Ndugu zetu wa Zanzibar hawataweza kuendelea kwa sababu serikali yao ni kubwa sana ukilinganisha na idadi ya watu. Zanzibar ina budget ya $400 million tu na watu wasiozidi 1,500,000!. Zanzibar serikali yao ni kubwa kiasi kwamba inawezekana $200 million inatumika kuwahudumia viongozi tu kuanzia wabunge, mawaziri, ikulu, wakuu wa mikoa, wakuu wa jeshi na polisi. Zanzibar inatakiwa kuwa na serikali ndogo sana. Zanzibar ina watu kama mji wa mwanza lakini angalia ni watu wangapi wanategemea serikali. Je pesa ya shule itatoka wapi?, pesa ya hospitali itatoka wapi wakati hospitali moja ya kisasa ya rufaa inaweza kujengwa kwa hadi $80-$100m hivyo ndugu zangu wa Zanzibar kama kweli tunataka maendeleo tuanza na ukubwa wa serikali.