Zanzibar haina uwezo wa kuwa na sarafu yake

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
← Posted on July 9, 2012 by zanzibaryetu


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Fatma Abdulhabib Fereji akibadilishana maweazo na Dk Bakari S, Asseid nje ya ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Mbweni nje ya mji wa Zanzibar


SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema kuwa haiwezi kuanzisha sarafu yake (fedha zake) kutokana na kuwa katiba ya jamhuri ya muungano wa Tanzania hairuhusu kufanya hivyo.

Hayo yameelezwa na waziri wa nchi ofisi ya rais fedha, uchumi na mipango ya maendeleo, Omar Yussuf Mzee wakati kijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mji Mkongwe (CUF) Ismail Jussa Ladhu aliyetaka kujua sababu za Zanzibar kutokuwa na sarafu yake ili kuimarisha uchumi wake.

Jussa alisema sarafu ya Tanzania inaendelea kushuka thamani dhidi ya fedha za kigeni (dola) siku hadi siku na kufanya Zanzibar kuwa katika hali ngumi kiuchumi ikiwemo wananchi wake kukabiliana na mfumko wa bei na kupelekea maisha kuwa magumu.

Akijibu suali hiyo Mzee alisema kimsingi Zanzibar ina uwezo wa kiuchumi wa kuanzisha sarafu lakini katiba iliyopo hivi sasa sarafu ni suala la muungano na hivyo haitoi fursa kuanzisha sarafu yake.

"Sio kweli kwamba sarafu ya Tanzania inaendelea kushuka thamani siku hadi siku lakini ni kweli kwamba thamani ya shilingi yetu (Tanzania) ikilinganishwa na ile ya dola za kimarekani imekuwa na muelekeo wa kushuka" alisema waziri.

Akitaja sababu nyengine za kushindwa kuwa na sarafu Zanzibar, Mzee alisema hivi sasa nchi za Afrika Mashariki zimo katika mchakato (Process) za kuelekea katika kuwa na muungano wa fedha ambao utakapokamilika nchi zote katika jumuiya hiyo zitakuwa na sarafu moja tu.


"Mheshimiwa Spika kufuatia upepo huo unaovuma kuelekea katika sarafu moja haitayumkinika kwa Zanzibar kujitenga kwa kuanzisha, kuhudumia na kusimamia sarafu yake hata kama ina uwezo wa kiuchumi kufanya hilo" aliwaambai wajumbe hao.


Akielezea zaidi kuhusiana na sababu za kushuka thamani ya fedha ya Tanzania alisema ni kutokana na urari wa malipo ya nchi za nje, tofauti ya mfumko wa bei na nchi zinazofanya biashara na Tanzania na kuchafuka kwa masoko duniani.


Pia alitaja kuwepo kwa mahitaji makubwa ya fedha za kigeni kwa ajili ya miradi ya miundo mbinu kutokana na kuchelewa kwa fedha za wahisani na mikopo, na hisia za upungufu wa fedha za kigeni kuwa ni miongoni mwa sababu za kushuka thamani ya fedha za Tanzania.



 
..waache visingizio.

..mbona waliweza kuondoa mafuta ktk masuala ya muungano??
 
Back
Top Bottom