Zanzibar huchangia TRA 1.4% lakini hugawiwa 4.5% ya mapato ya Muungano!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar huchangia TRA 1.4% lakini hugawiwa 4.5% ya mapato ya Muungano!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JokaKuu, Feb 2, 2012.

 1. J

  JokaKuu Platinum Member

  #1
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  ..waziri wa Fedha wa ZNZ amedai TRA hukusanya bilioni 6 kwa mwezi.

  ..TRA nao wametoa taarifa kwamba makusanyo kwa wastani ni bilioni 430 kwa mwezi.

  ..kwa msingi huo ZNZ wanachangia 1.4% ya mapato ya TRA.

  ..je, kwanini serikali ya muungano inawapatia mgao wa 4.5% ya mapato ya muungano?

  ..KWANINI MUUNGANO UNARUHUSU UNYONYAJ HUU WA ZNZ DHIDI YA WATANGANYIKA?

  ..zaidi, ZNZ wanadai 4.5% haitoshi wanataka waongezewe!! Halafu ongeza na umeme wa bure toka Tanesco.
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kafanye utafiti ndipo uje na hoja za maana, yaonekana umekurupuka. 4.5% wanayo pata Znz sio kwamba inatokana tu mapato ya TRA , bali pia inajumuisha misaada ya kimaendeleo inayotolewa kwa Tanzania

   
 3. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #3
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Yakhe inaonekana huna wala hujui kama wewe au huyo wa TRA kuhusiana na hiyo 4.5% ,ambayo mnaonekana hamjui msingi wake na wapi ilipoanzia ,hebu tafuteni mtaji ulioianzisha benki kuu ya Tanzania ,halafu mpange mahesabu .
   
 4. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #4
  Feb 2, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Ifike wakati Mods muwe mnawapiga ban watu wanaokurupuka kuchangia upupu humu ndani ndiyo kutakuwa na nidhamu! huyu jamaa sijui katoka wapi anaweka uongo hapa!
   
 5. J

  JokaKuu Platinum Member

  #5
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  Genious Brain,

  ..lakini mchango wa kila upande si ndiyo basis ya mgawanyo wa mapato ya aina yoyote ile?

  ..sasa hebu nieleze uhalali wa ZNZ kupewa 4.5% ya mapato ya TRA + misaada ya kimaendeleo.

  ..pia naomba utueleze uhalali wa ZNZ kudai wapewe zaidi ya wanachopewa sasa hivi, pamoja na upendeleo wa aina nyingine kama kupewa umeme bure au kwa kulipia umeme kwa kiwango cha chini kuliko Watanganyika
   
 6. J

  JokaKuu Platinum Member

  #6
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  VGL,

  ..mod akinifungia atakuwa amenionea.

  ..kama wewe unafahamu kwamba ZNZ inachangia zaidi ya hiki nilichokieleza naomba ulete ushahidi wako.

  ..kwa taarifa yako nimezipata habari hizi ktk mitandao ya Wazanzibari kama MZALENDO.NET, na ZANZIBARWEBSITE.
   
 7. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #7
  Feb 2, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Zanzibar ni mzigo !
   
 8. WiseLady

  WiseLady JF-Expert Member

  #8
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 22, 2010
  Messages: 3,248
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  halafu cha ajabu pamoja na kubebwa kote bado wanasema wanadhulumiwa!
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Mchakato wa kumfanya Mwl Nyerere mtakatifu nitaukwamisha kwasababu katuachia dhuluma kubwa waTanganyika zanzibar wamezidi kutunyonya.
   
 10. J

  JokaKuu Platinum Member

  #10
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  WiseLady,

  ..Waznz wanapiga kelele kwamba hawaitaki TRA ktk ardhi yao.

  ..Pia wanadai wanapunjwa ktk mapato ya muungano kwa kupewa 4.5%.

  ..kwa msingi huo hawataki kuchangia chochote ktk muungano, na juu yake wanataka wapewe mgao mkubwa zaidi.

  NB:

  ..Arusha wanachangia zaidi. On the average wanachangia billion 11.66 kwa mwezi.
   
 11. K

  Kizibao JF-Expert Member

  #11
  Feb 2, 2012
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 739
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 80
  Hahaha inaonyesha hamna hata idea system ya ukusanyaji kodi zanzibar.kodi ZNZ inakusanywa na ZRB na TRA.lakini mainland inakusanywa na TRA tu sasa unapotaka kupiga mahesabu ya kodi inazokusanywa ZNZ basi ujumuuishe makusanyo ya ZRB na TRA.sasa ZRB inakusanya mara mbili ya TRA na siyo kweli ya kuwa arusha inakusanya kodi kubwa zaidi ya ZNZ kwani hiyo 6bil ni makusanyo ya TRA tu. sasa tafuta ya ZRB na nina uhakika unajua simple addition..
   
 12. T

  Topical JF-Expert Member

  #12
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Te te te ..mtakatifu nyerere tuombee tupunguzie dhambi zetu..lol..sipati picha maombi haya ya MaK.
   
 13. T

  Topical JF-Expert Member

  #13
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Watanganyika wangeshatua huo mzigo, maana kimsingi zanzibar hawataki muungano so Tanganyika wanafaidika sana ndio maana hawataki kuachia...
   
 14. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #14
  Feb 2, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jee munajua kama share ya Zanzibar ilikua 11% au munajua habari za mgao wa 4.5% tu?
   
 15. t

  timbilimu JF-Expert Member

  #15
  Feb 2, 2012
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 4,780
  Likes Received: 151
  Trophy Points: 160
  Mkuu JokaKuu umesahau na zile pesa bwerere jamaa zao wanabeba kutoka bunge la Muungano,maana haiwezekani eneo lenye ukubwa wa kitongoji ligeuzwe kuwa jimbo la uchaguzi. Tunawabeba sana hawa jamaa.
   
 16. J

  JokaKuu Platinum Member

  #16
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  Kizibao,

  ..naelewa uwepo wa ZRB ambayo inakusanya kodi tofauti na zinazokusanywa na TRA huko Zanzibar.

  ..hata Arusha kuna mapato yanayotokana na kodi zinazokusanywa na manispaa ya mji ambayo hayajumuishwi ktk mapato ya TRA.

  ..hoja yangu ni kwamba ZNZ inainyonya Tanganyika kwa kujipatia mgao usioendana na mchango wa ZNZ ktk mapato ya muungano.
   
 17. J

  JokaKuu Platinum Member

  #17
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  Mpemba Mbishi,

  ..yapo madai kwamba ZNZ ilitoa 11% ya mtaji wa BOT.

  ..baada ya hapo 1966 ZNZ ikaanzisha ZPB ambayo ilikuwa ndiyo "benki kuu" ya SMZ.

  ..toka 1966 mpaka 2001 ZNZ walikuwa wanahifadhi fedha zao wenyewe ktk PBZ.

  ..haya siyo maneno yangu, nimeyapata kwenye makala ya Mwanasheria Mkuu wa ZNZ akizungumzia masuala ya muungano yasiyo na majibu ya kuridhisha.
   
 18. J

  JokaKuu Platinum Member

  #18
  Feb 2, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,791
  Likes Received: 5,051
  Trophy Points: 280
  Topical,

  ..hii posting yangu ni ktk kutafuta faida za muungano kwa Tanganyika.

  ..so far nimekutana na hasara tupu. mfano mdogo ni jinsi Tanganyika inavyobeba mzigo wa kuwalipa wabunge toka ZNZ.
   
 19. T

  Topical JF-Expert Member

  #19
  Feb 2, 2012
  Joined: Dec 3, 2010
  Messages: 5,176
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  @JK

  Muungano si kwa ajili ya fedha za kodi tu..bali Tanganyika inapokea fedha nyingi sana za Zanzibar in the name of Muungano panua uwigo wa mapato utaona wapi Tanganyika inavyofyonza kutoka Zanzibar...ni bahati mbaya wazenj wapole sana..lol wangekuwa kama watu wa Arusha au Moshi ingekuwa balaa hapa
   
 20. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #20
  Feb 2, 2012
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Wenda ni kweli, lakini wazanzibar wakiachiwa wanaweza fanya vizuri zaidi na kuwa pato lao kubwa. Ninachoelewa wazanzibari hawataki ukilitimba unaofanywa na system za bara.

  Ukilitimba huu ndo unawafanya wazanzibari kudumaa. Mfano kuna mambo ili wafanye lazima wawaulize wakilitimba wa bara na bila kuwahidi 10% watakupiga dana dana na mipango yao mielevu inashindwa na hatimaye kudumaa kwa zanzibar.
   
Loading...