Kuna jambo moja lipo wazi; kwamba Wazanzibari wengi hususani wale walio nje ya system (hususani Watendaji wakuu CCM) hawautaki muungano. Aidha, Wazanzibar waishio nje nao, kwa uwingi wao ndo hawataki kabisa kusikia lolote kuhusu muungano. Wengi wa hawa, wanaamini kwamba Zanzibar iliburuzwa tu kuingia kwenye muungano na hadi sasa hakuna cha maana wanachofaidika nacho kutokana na muungano huo!
Kama nilivyotangulia kusema hapo awali, Zanzibar iliburuzwa kuingia kwenye muungano. Hali kadhalika, hata Watanganyika nao waliburuzwa na wanaendelea kuburuzwa kuwepo ndani ya muungano huu. Hakuna kura yoyote ambayo ilipata kufanyika ya kuwauliza wananchi wa pande hizi mbili kuhusu kuafiki kwao kuwepo ndani ya ndoa hii ya mkeka.
Pamoja na yote hayo, tofauti na ilivyo huku bara, Zanzibar kwa miaka yote wamekuwa wakitafuta nafasi ya kujipatia Zanzibar yao kama Taifa. Kwa bahati mbaya kabisa, fursa hiyo hawakuipata kutokana na ukweli kwamba Tanzania kwa ujumla ilionekana ni sawa na dhambi ya mauaji kuzungumzia suala la kuvunjwa kwa muungano. Wachunguzi wa mambo wanaamini kwamba, baada ya mifumo mingi ya Nyerere kushindwa; hususani siasa ya ujamaa na kujitegemea pamoja na Azimio la Arusha, CCM walibakiwa na turufu moja tu ya kuaminisha uwezo wao. Nayo ni MUUNGANO! Na kutokana na hilo, MUUNGANO umeonekana kulindwa kwa gharama zozote zile pasipo kuzingatia matakwa ya wananchi.
Baada ya Wazanzibari kusubiria kwa muda mrefu fursa ya kujipatia taifa lao; hatimae wakaamini kwamba fursa hiyo imeshawadia! Waliamini kwamba mchakato wa upatikanaji wa katiba mpya utawapatia fursa ya kutoa maoni yao kwamba hawapo tayari kuwepo ndani ya muungano!! Inavyoelekea, hawakubaini mapema kwamba rasimu ya katiba mpya ilishatamka wazi kwamba tumetaka tusitake; muungano lazima!
Bila shaka, ni kauli ya JK wakati akiiapisha Tume ya Katiba Mpya ndiyo iliyoamsha ari na ghadhabu za Wazanzibari. Bila kutafuna tafuna maneno na katika hali iliyoonekana kuwapa vijembe wale wote wanaofikiria kuvunja muungano; JK akatamka wazi kwamba kitakachojadiliwa ni aina ya muungano na sio suala la kuendelea ama kutoendelea kwa muungano. Hapo ndipo, baadhi ya Wazanzibari walipokuja kubaini kwamba ndoto ya kuamua mustakabali wa taifa lao imeyyoyoma. Na hapo ndipo wana-Uamsho walipoongeza nguvu ya kuendesha mihadhara dhidi ya muungano. Ni bahati mbaya sana kwamba ingawaje kikundi hiki kina madai ya msingi, wametumia approach ambayo inatia shaka uhalisia wa madai yao.
Hivyo basi, suluhisho la tatizo hili ni kutoa fursa ya kuwepo kwa kura juu ya kama tuendelee na muungano au tusiendelee nao. Haikuwa busara hata kidogo kuweka kizingiti cha wananchi kujadili suala hili. Muungano unaohitajika ni wenye ridhaa za wananchi na sio kushinikizwa na viongozi.