Zanzibar hakukaliki; siri nzito yafichuka fedha zatoka Oman na Uingereza | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanzibar hakukaliki; siri nzito yafichuka fedha zatoka Oman na Uingereza

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Jun 3, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145

  Siri nzito ya machafuko yanayoendelea mjini hapa, imefichuka.

  Habari za kuaminika zilizopatikana jana kutoka Zanzibar, zinasema kuna kundi kubwa la wafanyabiashara wa Kizanzibari wanaoishi katika nchi za Oman na Uingereza, wanadaiwa kutoa fedha nyingi kufadhili vikundi vya kidini na wanaharakati kushinikiza Muungano uvunjwe.

  “Tunasikitishwa mno na machafuko haya, yameiaibisha Zanzibar, ambayo baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, ilitulia… lakini tunasikitishwa na tukio hili ambao linafadhiliwa na Wazanzibari wenzetu wanaoishi Oman na Uingereza.

  “Watu hawa wanamekuwa wafadhili wakubwa wa kutoa fedha kwenye vikundi vya kidini na wanaharakati, jambo ambalo tunaona ni hatari kubwa kwa amani kisiwani hapa, tunavishauri vyombo vya dola, vichukue hatua,” kilisema chanzo chetu.

  Aidha chanzo hicho, kinasema kutokana na nguvu kubwa ya fedha, vikundi hivyo vimekuwa na ushawishi mkubwa kwa vijana ambao wengi wao hawana kazi maalum za kufanya.

  “Utashangaa kuona, baada ya kutokea machafuko haya, wengi walioonekana walikuwa vijana tu, huoni watu wazima, akina baba au akina mama… ni wazi utaona fedha zina nguvu kubwa kwa vijana wetu, ukiangalia wale waliondamana juzi ni vijana wenye umri kati ya miaka 18 hadi 24.

  “Lakini pia tumebaini kwamba, mbali ya vikundi hivi, kuna chama kimoja cha siasa kisiwani hapa, kwa namna moja au nyingine kina mkono wake ndani ya machafuko haya, kimekuwa bingwa wa kuchochea uvunjifu wa amani,” kilisema chanzo chetu.

  Chanzo hicho kiliiambia MTANZANIA kwamba Wazanzibari hao wamekuwa na ushawishi mkubwa wa kuwashinikiza wananchi waibane Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ili iitishe kura ya maoni.

  “Issue ya Muungano ni muhimu, lakini hawa jamaa wanafanya hivi ili kuishinikiza Serikali iitishe kura ya maoni ili kuona kama kuna watu wanaukubali Muungano au la! Jambo hili si baya, lakini walitakiwa kupitia njia ambazo ni sahihi,” kilisema chanzo chetu.

  Kwa upande wake, Mjumbe wa Umoja wa Vijana wa CCM Taifa, Daud Ismail, lisema matatizo yanayoendelea Zanzibar, ni vema Serikali ipitie ripoti mbalimbali zinazohusu kero za Muungano.

  “Ili kuweza kuondokana na hali hii, ni vema Serikali zote mbili zifanyie kazi ripoti za Hassan Moyo, William Shelukindo, Amina Salum Ally na ya aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mzee Edwin Mtei, ambazo zote zilieleza wazi tatizo linatotekea sasa Zanzibar.

  “Leo huwezi kudhibiti hali hii ya machafuko kwa kukaa mezani na Jumuiya ya Uamsho, kufanya hivi ni sawa na kuchochea jambo hili ila kinachotakiwa hapa ni kufanyia kazi jambo hili kwa undani.

  “Wazanzibari kwa muda mrefu, wamekuwa wakilalamika kuhusu hata namna ya mapato yanavyopendelea upande mmoja wa Tanganyika, na katika kulithibitisha hili, hata ripoti ya mshauri wa Zanzibar ya mwaka 2010, imeeleza wazi, kwa hili ni lazima chama changu cha CCM kitoe tamko na si kunyamaza kimya,” alisema Daud.
   
 2. bucho

  bucho JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2012
  Joined: Jul 13, 2010
  Messages: 4,547
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  [​IMG]
   
 3. MNYISANZU

  MNYISANZU JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 21, 2011
  Messages: 7,056
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  The way forward ni kuruhusu muungano ujadiliwe kwenye katiba mpy
   
 4. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Hatari, Tunawapenda Wazanzibari lakini kama wanaoishi UK pia wanatuma pesa kupinga Muungano kwa Usalama ni haki

  Yao kwa Ukweli, lakini hizo Vurugu bado kuna uwalakini kama kweli walifanya walioandamana sababu serikali yetu pia ni

  Janja. Kwahiyo Wakristo waangalie suala hilo kiuwalakini na kwa ustaarabu;
   
 5. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
   
 6. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #6
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,911
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  ccm na viongozi wake walishazoea kuwa kila kitu "ni upepo tu utapita". Matokeo yake ndiyo hayo tunayoyashuhudia na tutakayoendelea kuyashuhudia zanzibar siku zijazo.
   
 7. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #7
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Hatutaki matamko, tunawasubiri bungeni Hamadi Rashid mb na Habib Mnyaa, walituambia kupitia bunge kuwa muungano ni stronger than ever! wakidhani wanamshushua TUNDU LISSU.
   
 8. M

  Moses msisia Member

  #8
  Jun 3, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 57
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  akate haraka basi hilo tawi .mbona anachelewa?
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jun 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  mule ndan si kila kinachoongewa kina maana,,,,,,mengine uyaache tu,,,,,mangap yameongewa mule na yamefanyiwa kazi??????
   
 10. e

  evoddy JF-Expert Member

  #10
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 302
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Kuna maswali ni lazima tujiulize kama ifuatavyo

  1.Je!Ni kwanini watanganyika tunajifanya sana kuwajali hawa wazanzibar kuliko wao wanavyojijali?Kama wanahitaji nchi yao kwa nini tusiwaachie ili kama wanataka kuwa kama Somalia na basi wawe?

  2.Sisi Watnganyika tunachokiogopa nini kwani kabla ya 1964 si tuliishi bila kuwa na huo muungano?Acha wazanzibar wabaki huko zanzibar siku wakitaka tuwasaidie basi na sisi tutaangalia kama tukubali au tukatae.

  3.Kumekuwa na hii propaganda kuwa Muungano wetu ni kwa ajiri ya usalama zaidi ,hivi naomba niulize tena kabla ya 1964 mbona usalama wa tanganyika ulikuwa sawa?
   
 11. e

  ebrah JF-Expert Member

  #11
  Jun 3, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Elimu ya ziada inahitajika, Mi ni mtanganyika na Siimi umuhim wamuungano Wala fairs yake zaidi wanatunyonya tu!
   
 12. T

  Tiger One JF-Expert Member

  #12
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 11, 2012
  Messages: 569
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  Let them go!!!
   
 13. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #13
  Jun 3, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Kubalini kutumiwa kupika propaganda na serikali, kwani kufadhiliwa ni stori za leo hizo? mbona hata baadhi ya vyama tulishaambiwa vinafadhiliwa kwa mapesa toka nchi fulani za magharibi na kuna ushauri ulitolewa wa serikali kuwa "makini", au hamjasikia hilo?

  Hili la vijana wa umri wa 18-24 unawadharau hao? hao ndio wana mapinduzi nchi zote (Youth) ndio wapiganaji fuatilia....., kisha mjumbe, Tanzania ni mingoni mwa nchi zenye young population ambapo estimates za sensa iliyopita zinaonyesha kuwa karibu 65% ya total population wapo below 24 years of age.

  Serikali ilete hoja, sio propaganda...

  Inaboa aisee
   
 14. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #14
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Abunuwas, aliambiwa na mpita njia kuwa asikate tawi alilokalia; yeye kwa ubishi tu akalikata na hatimaye akaanguka chini na kuvunjika miguu yote miwili na almanusura kifo! Ilibidi akamuulize yule mpita njia siku yake (Abunuwas) ya kufa ni lini!
   
 15. S

  Sweetbert da Sucre Member

  #15
  Jun 3, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Labda muungano ni muhimu,lakini nafikiri si wa lazima kiasi cha kutupasa kuutetea hata kwa ghalama ya kumwaga damu kama dalili zinavyoonesha.Lakini pia tusizipe dalili hizi jina jingine labda na zuri zaidi ya jina lake halisi la "DALILI ZA VITA"
   
 16. N

  Ngoiva JF-Expert Member

  #16
  Jun 3, 2012
  Joined: Nov 17, 2011
  Messages: 236
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mungu isaidie kikundi cha uamsho wafikishe lengo. Huu muungano ni wa kijanja janja kwa karne hii ni aibu mtupu
   
 17. ndenga

  ndenga JF-Expert Member

  #17
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 1,697
  Likes Received: 429
  Trophy Points: 180
  Kwa upande wangu ningeshauri Muungano uvunjwe.. Mpaka pale tutakapoujadili tuone jinsi ya kuungana upya kwa kuangalia maslahi ya pande zote. Kwa hiyo viongozi wa Zanzibar walioko kwenye SJM warudi kwao kuweka mikakati mipya ya muungano. Otherwise malalamiko ya kuonewa hayataisha na yataendelea kuchochea chuki zisizo na maana.
   
 18. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #18
  Jun 3, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Iitishwe kura ya maoni kama huu muungano unahitajika au la. Kuendelea kuung'ang'ania na kuutetea wakati kuna watu hawauhitaji ni uwendawazimu!
   
 19. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #19
  Jun 3, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,316
  Trophy Points: 280
  Tawi lenyewe halizaagi chochote zaidi ya kuwapa maskani popo.
   
 20. Ulukolokwitanga

  Ulukolokwitanga JF-Expert Member

  #20
  Jun 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 8,418
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Hao vijana wa Zenji asilimia 80 ni mateja. Walivamia bar wanazodai ni za wabara na kupora pombe zote wakanywa, mbaya zaidi Valeur ndio ziliibiwa sana. Wakavamia kanisa katoliki la Mpendae wakapora divai yote wakanywa. Huenda hata mabucha ya kitimoto na vibanda vya kukaangia viliporwa. Vijana wa Zenji mmeyagalagaza maadili ya mzanzibari, ni aibu sana kwa kweli
   
Loading...