Zanzibar huchangia TRA 1.4% lakini hugawiwa 4.5% ya mapato ya Muungano!!

Topical,

..hii posting yangu ni ktk kutafuta faida za muungano kwa Tanganyika.

..so far nimekutana na hasara tupu. mfano mdogo ni jinsi Tanganyika inavyobeba mzigo wa kuwalipa wabunge toka ZNZ.

Sijaona mtanganyika amepaza sauti kuvunja muungano hata mara moja...unafikiri ni wajinga ki-hivyo..

Wanawavyonza wazenj sana ndio maana wanao hicho kiasi kidogo sana ..peanuts

Nawashangaa wazanzibar kwa upole wao.
 
halafu cha ajabu pamoja na kubebwa kote bado wanasema wanadhulumiwa!

MASUALA YASIYO NA MAJIBU KATIKA
MUUNGANO [Mada imetayarishwa na Kuwasilishwa
Katika Mkutano Maalum ulioandaliwa
na Zanzibar Law Society Kuadhimisha
Miaka 41 ya Muungano. Hoteli ya
Bwawani Zanzibar tarehe 23.4.2005]
UTANGULIZI Tokea kuasisiwa hapo tarehe 26
Aprili, 1964 Muungano wa
Tanganyika na Zanzibar ambao ndio
uliozaa Jamhuri ya Muungano ya
Tanzania umekuwa na sifa mbili kuu.
Sifa moja ni ile ya kuwa nyenzo au kitambulisho cha umoja wa kitaifa
Tanzania, na hivyo wale wanaojinadi
kwa uzalendo na hisia za umoja wa
kitaifa wamekuwa wakijinasibisha na
kuupenda mno Muungano na kuahidi
kuulinda kwa gharama zozote. Mapenzi haya ya Muungano
yamepelekea hata Katiba ya Jamhuri
ya Muungano kuwa na kifungu
mahsusi cha kuwataka Viongozi wa
Kitaifa (Rais wa Jamhuri ya Muungano,
Makamo wa Rais, Waziri Mkuu na Rais wa Zanziba) kula kiapo cha kuulinda
Muungano kabla ya kuanza kazi zao
(Kifungu cha Katiba ya Muungano).
Aidha Sheria ya Vyama vya Siasa
inakiondolea sifa ya kutosajiliwa
chama chochote cha Siasa ambacho Katiba yake au sera zake ni za kutaka
kuvunja Muungano. Hii ni kusema
kwamba Katiba na Sheria zetu
zinakataza wananchi kuwa na
mawazo ya kuvunja Muungano. Huu
ni ulinzi na mapenzi makubwa kwa Muungano.
Sifa ya pili ni kuwa Muungano
umekuwa ni kitu kinachotambuliwa
na kukubaliwa na wale
‘WANAOUPENDA’ na “WASIOUPENDA”
kwamba una kasoro nyingi – lugha ya siku hizi huitwa KERO za MUUNGANO.
Fedha, wataalamu na muda mwingi
umetumika katika kutafuta suluhisho
la Kasoro au Kero hizo, lakini
mafanikio yamekuwa madogo mno
(kama yapo). Kuna wanaosema kuwa Kasoro au Kero za Muungano
zimekuwa zikiongezeka badala ya
kupungua. Wanaosema hivyo mimi
nawaunga mkono. Naamini yeyote
atayetafakari kwa makini atawaunga mkono. Hivyo,
suala la msingi ni kwa nini kipenzi hiki
cha Taifa la Jamhuri ya Muungano
kinachoitwa MUUNGANO ambacho
sote tunakubali kuwa kinaumwa
tokea uchanga wake hadi leo, miaka 41 tokea kizaliwe, kimeshindwa
kupatiwa dawa pamoja na Tanzania
kuwa na mabingwa wa dawa za
kisiasa na pamoja na juhudi kubwa za
mabingwa hao bado MUUNGANO
unaumwa zaidi. Wapo wanaodai kuwa dawa ipo na inajulikana lakini
pengine inaonekana ni chungu sana
kupewa kipenzi hicho cha
Watanzania!!. 1.2 Ni maoni yangu kwamba
MUUNGANO una kasoro za msingi za
kimaumbile. Kasoro hizo ni miongoni
mwa sababu za MUUNGANO kuwa na
KERO sugu. Kasoro hizo za maumbile
ni kuwepo kwa masuala ya msingi ya kikatiba ambayo hayana majibu ama
kutoka ndani ya Katiba, Sheria, Sera na
hata kutoka kwa watendaji. 1.3 Katika Waraka huu nitajaribu
kueleza juhudi mbali mbali za
kuondoa Kero za Muungano ambazo
zimeshindwa kuondoa Kero hizo.
Juhudi hizo na kushindwa kwake ni
kielelezo cha kuwepo kwa kasoro za maumbile katika Muungano. Aidha
nitaeleza baadhi ya Masuala yasiyo na
Majibu katika Muungano. Maswali
hayo ni kielelezo cha kasoro za
maumbile na ni miongoni mwa
sababu za kushindwa kupatiwa dawa KERO za Muungano. Kwa kuelewa
mambo hayo mawili pengine
itatusaidia sote kwa pamoja kutoa
mapendekezo ya kusawazisha KERO
za Muungano. 2.0 JUHUDI ZA KUONDOA KERO ZA
MUUNGANO 2.1 Katika kutekeleza shughuli za
Muungano matatizo kadhaa
yamejitokeza ambayo yamepelekea
kuwepo zinazoitwa Kero za
Muungano. Tatizo la siku za mwanzo kabisa la
Muungano lilijitokeza mwaka 1965
wakati jambo jipya la Muungano
lilipoongezwa katika orodha ya
mambo ya Muungano; inaonyesha bila
ya makubaliano baina ya Serikali hizi mbili. Mawasiliano yaliopo katika
kumbukumbu baina ya Waziri wa
Fedha wa Zanzibar na Waziri wa Fedha
wa Serikali ya Muungano
yanaonyesha kuwa mawazo ya
Serikali ya Zanzibar katika uundaji wa Benki Kuu hayakusikilizwa. Baada ya
muelekeo wa kuwa na Shirikisho la
Afrika Mashariki kufifia, nchi za Afrika
Mashariki zikitanguliwa na Uganda
zilichukua hatua za kuanzisha Benki
Kuu zao hata kabla ya kuivunja rasmi Bodi ya Sarafu ya Afrika Mashariki.
Katika hali hiyo ndipo Serikali ya
Muungano ilipochukua hatua za
haraka za kuanzisha Benki Kuu ya
Tanzania bila ya maafikiano rasmi na
Zanzibar na hivyo kupelekea Zanzibar kukosa haki zake katika Bodi ya
Sarafu na ndani ya Benki Kuu ya
Tanzania. Kutokana na hatua hiyo Rais wa
Zanzibar Sheikh Abeid Amani
Karumed aliunda Kamati ya watu 12
ikiongozwa na mtaalamu wa Masuala
ya Benki Bw. E. Ebert ili kuishauri
Serikali juu ya kuanzisha Benki ya Serikali ya Zanzibar. Kamati hiyo
iliwasilisha ripoti yake mwishoni wa
mwaka 1965. Ripoti hiyo pamoja na
mambo mengine ilipendekeza kuwa
Benki hiyo iwe ndio Benki ya Serikali
na itumike kusimamia hesabu za (Accounts) Serikali. Kamati
ilipendekeza hadi ifikapo July, 1966
‘accounts’ zote za Serikali ziwe
zimehamishiwa Benki hiyo. Hapo
ndipo ilipoanzishwa Benki ya Watu wa
Zanzibar (PBZ) ambayo iliendelea kuwa ndio Benki ya SMZ hadi mwaka
2001 wakati Benki Kuu ya Tanzania
ilipoanza rasmi kuwa Benki
inayotumiwa na Serikali ya Zanzibar.
Hivyo pamoja na kuwepo Benki Kuu
kama chombo cha Muungano lakini kuanzia awamu ya kwanza hadi ya
Tano za Serikali ya Zanzibar,
haikutumia Benki hiyo. Serikali ya
Muungano ilikuwa siku zote
ikililalamikia jambo hilo. 2.2 Wakati wa Awamu ya Pili ya
Serikali ya Zanzibar, matatizo ya
Muungano yalijitokeza zaidi. Rais
Aboud Jumbe alionekana dhahiri
kutoridhishwa hata kidogo na
mwenendo wa Muungano. Mbali ya kutafuta mtaalamu wa Sheria kutoka
Ghana, Bw. Bashir Swanzi ili kujenga
Hoja ya kukiukwa kwa Katiba ya
Muungano na kupendekeza hatua za
kisheria za kuondoa kasoro hizo,
hatua iliyopelekea kuanguka kwake katika Uongozi, lakini yeye binafsi
alichukizwa sana na mambo ya
Muungano yanavyoendeshwa bila ya
kufuata Katiba na ‘sprit’ ya Muungano.
Katika moja ya mawasiliano yake ya
kiserikali ya tarehe 23 Oktoba, 1983 aliwahi kuandika yafuatayo: “Kosa moja ambalo linaendelea
kufanywa ni lile la kudhani kwamba
kuimarisha Muungano kuna maana
moja na kuhaulisha shughuli
zisizokuwa za Muungano ziwe za
Muungano na kwamba Chama na Serikali ya Muungano wanaweza
kufanya hivyo – bila ya kuzingatia
Katiba wala hisia au matakwa ya
Zanzibar. Dhana hizo ni ama ni za kupotosha
kusudi kwa sababu wanazozielewa
wenyewe wafanyao hivyo, au ni
kukataa kuelewa Katiba. Vyovyote
vile ilivyo ni mashaka. Kisheria shughuli yoyote isiyo ya
Muungano haiwezi kufanywa iwe ya
Muungano bila ya ridhaa ya Serikali ya
Zanzibar na Serikali ya Tanganyika au
na Serikali ya Muungano kwa niaba ya
Tanzania Bara. Mpango wa Serikali ya Muungano kuwakilisha pia Tanzania
Bara umeleta fadhaa na wasiwasi wa
kutosha katika miaka kadhaa, hasa ya
hivi karibuni. Hata kingekuwa Chama au Serikali ya
Muungano vingeweza Kikatiba
kufanya hivyo, na haviwezi , basi
lingelikuwa ni kosa la uadilifu na pia la
kisiasa kufanya hivyo, bila ya ridhaa
na makubaliano ya pande zote mbili za Muungano, wala hicho
kisingekuwa kitendo cha kuimarisha,
bali cha kudhoofisha na hata
kupotosha dhamiri na maana ya
Muungano. Najua baadhi wana mashaka na kimya
changu na wangependa kujua
msimamo wangu juu ya suala hili la
masahihisho ya Katiba. Msimamo
haunihusu kwa sasa, jambo la msingi
ni kwamba lazima Katiba ziheshimiwe, maadili yafatwe na dhamiri ya
Muungano ihifadhiwe. Dhamiri lazima
siku zote ibaki kuwa ni zao la
nidhamu ya hali ya juu kabisa. Muungano au Umoja hauwezi
kuimarishwa kwa upande mmoja
kutwaa madaraka ambayo ni ya
pande mbili za umoja huo. Ikiwa wote
tutatekeleza wajibu wetu kwa dhati,
haki haitakuwa mbali kuonekana na kila upande utakuwa na utaridhika na
haki yake. Huko ndiko kuimarisha
Muungano”. Hii ni ushahidi wa wazi kuwa pamoja
na viongozi wakuu wa Muungano
kuupenda Muungano lakini waliona
kasoro za wazi za utekelezaji wa
Muungano zaidi ya miaka 20 iliyopita. 2.3 Katika Awamu ya Tatu na Nne
mbali ya mambo ya Muungano
kuongezeka, juhudi za kusawazisha
kasoro za Muungano ziliendelea. Njia
kubwa iliyotumika ilikuwa ile ya vikao
vya pamoja baina ya Serikali ya Muungano na Zanzibar. Vikao hivyo
vikiongozwa na Waziri Mkuu na Waziri
Kiongozi. 2.4 Katika Awamu ya Tano, kama
tutavyoona hapo baadae, Serikali
ilichukua hatua nyingi zaidi kuliko
awamu yoyote kushughulikia kasoro
za Muungano. Dr. Salmin Amour
hakuwa akificha hisia zake za kutoridhishwa na utekelezaji wa
Muungano. Miongoni mwa mambo
aliyoyawekea msimamo wazi wa
kutaka kuwe na uwazi na
masawazisho ni masuala ya uchumi,
kupunguzwa mambo ya Muungano yasiyo ya lazima na suala la Jumuiya
ya Afrika Mashariki. Kuna taaarifa za
kuaminika kuwa wiki chache kabla ya
kutiwa saini Mkataba wa Jumuiya ya
Afrika ya Mashariki, Rais Salmin Amour
alimuandikia Waraka maalum Rais Benjamin Mkapa, kueleza msimamo na
mtazamo wa Zanzibar juu ya
uwakilishi katika Jumuiya ya Afrika
Mashariki. Jambo ambalo nina hakika
ni kuwa Waraka huo wa kurasa 10
wenye maoni na mtazamo wa Zanzibar haukushughulikiwa hadi
leo!! 2.5 Awamu ya Sita ya Serikali ya
Zanzibar inajulikana wazi kwa
msimamo wake juu ya suala la
uchimbaji wa mafuta – msimamo
ambao iliurithi kutoka Awamu ya
Tano. Mbali ya suala hilo, iliunda Kamati ya Wataalamu katika siku za
mwanzo za kuingia madarakani.
Kamati ilichambua kasoro za
Muungano na kupendekeza mambo
ya kubaki katika Muungano, mambo
ya kupunguzwa, mambo ya kuongezwa na utaratibu wa
kuendesha masuala ya Muungano
kisera, kiutawala na katika kutunga
Sheria za Muungano. Miongoni mwa
mapendekezo mahsusi ya Kamati
ilikuwa ni pamoja na kuwa Bunge la Tanzanzia liwe na sehemu mbili –
‘Lower house’ itayoshughulikia
mambo yasiyo ya Muungano ya
Tanzania Bara na ambapo Wabunge
wa Zanzibar hawatoshiriki na “Upper
House” ambayo itashughulikia mambo ya Muungano tu na itakuwa na
uwakilishi sawa baina ya Tanzania
Bara na Zanzibar. Aidha Kamati ilirudia
mapendekezo ya Bomani ya kuwa na
Baraza la Taifa (Council of State)
ingawa kwa muundo tofauti. Baraza hilo kazi yake ni kushughulikia
mambo ya Muungano kisera na
kiutawala. Kamati iliwasilisha Ripoti
yake Serikalini mwezi March, 2001.
Kwa kadri ya ninavyoelewa hakuna
hata moja katika mapendekezo ya Kamati, na ambayo yalikubaliwa na
Serikali lililofanyiwa kazi. Eneo jengine
lilofanyiwa kazi na Awamu ya Sita ni
masuala ya fedha – Benki Kuu na
Tume ya Pamoja ya Fedha. 2.6 Maelezo hayo yanathibitisha
mambo mawili:-
(a) Muungano una kasoro za msingi
(b) Juhudi za kuondoa kasoro hizo
zinazofanywa na viongozi wa SMZ
hazijawa na mafanikio ya maana JUHUDI MAHSUSI ZA SMT NA ZA SMZ 2.7 SMZ peke yake ama kwa
kushirikiana na Serikali ya Muungano,
zimechukua hatua kadhaa za kutafuta
ufumbuzi wa Kero za Muungano. Kwa
upande wa SMZ, miongoni mwa hatua
ilizochukua na ambazo zinajulikana ni pamoja na kuunda Kamati mbali mbali.
Miongoni mwa Kamati zilizoundwa na
SMZ kushughulikia Kero za Muungano
kati ya mwaka 1990 na 2003 ni
pamoja na ziufatazo:
(a) Kamati ya Baraza la Mapinduzi (Kamati ya Amina) ya 1992. (b) Kamati ya Rais ya Kupambanua na
Kasoro za Muungano (Kamati ya
Shamhuna, 1997). (c) Kamati ya Rais Kuchambua Ripoti
ya Kisanga (Kamati ya Salim Juma). (d) Kamati ya Rais ya Kuandaa
Mapendekezo ya SMZ juu ya Kero za
Muungano. (Kamati ya Ramia, 2000). (e) Kamati ya BLM juu ya Sera ya
Mambo ya Nje. (f) Kamati ya Rais ya Wataalamu juu ya
Kero za Muungano (2001). (g) Kamati ya BLM ya Jamuiya ya Afrika
Mashariki. (h) Kamati ya Mafuta (i) Kamati ya Madeni baina ya SMZ na
SMT. (j) Kamati ya Suala la Exchusive
Economic Zone (EEZ)
(k) Kamati ya Masuala ya Fedha na
Benki Kuu. (l) Kamati ya Rais ya Masuala ya Simu –
(1996 – 1999) SMZ pia imewahi kuajiri mtaalamu wa
mambo ya fedha
Dr. Courtrey Blackman na Mtaalam wa
masuala ya mafuta. 2.8 Mbali ya baadhi ya Kamati hizo za
SMZ peke yake, SMT na SMZ zimeunda
Tume, Kamati na Kuajiri Wataalamu
mbali mbali ili kutafuta suluhisho la
Kero mbali mbali za Muungano.
Miongoni mwa Tume na Kamati hizo ni kama zifuatazo:
(a) Kamati ya Mtei
(b) Tume ya Nyalali
(c) Kamati ya Shellukindo
(d) Kamati ya Bomani
(e) Kamati ya Shellukindo 2, ya kuandaa Muafaka juu ya Mambo ya
Muungano baina ya SMZ na SMT.
(f) Kamati ya Harmonisation.
(g) Kamati ya Masuala ya Simu (Kamati
ya Kusila) Aidha SMZ na SMT zimefanya vikao vya
pamoja visivyopungua 80 katika
ngazi mbali mbali ili kuzungumzia
Kero za Muungano. Aidha Serikali hizi
mbili mwaka 1994 ziliomba msaada
wa IMF ili kuzishauri kuhusiana na Benki Kuu, mgawano wa Misaada na
uhusiano wa kifedha
(intergovernmental fiscal relationship). 2.9 Mbali ya juhudi zote hizo, tarehe
14 Novemba, 2000 wakati Rais
Benjamin Mkapa alipokuwa
akizundua Bunge aliahidi kuzipatia
ufumbuzi Kero za Muungano ndani ya
siku 60!! Tokea ahadi ilipotolewa hadi leo ni siku 1620 – yaani siku 60
zimepita mara 27. 2.10 Pamoja na hatua zote hizo
zilizoambatana na masikitiko ya
Viongozi wa juu, manung’uniko ya
wananchi wa pande zote mbili juu ya
uendeshaji wa Muungano na ahadi
nzito za viongozi wa juu wa Serikali za kuondoa kasoro za Muungano – lakini
bado Kero au Kasoro hizo zipo pale
pale au zimezidi zaidi. Cha kusikitisha
zaidi kuwa baadhi ya Kero
zilizozungumzwa mwaka 1984 katika
vikao vya pamoja ndizo Kero hizo hizo zilizozungumzwa katika Ripoti ya
Shellukindo ya 1992 na katika
Muafaka baina ya SMZ na SMT wa
mwaka 1994 na ndizo hizo hizo
zilizozungumzwa katika Ripoti ya
Kamati ya Wataalamu ya SMZ ya 2001. Suala muhimu ni kuwa ni kwa nini
juhudi zote hizo zimeshindwa? Jibu
langu ni kuwa Muungano una Kasoro
za maumbile, za kuzaliwa nazo!! 2.11 Suala muhimu ni kuwa ni vipi
tutaweza kuzibaini Kasoro hizo za
Maumbile katika Muungano? Jibu ni
kuwa baadhi ya kasoro hizo hazitaki
utaalamu kuziona. Hata hivyo kwa
sababu kasoro nyingi za Muungano ziko wazi na zimeshazungumzwa
mara nyingi, wengi wamezizoea na
kuona kwamba kasoro ni sehemu ya
Muungano. Lakini tunaposogea mbele
zaidi na kujiuliza ni kwa nini Kero za
Msingi Muungano zimeshindwa kupatiwa ufumbuzi pamoja na juhudi
na ahadi nzito za viongozi, nadhani
jibu si kuwa Kero hizo zimezoeleka au
kuwa ni sehemu ya Muungano.
Tunapaswa tujiulize zaidi nini kiini cha
tatizo. Wengi wana maoni kuwa kiini cha tatizo ni mfumo wa Serikali mbili.
Ingawa mfumo huo kweli
umechangia, lakini hilo bado ni jibu
rahisi kwa suala zito (gumu) – “it is an
oversimplified answer to a very
complicated question”. 2.12 Kwa maoni yangu, tatizo la
msingi ni kuwa kila uhusiano baina ya
watu una Kanuni za msingi
zinazoongoza uhusiano huo (“basic
principles” au “grundnorm” za
uhusiano). Aidha kuna mipaka ya uhusiano (parameters). Nyenzo za
uhusiano kama vile nyaraka na sera
lazima ziwe na uwezo wa kujibu
maswali ya msingi kuhusiana na
uhusiano huo. 2.13 Katika Muungano wa Tanzania,
Zanzibar na Tanganyika ziliungana
kwa baadhi ya mambo tu na sio
mambo yote na ndio maana kuna
orodha ya mambo ya Muungano.
Aidha ibara ya 64 ya Katiba ya Muungano inaeleza wazi kuwa Bunge
halina mamlaka ya Kutunga Sheria
kwa mambo ya Zanzibar yasiyokuwa
ya Muungano. Hivyo ilitarajiwa
kwamba, kwa vile pande hizi
zimeungana kwa baadhi ya mambo tu Kanuni ya msingi ni kuwa pande hizo
lazima ziwe na kauli sawa kuhusiana
na Mambo ya Muungano katika Sera,
Utawala na katika kuyatungia Sheria.
Aidha ziwe na kauli sawa katika
kuongeza na kupunguza mambo ya Muungano na Katiba iweke bayana
jambo hilo. Katika Muungano wa Kikatiba au wa
kisiasa, Katiba au Mkataba wa
Muungano, Sheria na Sera za
Muungano ndio nyenzo kuu. Iwapo
nyenzo hizo zinashindwa kutoa
majibu kwa masuala ya msingi kuhusiana na Muungano ni kielelezo
tosha kuwa Muungano huo una
kasoro za maumbile. Kasoro hizo ni
pamoja na kutokuwa na Kanuni za
Msingi na kutokuwepo Mipaka katika
Waraka huu tutaeleza Masuali ya Msingi ambayo hayana Majibu katika
Katiba, Sheria na Sera za Muungano. 3.0 MASUALA YASIYO NA MAJIBU 3.1 SUALI LA KWANZA: JE WASHIRIKI
WA MUUNGANO BADO WAPO AU
HAWAPO? 3.1.1 Suala hili ni la msingi kwa vile
nchi ambazo zimeungana kwa baadhi
ya mambo tu, inategemewa kwamba
waliounganisha mambo hayo wapo,
wana vikao rasmi vinavyotambuliwa
na Katiba na Sheria za Nchi. Ilitegemea kuwa Washirika hao wanaamua
kuongeza kupunguza mambo ya
Muungano wakiwa na nguvu sawa ya
uamuzi. Ilitegemea kuwa Washirika
hao wana kauli sawa za maamuzi juu
sera, uendeshaji na Sheria za Muungano. Suala ni kuwa hivi ndivyo
hali ilivyo? 3.1.2 Suala hili kila mtu anaweza kuwa
na maoni na fikra zake, lakini sio jibu
na wala huwezi kupata jibu ndani ya
Katiba, Sheria na Sera za Muungano.
Sababu zinazoonyesha kuwa hakuna
jibu la suali hili ni zifuatazo: (a) Wengi wanadhani kuwa Zanzibar
ipo na ni Tanganyika tu ndio haipo –
lakini ukweli Zanzibar haipo katika
Muungano. Wengine wanahisi
Tanganyika ipo ndani ya Muungano
ikivaa koti la Muungano lakini hata hilo haliko wazi kama iliomo ndani ya
Muungano ni Tanganyika au nalo ni
koti tu la Tanganyika. (b) Hakuna Kikao kinachotambulika
kisheria kinachozikutanisha pande
mbili za Muungano. (c) Mambo ya Muungano kiutawala na
kisera yanaamuliwa na Baraza la
Mawaziri la Serikali ya Muungano.
Zanzibar haiwakilishwi ndani ya
Baraza hilo. Rais wa Zanzibar anaingia
kama Mjumbe wa Baraza la Mawaziri na sio kama upande mmoja wa
chombo hicho ambao unaruhusiwa
kutetea msimamo wa Zanzibar. Hivyo
ndani ya Baraza Rais wa Zanzibar
haiwakilishi Zanzibar kwa vile akiwa
ndani ya Baraza hilo anawajibika kwa Rais wa Muungano na sio kwa
mamlaka yoyote ya Zanzibar. Mawaziri
ambao ni Wazanzibari nao
hawawakilishi Zanzibar bali ni
Mawaziri sawa na wengine ambao
wanafungwa na Kanuni ya kuwajibika kwa pamoja (Collective responsibility).
Hivyo lazima wakubaliane na maamuzi
ya wengi na kwa vyovyote vile
hawamo ndani ya Baraza kuiwakilisha
Zanzibar. (d) Inapotokea Rais wa Muungano au
Makamo wa Rais anatoka Zanzibar –
jee anaiwakilisha Zanzibar.
Ameteuliwa na Zanzibar kama
mshirika wa Muungano kuiwakilisha?
Anayo haki na uwezo wa kisheria wa kutetea maslahi ya mmoja wa
Washiriki ndani ya Muungano ambayo
ni Zanzibar. Jibu ni kuwa Makamo wa
Rais wala Rais anapotokea kutoka
Zanzibar haiwakilishi Zanzibar ndani
ya Muungano bali anatumia fursa yake kama Mtanzania kushika nafasi hiyo.
Hapaswi na hana uwezo wala wajibu
wa kutetea Zanzibar ndani ya
Muungano. (e) Katika kutunga Sheria za
Muungano Zanzibar kama mshirika
inawakilishwa? Takribani Sheria zote
za mambo ya Muungano zinapitishwa
kwa wingi wa Kura. Kwa vile idadi ya
wabunge kutoka Zanzibar takriban ni robo tu ya Wabunge wa Bunge la
Muungano ni wazi kuwa Zanzibar
kupitia Wabunge hao haina kauli
katika kutunga Sheria za Muungano.
Ni mambo yale tu yaliyoainishwa
katika Orodha ya Pili ya Jadweli ya Pili ya Katiba ya Muungano ndio
yanayoamuliwa kwa kauli sawa.
Kichekesho ni kuwa kati ya mambo
hayo 8 yaliyoorodheshwa baadhi sio
mambo ya Muungano. (f) Inapotokea Zanzibar kushirikishwa
kama Zanzibar katika masuala ya
Muungano ni kwa njia ya SMZ
kutakiwa kutoa maoni. Hata hivyo,
maoni hayo ya SMZ ambayo baadhi ya
wakati huandaliwa na Baraza la Mapinduzi, mara nyingi hukataliwa na
hata Mkurugenzi tu wa Serikali ya
Muungano au Katibu Mkuu au Waziri.
Baadhi ya mifano mashuhuri ambapo
maoni ya Zanzibar hayakuzingatiwa
katika masuala muhimu ya Muungano ni: (i) Katika uanzishaji wa Benki Kuu,
mwaka 1965 na marekebisho ya
Benki Kuu, 1995.
(ii) Uanzinshwaji wa Mamlaka ya
Mapato TRA.
(iii) Katika suala la Jumuiya ya Afrika Mashariki.
(iv) Sera ya Mambo ya Nje
(v) Uraia na Uhamiaji na
(vi) Sheria ya Deep Sea Fishing
Authority. (g) Kwa upande wa pili, ingawa
tunasema kuwa Tanganyika imevaa
koti la Muungano lakini suala bado
linabaki, kuwa Tanganyika (T/Bara)
kama mshirika wa Muungano ipo. Jee
Serikali ya Muungano kweli inawakilishwa na kutetea maslahi ya
Tanganyika ndani ya Muungano na
kwa utaratibu gani? 3.2 NINI MAANA YA JAMBO LA
MUUNGANO
3.2.1 Suala hili lina sehemu mbili
zifuatazo:
(a) Mambo ya Muungano ni mangapi;
na (b) Jambo linapoitwa ni la Muungano
maana yake ni nini. Mambo ya Muungano ni Mangapi:
3.2.2 Jibu rahisi kwa watu wengi
kuhusiana na suala hili ni kuwa
mambo ya Muungano ni 22 kama
yalivyoainishwa na Katiba ya
Muungano katika Jadweli la Kwanza. Lakini hata Jadweli hilo limeorodhesha
zaidi ya mambo 22 kama ifuatavyo:
(i) Katiba ya Muungano
(ii) Mambo ya nje
(iii) Ulinzi
(iv) Usalama (v) Polisi
(vi) Hali ya Hatari
(vii) Uraia
(viii) Uhamiaji
(ix) Mikopo ya Nje
(x) Biashara (xi) Utumishi katika Serikali ya
Muungano
(xii) Kodi ya Mapato
(xiii) Forodha (Ushuru)
(xiv) Kodi ya Bidhaa (exercise)
(xv) Bandari (xvi) Usafirishaji wa Anga
(xvii) Posta
(xviii) Simu
(xix) Sarafu
(xx) Mabenki
(xxi) Fedha za Kigeni (xxii) Leseni za Viwanda
(xxiii) Takwimu
(xxiv) Elimu ya Juu
(xxv) Mafuta yasiyosafishwa
(xxvi) Gesi asilia
(xxvii) Baraza la Mitihani (xxviii) Usafiri wa Anga
(xxix) Utafiti
(xxx) Mahkama ya Rufaa
(xxxi) Usajili na Shughuli za Vyama
vya Siasa 3.2.3 Pamoja na Orodha hiyo jadweli
ya Pili, Orodha ya Pili inaeleza kwamba,
Bunge lilipotaka kubadili masuala
yanayohusiana na Mamlaka ya Serikali
ya Zanzibar na suala la Mahkama Kuu
ya Zanzibar – lazima yakubaliwe na theluthi mbili ya Wabunge wa
Tanzania Bara na theluthi mbili ya
Wabunge wa Zanzibar. Suala hapa ni
kuwa kwani hayo ni mambo ya
Muungano? 3.2.4 Dalili ya pili inaonyesha kwamba
Mambo ya Muungano hayajulikani ni
mangapi ni kuwa yapo mambo
yanayofanywa kimuungano pamoja
na kwamba si ya Muungano (kama
vile Bima – inayosimamiwa na Kamishna ya Bima). Aidha yapo
mambo ya Muungano ambayo
hayasimamiwi kimuungano kama vile
Takwimu (isipokuwa sensa ya Idadi
Watu), Bandari na Leseni za Viwanda. 3.2.5 Dalili ya tatu ni kuwa Bunge
limekuwa likitunga Sheria na
kuzifanya za Muungano hata kwa
mambo ambayo hayamo katika
orodha ya Muungano. Mfano ni Sheria
ya Proceeds of Crimes Act ya 1991. 3.2.6 Dalili ya nne ni kuwa kuna
baadhi ya maeneo ambayo Serikali
zenyewe (pamoja na Wanasheria
Wakuu) hazikubaliani kama ni ya
Muungano au si ya Muungano.
Maeneo hayo ni kama vile “Deep Sea Fishing Authority”, na Tume ya Haki za
Binaadamu na Utawala Bora. Aidha
suala la Ushirikiano wa Kimataifa. 3.2.7 Dalili ya Tano ni kuwa hata kwa
yale mambo ambayo yamo katika
Orodha ya Mambo ya Muungano,
mengi hayana tafsiri na hivyo
hayajulikani mipaka yake. Mifano ni
kama vile Elimu ya Juu (inaanzia wapi inaishia wapi?), Usalama (Jee ni ule wa
hata kuweka “watchman”) jee Serikali
ya Zanzibar haina siri zake peke yake
ambazo hazipaswi kujulikana na
Serikali ya Muungano na hivyo kuwa
na taratibu zake za usalama? Mikopo ya Nje, Biashara za Nje. Posta na Simu
jee ni miundo mbinu au udhibiti
(regulatory aspect). 3.2.8 Dalili au hoja ya Sita ni kuwa jee
mambo yasiyo ya Muungano ya
Tanzania Bara pekee nayo ni ya
Muungano au si ya Muungano. Hili
linaonekana kama suali la kijinga
mno, lakini ndio suali gumu hata kwa wanaojiona werevu mno. Hakuna
ubishi kuwa jambo lisipokuwa la
Muungano Zanzibar inaweza
kulisimamia wenyewe, lakini kuna
matatizo kwa upande wa Tanzania
Bara. 3.2.9 Baadhi ni kama yafuatayo:
(i) Bajeti: Zipo baadhi ya Taasisi za
Muungano ambazo zinafanya kazi za
Muungano na sizizo za Muungano –
kwa mfano Bunge linatunga Sheria na
kusimamia mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano. Vivyo hivyo kwa
‘Executive’ na Judiciary ya Muungano.
Hivi gharama zake zitoke wapi. Kwa
sasa Bunge na Executive inajulikana
kuwa ni za Muungano, hivyo
igharamiwe na Mfuko wa Muungano? (ii) Taasisi zisizo za Muungano ndizo
zinazoiwakilisha Zanzibar nje kwa jina
la Tanzania mfano Kilimo, Kazi, Utalii na
hata Tanzania Football Federation.
Hivyo suala linakuja ni wakati gani
taasisi ya Tanzania Bara isiyokuwa ya Muungano inakuwa sio ya
Muungano? 3.2.10 Majibu ya maswali yote hayo
hayamo katika Katiba wala Sheria zetu
wakati ni mambo ya msingi na ndio uti
wa mgongo wa Muungano. Jambo linapoitwa la Muungano Maana
yake Nini. 3.2.11 Jibu la rahisi ni kuwa jambo
linapoitwa la Muungano ni kuwa
Zanzibar haina uwezo wa kulisimamia
kisera, kiutawala na kisheria. Hata
hivyo suala hili ni gumu kuliko
linavyoonekana. Kabla ya kuja sera za biashara Huria mashirika kama vile Air
Tanzania, Shirika la Posta na Simu na
Benki ya Taifa ya Biashara n.k
yakijulikana kama mashirika ya
Muungano. Katika vikao kadhaa
ilikubaliwa kuwa Zanzibar ishirikishwe katika uendeshaji wa mashirika hayo
ya Muungano. Mashirika hayo mengi
yamebinafsishwa. 3.2.12 Hisa za mashirika ama
zinamilikiwa na HAZINA ya Serikali ya
Muungano ama zimeuzwa kwa
‘Strategic Investors” au hata kwa
wananchi. Zanzibar haikupewa hisa.
Kuna hoja kwamba zile hisa za Serikali ya Muungano ndio pia za Zanzibar.
Hoja hii haina uzito kwani katika
Muafaka baina SMT na SMZ ilikubaliwa
kuwa suala hilo lizungumzwe upya
baina ya Serikali mbili (Uk. 46, dondoo
la 18.4.3 la Muafaka). Kwa kadri ya ninavyofahamu suala hilo
halijazungumzwa tena na Zanzibar
imekosa haki zote katika mashirika
hayo yaliyokuwa ya Muungano. Tatizo
kama hilo lilijitokeza katika Benki Kuu.
SMZ ilipodai kuwa na hisa ambazo ilizilipia kupitia Bodi ya Sarafu ya
Afrika Mashariki, Zanzibar ilielezwa na
SMT kuwa haiwezi kuwa na hisa
katika Benki Kuu lakini inaweza
kupewa mafao kwa kima cha asilimia
4.5. 3.2.13 Kwa upande wa pili, taasisi
ambazo ni za Muungano kama vile
TRA, TPDC, TCRA, TCAA, n.k
zinaonekena ni za Muungano katika
ngazi ya Bodi ya Wakurugenzi. Hata
hivyo katika ajira vigezo vinavyotumika ni vya Tanzania Bara.
Kwa mfano anayeomba kuajiriwa
katika Taasisi hizo kama Mwanasheria,
lazima awe ni Wakili wa Mahkama Kuu
ya Tanzania (Bara) ingawa Mahkama
Kuu ya Zanzibar na Tanzania (Bara) zina mamlaka sawa, lakini kuwa wakili
wa Mahkama Kuu, Zanzibar
hakutambuliwi. Aidha Makao Makuu
ya taasisi zote hizo yapo upande
mmoja wa Muungano. Mashirika haya
sio tu kuwa yanatoa fursa za ajira lakini yanatumia fedha nyingi sana
kufundisha wafanyakazi wake kuliko
fedha zinazotumiwa na bajeti ya SMZ
kufundisha watumishi wake. Hivyo
kama taasisi hizo ni za Muungano kwa
nini Mshirika mmoja asifaidike na fursa hizo? Maelezo haya yanaweka bayana suala
ambalo
halijapatiwa jibu la nini maana ya
jambo la
Muungano? 3.3 NINI MAANA YA MTU ANAYETOKA
ZANZIBAR/TANZANIA BARA. 3.3.1 Moja kati ya zilizokuwa nguzo
kuu za Muungano ni ile ya uwakilishi
wa Zanzibar ndani ya Muungano
kupitia Rais wa Zanzibar ambaye
alikuwa Makamo wa Rais wa
Muungano kwa kupitia wadhifa wake wa Urais wa Zanzibar. Baada ya
Marekebisho ya 11 ya Katiba Rais wa
Zanzibar aliondolewa katika nafasi ya
Makamo wa Rais kwa kupitia wadhifa
wake. Badala yake Makamo wa Rais
anapatikana na utaratibu wa Mgombea Mwenza. Chini ya ibara ya
47(3) ya Katiba ya Muungano,
Mgombea Mwenza anateuliwa kwa
Kanuni kuwa iwapo Rais ni mtu
anayetoka upande mmoja wa Jamhuri
ya Muungano, Makamo wa Rais awe ni mtu anayetoka upande wa pili wa
Muungano. 3.3.2 Suala ni kuwa mtu anayetoka
upande mmoja wa Muungano ni sifa
ya uzawa, ukaazi au ya mahusiano?
Mtu anaweza, kwa mfano kutoka
Zanzibar kwa sababu ya kuzaliwa ama
kwa sababu ameishi Zanzibar au kwa sababu wazazi au mmoja wa wazazi
wake ametoka Zanzibar lakini yeye
mwenyewe hajazaliwa wala hajawahi
kuishi Zanzibar. 3.3.3 Nafasi ya Urais (iwe Rais au
Makamo) ni muhimu katika
Muungano, Ni moja ya nguzo zake
kuu. Aidha Katiba ndio muongozo wa
uteuzi wake. Hivi sasa kuna madai
kuwa hakuna utaratibu wa kubadilishana zamu za Urais baina ya
Bara na Zanzibar kwa vile haijaelezwa
ndani ya Katiba wala Sheria yoyote.
Kutokana na utaratibu uliopo
(angalau ndani ya CCM) ya uteuzi wa
mgombea Urais, tunaanza kuandika Kanuni kuwa Zanzibar itaendelea
kutoa Makamo wa Rais. Lakini kwa
vile maana ya mtu anyetoka upande
mmoja wa Jamhuri ya Muungano
hajafafanuliwa ndani ya Katiba, kesho
itakuja Hoja kuwa neno hilo halikutafsiriwa ndani ya Katiba wala
Sheria, hivyo sifa moja yoyote ya
uzawa, ukaazi au uhusiano inafaa.
Sijui kama kuanzia hapo patakuwa
tena na Muungano huu tunaoujua leo.
Njia rahisi ilikuwa ni kusema kwamba mtu anayetoka Zanzibar ni yule
ambaye ana sifa ya kuwa Mzanzibari
chini ya Sheria za Zanzibar. 3.3.4 Serikali ya Muungano ilikataa
wazo hilo kata kata wakati wa kujadili
Muafaka baina ya SMZ na SMT hapo
mwaka 1994. Kamati ya Shellukindo
iliwahi hata kupendekeza Sheria ya
Mzanzibar ifutwe kwa vile inatoa dhana ya uraia wa aina mbili (Angalia
uk. 10 – Dondoo 2.6 la Ripoti ya
Shellukindo). Serikali ya Muungano
hata hivyo katika muafaka wa 1994
ilikubali kuwa kuifuta Sheria hiyo ni
makosa, na hivyo iendelee kuwepo kwa vile ndiyo inayofafanua nani ana
haki ya kuchagua na kuchaguliwa
katika uchaguzi wa Zanzibar. (Angalia
uk. 10 – Dondoo 2.2.2.1 ya Taarifa ya
Muafaka). Hivyo suala hili muhimu halina majibu
ndani ya Katiba na Sheria zetu na ni
wazi kuwa ni mbegu ya mzozo wa
baadae. 3.4 JEE TANZANIA INA UCHUMI MMOJA
AU CHUMI MBILI 3.4.1 Ingawa katika Kitabu cha
Muafaka baina ya SMT na SMZ inaeleza
kuwa “Tanzania ni nchi moja yenye
uchumi mmoja wenye mazingira
tofauti” lakini katika utekelezaji
Serikali zote mbili zinaonyesha kuwa na jibu tofauti – kwamba uchumi wa
Tanzania Bara na Zanzibar ni tofauti.
Hata katika hali halisi ndivyo ilivyo.
Mtafaruku uliopo unatokana na
ukweli kwamba ingawa chumi ni mbili
lakini nyenzo zote kuu za uchumi zinadhibitiwa na Serikali ya
Muungano. Nyenzo kama vile udhibiti
wa sera za fedha, kodi na mahusiano
na nchi za nje hazimo mikononi mwa
Zanzibar ingawa Zanzibar inategemea
ijiendeshe kiuchumi. Dalili au sababu zinazoonyesha wazi
kuwa Tanzania ina chumi mbili ni
pamoja na zifuatazo: (i) Masuala ya Maendeleo ya Uchumi
sio ya Muungano; hivyo kila upande
una Wizara yake inayoshughulikia
uchumi, mipango na sera zake za
uchumi na bajeti yake. (ii) Kila upande una Mfuko wake Mkuu
wa Serikali na hivyo mapato yake. (iii) Kila upande una jukumu la
kushughulikia huduma za jamii,
miundo mbinu n.k. (iv) Kila upande una Sera na Sheria
zake za biashara na uwekezaji na hata
Sheria za ajira. Pamoja na ukweli huo Katiba ya
Muungano haiweki bayana na ndio
inayofanya kusiwe na majibu ya wazi
ya suala hili kwa sababu zifuatazo: (i) Kodi ya Mapato, Mikopo ya nje na
Biashara za Nje bado yamefanywa ni
mambo ya Muungano. Kodi ya Mapato
ambayo ni nyenzo kuu ya uchumi wa
visiwa ambao ni “Service oriented”
badala ya kuwa “resource based” kama ilivyo kwa Bara, bado ni jambo
la Muungano kisera, ingawa mapato
halisi yanatumika Zanzibar. (ii) Sera za fedha na mahusiano ya
kikanda yapo chini ya Serikali ya
Muungano bila ya kuwa na uwazi
wala Sheria inayoilazimisha
kushughulikia maslahi ya kiuchumi ya
Zanzibar. 3.4.2 Kutokana na kutokuwepo
majibu ya wazi na pia kuwepo
mtafaruku ya lipi hasa ndio sahihi,
ndio maana Kero za Muungano
zinaonekana kuzidi badala ya
kupungua kwani maisha ya watu hasa wa Zanzibar yamedidimia
kutokana na uchumi wa Zanzibar
kuanguka kutokana na zao la karafuu
kushuka bei. Mategemeo pekee ya
kiuchumi au uwekezaji katika nyanja
zote hasa za huduma. Hata hivyo Zanzibar haiwezi kuweka sera huru na
za kuvutia za kiuchumi kuliko
Tanzania Bara kwa vile haina mamlaka
katika eneo hilo. Mfano mzuri ni
kushindwa kwa miradi ya EP2,
Bandari Huru na Off-Share Companies. 4.0 HITIMISHO
4.1 Muungano wetu hautalindwa kwa
siasa na kuusifu pekee na kuwaita
wale wanaoukosoa kuwa ni maadui
wa Muungano ingawa wapenzi wa
Muungano wenyewe wanazikubali kasoro hizo hizo na hata
wameziandika na kuzifanyia vikao.
Muungano utalindwa kwa kuwekewa
misingi madhubuti iliyo wazi na
ambayo italindwa kwa misingi ya
Katiba na Sheria inayokubalika na ambayo itatokana na ridhaa za
washirika wa Muungano. 4.2 Mifano ipo mingi. Muungano wa
Uingereza (England) na Scotland
ingawa ulianzia mwaka 1603 lakini
ulijadiliwa rasmi mwaka 1705 na
kuanzishwa rasmi kisheria mwaka
1707. Hata hivyo miaka ya 1990 imeshuhudia ukizungumzwa tena na
kuafikiwa kurejeshwa kwa Bunge la
ndani la Scotland. Aidha, kwa upande
mwengine, ingawa Uingereza
iliungana rasmi na Ireland mwaka
1800 kwa Sheria ya “Union of Great Britan and Ireland” lakini kwa
kukosekana misingi madhubuti
mwaka 1922 majimbo 26 yalijitoa
katika Muungano na kuanzisha Irish
Free State ambayo sasa ni Ireland.
Mfano mwengine, ambao pengine si mzuri ni ule wa Canada na Uingereza.
Ingawa Canada ilipewa hadhi ya
kuwa Dominion kupitia Sheria ya
British North America Act ya 1867
lakini bado kulikuwa na matatizo
mengi ambayo yalifanyiwa kazi ambako kulipelekea kutungwa Sheria
ya kuweka bayana masuala yenye
mzozo kwa Sheria ya Statute ya
Westminster ya 1931. 4.3 Hali ni tofauti katika Muungano wa
Tanzania ambapo marekebisho mengi
ya kikatiba, kishera na kisera
yanafanya Muungano kuwa na
matatizo zaidi kwa vile kiini cha Kero
za Muungano hakijashughulikiwa. Masuala ambayo hayana majibu ni
mengi ndani ya Muungano. 4.4 Niliyoyaeleza ni mifano tu ya
masuala hayo mengi.
Kinachojidhihirisha ni kuwa tatizo sio
la idadi ya Serikali tu lakini ni zaidi ya
hapo. Tatizo la msingi ni lile la Kanuni
za msingi za Muungano kutozingatiwa na kutopatiwa majibu. Kutokana na
Kasoro hizo ndio maana Muungano
wetu kama ulivyo hivi sasa hauwezi
kuhimili mabadiliko ya kisiasa. 4.5 Hakuna Muungano madhubuti
ambao unategemea kulindwa na sera
za chama. Muungano madhubuti ni ule
unaolindwa na misingi madhubuti,
uwazi na wenye majibu kwa masuali
yanayohusu nguzo kuu za Muungano huo
 
Kizibao,

..naelewa uwepo wa ZRB ambayo inakusanya kodi tofauti na zinazokusanywa na TRA huko Zanzibar.

..hata Arusha kuna mapato yanayotokana na kodi zinazokusanywa na manispaa ya mji ambayo hayajumuishwi ktk mapato ya TRA.

..hoja yangu ni kwamba ZNZ inainyonya Tanganyika kwa kujipatia mgao usioendana na mchango wa ZNZ ktk mapato ya muungano.

Ndiyo umetoa argument gani hiyo? kwani ZNZ mapato yanayokusanywa na manispaa yanaingia ZRB au TRA?Halafu cha ajabu kuja jamaa amekupa thanks hapo...hoja zako hazina mshiko
 
Wazanzibar ni kupe tu na JK anawapendelea coz ni dini moja!

kuna kitu kimoja mnachanganya,sisi nyerere ndio alituuza kwenye huu muungano kwa kuifuta tanganyika yetu katika ramani ya dunia kwa sababu anazozijua yeye peke yake,kibaya zaidi inaonekana sisi ndio tunaouhitaji muungano zaidi kuliko wao hivyo lazima tuugharamie,wao wanauona ni mzigo na wameshauri mara kadhaa tuwatue lakini sisi eti tunamuenzi julius nyerere!mtu mabae hata iweje hawezi kurudi tena
 
Mpemba Mbishi,

..yapo madai kwamba ZNZ ilitoa 11% ya mtaji wa BOT.

..baada ya hapo 1966 ZNZ ikaanzisha ZPB ambayo ilikuwa ndiyo "benki kuu" ya SMZ.

..toka 1966 mpaka 2001 ZNZ walikuwa wanahifadhi fedha zao wenyewe ktk PBZ.

..haya siyo maneno yangu, nimeyapata kwenye makala ya Mwanasheria Mkuu wa ZNZ akizungumzia masuala ya muungano yasiyo na majibu ya kuridhisha.

Hiyo ya ZNZ kuanzisha PBZ haiondowi ukweli ya kuwa ZNZ ilichangia 11%(tena bila kutaka) na ilikuwa ni haki yake kupata fungu lake katika faida inayopata BOT katika miaka yote hiyo mpaka 2000 ilikuwa hailipwi pesa hizo,na sina uhakika mpaka sasa kama inalipwa au vp
 
Wazanzibar ni kupe tu na JK anawapendelea coz ni dini moja!

zero thinking capacity..muungano ulianzishwa na mtakatifu (fake) nyerere, JK hahusiki amekuta huu uchafu anasafishi kidogo kidogo, maana WaG. wanaongoza katika kuchafua hali ya uchumi wa watu hapa Tanzania..wachoyo, roho mbaya na ufisadi ndio sifa za waG. wengi
 
Ndiyo umetoa argument gani hiyo? kwani ZNZ mapato yanayokusanywa na manispaa yanaingia ZRB au TRA?Halafu cha ajabu kuja jamaa amekupa thanks hapo...hoja zako hazina mshiko

Kizibao,

..hata huku Tanganyika mapato ya manispaa ya Arusha,Ilala,Kinondoni etc etc hayaingii TRA.

..the same with mapato yanayokusanywa na Zanzibar Revenue Board[ZBR] hayaingii TRA.

..kama sijakuelewa naomba ufafanuzi ili mjadala uweze kuendelea.
 
Kuna waungwana walishaanza kuleta dharau hapa so nimewawekea nondo hiyo. Kazi kwao sasa!

Mpemba Mbishi,

..unajua Watanganyika wengi hawafanyi utafiti kuhusu masuala ya muungano.

..Thanks to waZNZ kwa kutusaidia ktk hili, manaake wakati mlalamika mnafichua pia dhuluma na unyonyaji mnaotufanyia sisi Watanganyika.

..binafsi nisingeweza kujua kwamba waZNZ mlikuwa mnaweka fedha zenu PBZ toka 1966 mpaka 2001. kwa msingi huo mapesa yenu ya utajiri wa biashara ya utumwa na surplus ya karafuu yote mliyafuja wenyewe. kuna kipindi Aboud Jumbe alinunua ndege wakati wakaazi wa ZNZ wana uhaba mkubwa wa chakula.

..kipo kisa kingine cha Azizi Twala kupinga uamuzi wa Mzee Karume kuvuja hazina ya ZNZ kwa matumizi ya anasa kama manunuzi ya peremende. Tena inasemekana hicho ndicho kilichosababisha Karume kumpoteza Azizi Twala. Kisa hicho nacho nimekisoma ktk makala iliyokuwa ikimlaumu Nyerere kwa mauaji ya waZNZ!!!
 
Hiyo ya ZNZ kuanzisha PBZ haiondowi ukweli ya kuwa ZNZ ilichangia 11%(tena bila kutaka) na ilikuwa ni haki yake kupata fungu lake katika faida inayopata BOT katika miaka yote hiyo mpaka 2000 ilikuwa hailipwi pesa hizo,na sina uhakika mpaka sasa kama inalipwa au vp

Kizibao,

..mimi siyo mtaalamu sana wa masuala ya BOT.

..umezungumzia mgao wa faida which is an interesting subject.

..sasa naomba kuuliza kama kuna wakati BOT hupata hasara, na ktk mazingira hayo nini kifanyike.

..zaidi, ina maana ZNZ imeamua kutuadhibu waTanganyika na kutunyonya mapato yetu kwasababu mlichangia 11% ya mtaji wa BOT?

..umeme bure, mgao wa mapato usioeleweka, kujitwalia mapande ya ardhi wakati ardhi si suala la muungano, wabunge wa ZNZ kulipwa na serikali ya Tanganyika, mishahara ya watumishi wa SMZ etc etc, yote hayo ni malipo ya 11% ya mtaji wa BOT???
 
Kizibao,

..hata huku Tanganyika mapato ya manispaa ya Arusha,Ilala,Kinondoni etc etc hayaingii TRA.

..the same with mapato yanayokusanywa na Zanzibar Revenue Board[ZBR] hayaingii TRA.

..kama sijakuelewa naomba ufafanuzi ili mjadala uweze kuendelea.

Naona hujanifahamu hapo ukitaka kujua mapato yanayokusanywa ZNZ kwa mwezi basi yanakuwa mjumuisho wa makusanyo ya ZRB na TRA kwani taasisi hizo mbili zimegawana sehemu za kukusanya kodi(T.bara sehemu zote hizo zinakusanywa na TRA),lakini mwisho wa siku mapato yote yanaingi serikali kuu kama ilivyo mapato ya TRA kwa T.Bara.Na mapato ya manispaa yanabakia manispaa tu.kwa hivyo mapato yanayokusanywa na manispaa ZNZ ni tofauti na yale yanayokusanywa na ZRB na TRA.

Sasa wewe kataka argument yako ya mwazo uliposema Arusha pia mapato ya manispaa tofauti na TRA sawa swa na ZRB..ni kuwa siyo sawa na zanibar nako manispaa zinakusanya mapato yao ambayo hayaendi TRA wala ZRB.
Na kitu chengine ukumbuke ZNB kuna makampuni kibao ambayo yana Bracha zake kama mabenki na mashirika ya simu na haya yote yanafanya biashara zake ZNZ lakini wanalipa kodi Dar kwani ndiko yaliko makao makuu yao na mishahara ya wafanyakazi wa SMT walioko ZNZ kodi zake zote hazikusanywi zanzbar bali zinakusanywa T.Bara na SMZ imeomba miaka mingi sana kodi hizo zikusanywe zanzibar lakini SMT imegoma
 
Kizibao,

..mimi siyo mtaalamu sana wa masuala ya BOT.

..umezungumzia mgao wa faida which is an interesting subject.

..sasa naomba kuuliza kama kuna wakati BOT hupata hasara, na ktk mazingira hayo nini kifanyike.

..zaidi, ina maana ZNZ imeamua kutuadhibu waTanganyika na kutunyonya mapato yetu kwasababu mlichangia 11% ya mtaji wa BOT?

..umeme bure, mgao wa mapato usioeleweka, kujitwalia mapande ya ardhi wakati ardhi si suala la muungano, wabunge wa ZNZ kulipwa na serikali ya Tanganyika, mishahara ya watumishi wa SMZ etc etc, yote hayo ni malipo ya 11% ya mtaji wa BOT???
Nitajie mwaka gani BOT imepata Hasara na SMT hailipi mishahara ya SMZ
 
Naona hujanifahamu hapo ukitaka kujua mapato yanayokusanywa ZNZ kwa mwezi basi yanakuwa mjumuisho wa makusanyo ya ZRB na TRA kwani taasisi hizo mbili zimegawana sehemu za kukusanya kodi(T.bara sehemu zote hizo zinakusanywa na TRA),lakini mwisho wa siku mapato yote yanaingi serikali kuu kama ilivyo mapato ya TRA kwa T.Bara.Na mapato ya manispaa yanabakia manispaa tu.kwa hivyo mapato yanayokusanywa na manispaa ZNZ ni tofauti na yale yanayokusanywa na ZRB na TRA.

Sasa wewe kataka argument yako ya mwazo uliposema Arusha pia mapato ya manispaa tofauti na TRA sawa swa na ZRB..ni kuwa siyo sawa na zanibar nako manispaa zinakusanya mapato yao ambayo hayaendi TRA wala ZRB.
Na kitu chengine ukumbuke ZNB kuna makampuni kibao ambayo yana Bracha zake kama mabenki na mashirika ya simu na haya yote yanafanya biashara zake ZNZ lakini wanalipa kodi Dar kwani ndiko yaliko makao makuu yao na mishahara ya wafanyakazi wa SMT walioko ZNZ kodi zake zote hazikusanywi zanzbar bali zinakusanywa T.Bara na SMZ imeomba miaka mingi sana kodi hizo zikusanywe zanzibar lakini SMT imegoma

Kizibao,

..Thanks,

..kwa hiyo Zanzibar kuna TRA, ZRB,manispaa etc etc ambazo zinakusanya kodi mbalimbali.

..wakati huku Tanganyika kuna TRA [hakuna TRB], halafu kuna manispaa etc etc nazo zinakusanya kodi.

..kwa msingi huo basi sisi Watanganyika mabwege kwa kutoanzisha TRB ambayo ingekusanya kodi zetu ambazo waZNZ msingetia mkono wenu.

..kwanini mapato ya ZRB hayawekwi pamoja na mapato ya TRA ili kama kuna mgawanyo basi ufanyike kwa haki??

..ndiyo maana nasema waZNZ mnatunyonya na mmetuchukua msukule Watanganyika.
 
Nitajie mwaka gani BOT imepata Hasara na SMT hailipi mishahara ya SMZ

Kizibao,

..wewe ndiyo umeleta masuala ya faida inayopatikana ktk shughuli za BOT.

..sasa kama umweza kujua kuna kipindi BOT ilipata faida inawezekana unafahamu mwaka ilipopata hasara.

..kama hakuna mwaka BOT imepata hasara unaweza kutueleza tukasonga mbele na mjadala.

..Tanganyika tumekuwa tukiwakarimu SMZ kwa mishahara, na misamaha ya deni la Tanesco.
 
Kizibao,

..Thanks,

..kwa hiyo Zanzibar kuna TRA, ZRB,manispaa etc etc ambazo zinakusanya kodi mbalimbali.

..wakati huku Tanganyika kuna TRA [hakuna TRB], halafu kuna manispaa etc etc nazo zinakusanya kodi.

..kwa msingi huo basi sisi Watanganyika mabwege kwa kutoanzisha TRB ambayo ingekusanya kodi zetu ambazo waZNZ msingetia mkono wenu.

..kwanini mapato ya ZRB hayawekwi pamoja na mapato ya TRA ili kama kuna mgawanyo basi ufanyike kwa haki??

..ndiyo maana nasema waZNZ mnatunyonya na mmetuchukua msukule Watanganyika.
Hivi unajua kuwa mapato yanayokusanywa na ZRB hayaendi bank of Zanzibar bali yanaenda BOT na inayotoa report yote ya mapato ZNZ no BOT na siyo PBZ ni sawa na mainland?kwa hivyo it doesnt matter kama kuna ZRB au ZRT au TRB kwani BOT ndyo bosi wao kwa T.Bara na ZNB sasa dhulma iko wapi hapo?
Na kitu chengine hayo mahesabu hapo kwenye original post yako siyo sahihi na yanapotosha watu..kwa hivyo ninakuomba njo na data sahihi ya mapato yanayokusanywa ZNZ ambazo utazipata BOT na vile vile tuwekee ni kiasi gani ZNZ inatakiwa ipate kutokana na kodi ya mashirika ambayo yana opperate ZNZ lakini yanalipa kodi Dar na ukijumuisha makato ya wafanyakazi wa SMT ambao wao zanzibar... ukijumuisha vitu vyote hivyo hapo utapata data sahihi ya mapato yanayokusanywa ZNZ na utatuwekea hapa tuta discuss la siyo hivyo hakuna kitu cha kujadili kwani data zako haziko sahihi.
 
Back
Top Bottom