Zanzibar 2020 Zanzibar: Hali si shwari. Vurugu zaibuka na watu kadhaa wanadaiwa kujeruhiwa vibaya

pantheraleo

JF-Expert Member
Jan 5, 2013
690
841
KILICHOTOKEA MICHEWENI, ZANZIBAR

Watu walikuwa na mkutano wa Jimbo la Micheweni wamemaliza saa 12 watu wakaanza kurudi majumbani.

Kuna wanachama wa ACT, Shumba Mjini wakapita katika kijiji cha Kwale Kijiji ambacho kina CCM wengi.

Kilichotokea CCM wakawachokoza ACT wakaanza ugomvi wakaja Polisi. Usiku huu mabomu yanaendelea na Askari wanazidi kumiminika. Watu wanapigwa sana

Mpaka sasa kuna wengine wako hospitali Micheweni wengi wameumizwa.

EF4B280A-8824-440F-AD14-B717A7E67E89.jpeg


ILANI: Video niliyoipata haifai kukaa hapa kwani inatisha
 
Hahaha watanzania kwa kuzusha, sasa hapa vurugu ziko wapi?! Majeraha kama hayo hata Dispensary ya ikulu yapo.

Mtu anachukua picha hospitali analeta humu, anatia watu taharuki.

Hata ukienda Tandale Hospitali watu wanaokuja na majeraha madogo madogo kama hayo wapo, sasa jeraha linahashiria kwamba kuna vurugu?!

Kesho nami nitapiga picha hapa emergency room Muhimbili na nitaleta humu na kusema Dar es salaam hali siyo shwari kabisa.

Hapo nini kinasema kwamba kuna vurugu Zanzibar?!
 

Similar Discussions

8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom