Baraza la mawaziri kivuli Z`bar lafutwa
Na Mwinyi Sadallah
Baraza la Wawakilishi Zanzibar limetangaza mabadiliko makubwa ya muundo wake ikiwemo kufuta baraza la mawaziri kivuli na nafasi ya kiongozi wa upinzani, baada ya kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar (GNU).
Hayo yameelezwa na Katibu wa Baraza hilo, Ibrahim Mzee Ibrahim, wakati akizungumza na waandishi wa habari, Makao Makuu ya Baraza hilo Chukwani mjini Zanzibar jana.
Alisema kwamba kufuatia kuundwa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa kanuni za Baraza la Wawakilishi zinalazimika kufanyiwa marekebisho kuanzia mkutano wa pili unaotarajiwa kuanza Januari 19, mwaka huu.
Mzee alisema Baraza la Mawaziri Kivuli limefutwa na nafasi ya kiongozi wa upinzani haitokuwepo tena na badala yake kutaanzishwa nafasi ya Mnadhimu Mkuu wa Serikali katika Baraza la Wawakilishi na kila chama chenye wajumbe ndani ya baraza hilo kitakuwa na mnadhimu mmoja.
Alisema mnadhimu mkuu wa Serikali katika Baraza la Wawakilishi atateuliwa na Serikali na Makamo wa pili wa Rais ndiye atakayekuwa mtendaji mkuu wa shughuli za Serikali ndani ya baraza hilo.
Kabla ya marekebisho hayo ya kanuni, Waziri Kiongozi ndiye aliyekuwa kiongozi mkuu wa Shughuli za Serikali, mfumo ambao umebadilika baada ya marekebisho ya kumi ya Katiba ya Zanzibar yaliyokaribisha Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Aidha alisema kwamba kuanzia sasa wakuu wa mikoa hawatokuwa wajumbe wa Baraza la Wawakilishi kwa vile marekebisho ya kumi ya Katiba ya Zanzibar yamewaondoa na watabakia watendaji tu katika mikoa yao.
Alisema kwamba kanuni za baraza la wawakilishi za mwaka 2009 zimefanyiwa marekebisho upya ili ziendane na mazingira yaliyopo sasa katika utendaji wa baraza hilo likiongozwa na Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Katibu huyo alisema kwamba Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi hivi sasa watakaa ndani ya baraza bila ya kuzingatia tofauti za vyama vyao isipokuwa safu ya mbele itaongozwa na mawaziri na manaibu waziri na kufuatiwa na wajumbe wasiokuwa na nyadhifa katika Serikali.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
Haya ndiyo wasio na macho huyabeza! Hongera Wazanzibari!