunao pia hivi sasa Waziri Fatma Fereji na Zahara Ali Hamad katika serikali ya Dr. Shein. Hii kasumba inayowafungia wanawake ndani Zanzibar, imewezaje kuwapata Mawaziri hawa?
Lakini wapo pia wasomi na wanasiasa machachari kama Fatma Maghimbi na Nalaila Jidawi, hawa Mhariri wetu hawaoni?

Hivi Dar es Salaam na Pemba, ni wapi wanawake wana mwamko mkubwa zaidi wa kisiasa na wanashiriki hasa katika siasa, tena kwa gharama zao, sio kwa kutaraji malipo au kupewa posho na kanga?
Utasemaje Zanzibar inaficha wanawake ndani wakati unawaona wanawake wa Kizanzibari wamejaa vyuo vikuu, ndani ya serikali, katika siasa na sekta mbalimbali za kijamii.
Labda Mhariri huyu atuambie, pale Tunguu, Chukwani na SUZA, wanafunzi Wazanzibari wanawake ni wangapi na wanaume wangapi? Hakuna wanafunzi wanawake wa Kizanzibari katika Vyuo Vikuu hivyo?

Pengine tuseme kuwa, ukiyatizama yote haya utakubaliana na Profesa Semboja kwamba kama Zanzibar inataka kupiga hatua katika maendeleo, basi iachane na ‘longolongo' za Bara.
Kinachojidhirisha katika kinachoonekana kuwa nasaha katika kauli hii ya Mhariri ni kejeli na matusi ‘kwa Waswahili'. Ni chuki zisizo na sababu. Sasa ukimsikiliza mtu mwenye chuki, kamwe hatakusaidia maana muda wote, furaha yake yeye ni kukuona unapata shida, ukineemeka anakasirika.
Qur'an imesema kweli, yaliyojificha katika vifua vyao ni makubwa mno. Ni mazito. Na si ajabu wanachukia hata kuwepo kwa hii serikali ya umoja wa kitaifa. Wangependa kuona ‘Waswahili' wa Unguja na Pemba wakiendelea kuparurana. Vita vya panzi furaha ya kunguru.

"Kama kweli viongozi wa Zanzibar wataamua kufanya kazi na kuacha maneno, ndani ya miaka 10 ijayo uchumi wa Zanzibar utaufikia uchumi wa Singapore."
"Hilo linawezekana kama wataenda kwa ‘speed' kubwa, na kama…watafanya kazi zao kwa kujitenga na Tanzania Bara. Wasikubali kuambukizwa ugonjwa wa huku (Bara) ambao umejaa maneno matupu bila vitendo."

Hili ndilo la kushika. Hizi kejeli ni kuzipuuzilia kwa mbali na kuwapuuza pia wanaozisema.

Atafuta umaarufu tu...
 
Lole Gwakisa

JF-Expert Member
Nov 5, 2008
4,407
2,000
ZNZ Kuipiku Dubai?Soma Utoe Maoni Yako

Kweli Zanzibar
kuipiku Dubai

“Kama kweli viongozi wa Zanzibar wataamua kufanya kazi na kuacha maneno, ndani ya miaka 10 ijayo uchumi wa Zanzibar utaufikia uchumi wa Singapore.”
“Hilo linawezekana kama wataenda kwa ‘speed’ kubwa, na kama…watafanya kazi zao kwa kujitenga na Tanzania Bara. Wasikubali kuambukizwa ugonjwa wa huku (Bara) ambao umejaa maneno matupu bila vitendo.”

Hili ndilo la kushika. Hizi kejeli ni kuzipuuzilia kwa mbali na kuwapuuza pia wanaozisema.

Wishful thinking indeed!!
Huyo Semboja anawafahamu Wazanzibari au anawasikia tu?
Siyo siri kuwa utamaduni unaoongelewa hapo juu ni ule wa uvivu wa kupindukia-umwinyi.
Mtu haendelei kwa maneno matupu na inashangaza huyu Dr Semboja anaongea kwa dhati au ananogesha baraza tu?
 
chegreyson

JF-Expert Member
Nov 23, 2011
974
500
Professa,pale Zanzibar,hakuna serikali ya umoja,kuna serikali ya kutoaminiana.Kwani profesa hujasikia kuwa maalim anapokwenda kwenye ziara rasmi ya kiserikali amapokelewa na mana cuf na sio viongozi wa kiserikali bila kujali itikadi za vyama? Hapo umoja wa kitaifa uko,wapi.It was a marriage for conviniance rough then a marriage of conviction.
 
Zanzibar Spices

JF-Expert Member
Jul 14, 2013
7,364
2,000
Newvision,
Umesahau kwamba ni mazao hayo hayo ndiyo yaliipandisha sana Zanzibar kiuchumi enzi zile za Mzee Karume I? Hadi kufikia miaka ya 70`s kabla ya kifo cha Karume I, Zanzibar ni nchi pekee ukanda wa Africa mashariki iliyokuwa na akiba ya fedha nyingi za kigeni hadi kufikia kulipa madeni yote. Je unadhani Karume alipata wapi ujarisi wa kuutangazia ulimwengu kwamba kama kuna nchi yoyote inayoidai pesa ijitokeze iliwe? kama siyo biashara ya karafuu na nazi? je unafahamu kwamba Zanzibar ilikuwa inachangia pato kubwa kuizidi Bara kwenye ilitokuwa Benki ya Afrika Mashariki? Na ukiongezea vyanzo vipya kama vile Biashara ya utalii Bandari, Zanzibar kupaa kiuchumi si ni sawa na kumsukuma mlevi tu? Zanzibar kupiga hatua kiuchumi ni rahisi sana hata kama si kutegemea shares zake kwenye serikali ya muungano. Mimi ni M-bara ila kwa uzoefu wangu wa kuishi kule takribani mwaka mmoja na jinsi ya hali yasasa ya maridhiano iliyopo huko, sina shaka yoyote na Zenji kuipiga Bara GAP la kiuchumi.

Je wakati huo Zanzibar ilikuwa na watu laki ngapi?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom