ZANZIBAR HAINA FISADI hata mmoja

Mwiba

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
7,607
1,744
`Zanzibar haina fisadi`
2008-06-27 11:05:04
Na Mwinyi Sadallah, Zanzibar


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu, Fedha na Uchumi, Dk. Mwinyihaji Makame, amesema si vyema masuala ya ufisadi ya Tanzania Bara kuvushwa bahari na kupelekwa Zanzibar.

Kadhalika amesema Serikali ya ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) inafanya kazi kwa uadilifu na viongozi wake ni safi na hivyo kuliambia Baraza la Wawakilishi kuwa, Zanzibar hakuna ufisadi.

Akifunga mjadala wa bajeti ya SMZ kwa mwaka 2008/09 alisema serikali inafanya kazi kwa uadilifu, hasa katika utoaji wa misamaha ya kodi na kuzikataa shutuma zilizotolewa na baadhi ya wawakilishi kuwa misamaha ya kodi ni mingi na kwamba inawanufaisha baadhi ya wajumbe wa baraza hilo.

Alisema: ``Mambo ya EPA na ufisadi tusiyalete hapa. Sisi tupo safi na matunda tunayaona. Tusiyachukuwe mambo hayo (ya Tanzania Bara) na kuyaleta hapa.``
< BR>Hata hivyo, alikiri kutolewa misamaha ya kodi yenye thamani ya Sh. bilioni 19.6, kiwango kikubwa ikilinganishwa na makusanyo Sh bilioni 20.4 kupitia Idara ya Forodha Zanzibar.

Alifafanua kuwa misamaha hiyo ilitolewa kwa kuzingatia sheria na kunufaisha sekta ya uwekezaji, ujenzi wa Benki Kuu Zanzibar, bandari ya Zanzibar, taasisi zisizokuwa za kiserikali na mashirika ya umma na dini.

Waziri alisema misamaha ya kodi inapotolewa, wakaguzi wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) huhakikisha kuwa inatumika kama inavyokusudiwa.

Alisema ufisadi wa Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) uliojitokeza katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) unashughulikiwa kwa kuzingatia taratibu na sheria na kuwataka wawakilishi kuacha kuhamishia suala hilo barazani.

Alisema SMZ inafanya shughuli zake kwa uwazi, ndiyo maana kila mwaka inaweka wazi ripoti ya misamaha ya kodi iliyotolewa kwa taasisi mbali mbali.

Akizungumzia uchumi wa Zanzibar alisema umekuwa ukipanda na kushuka kutokana na sababu mbali mbali, na kwamba kuongezeka kwa omba omba isiwe kipimo cha kufikia uamuzi kuwa uchumi umeporomoka.

Alisema hata nchi zilizoendelea zina omba omba mitaani kwa maelezo kwamba kuomba ni tabia ya mtu.

Katika jitihada za kupunguza ukali wa maisha, Waziri alisema, SMZ imejenga uwezo wa mapato na imeweza kuchangia miradi kadhaa ya maendeleo, tofauti na hali ilivyokuwa katika miaka ya nyuma.

Akijibu maombi ya wawakilishi kwamba kodi ya mapato inayokusanywa Zanzibar na TRA, ikusanywe na ZRB, Waziri alisema hilo haliwezekani kwa vile huu ni utaratibu uliowekwa kikatiba.

Kwa sasa Serikali ya Muungano na ile ya Zanzibar zipo katika kufanya utaratibu wa kurekebisha kero za Muungano ili kuhakikisha kila upande unanufaika.

Wakati wa mjadala wa bajeti, Mwakilkishi wa Mji Mkongwe (CUF) Bi. Fatma Habib Ferej alisema kulingana na ripoti ya TRA ya mwezi uliopita, kumekuwepo misamaha mingi ya kod i inayohusisha wawekezaji, taasisi za dini, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na pamoja na mashirika ya umma.

Alisema kwa mwaka 2005/06 mapato yaliyokusanywa ni bilioni 14.5 wakati misamaha ya kodi ulikuwa na Sh. bilioni 11.7, kiwango ambacho alikiona ni kikubwa ikilinganishwa na mapato yaliyokusanywa.

Mwakilishi huyo alisema mazingira ya utoaji misamaha hiyo yanatia wasiwasi wa kuwepo kwa ufisadi kwa vile serikali imepoteza mapato mengi ambayo yangeweza kutumika katika bajeti ya mpango wa maendeleo wa wananchi.

Alisema misamaha ya kodi hivi sasa kupitia Idara ya Forodha Zanzibar imeongezeka kwa asilimia 68 wakati bajeti ya serikali inaendelea kutegemea ruzuku na misaada ya wahisani.

Baraza lilipitisha bajeti ya makadirio na matumizi ya Sh. bilioni 341.7, lakini wawakilishi wa upinzani hawakuunga mkono kwa madai kuwa hailengi kupunguza makali ya maisha ya mwananchi wa kawaida.
 
Ni vema Dr. Makame angefahamu ufisadi una maana gani. (http://kamusiproject.org/)

1. Fisadi: (corrupt person) ni &#8211; Mhongaji, Mpotoshaji

2. Fisadi: destroyer - Mvunjaji, Mwagamizi

3. Fisadi: evil person &#8211; Mleta balaa; Mbaya, Mwovu, Mkorofi; Mshari, Mleta ubaya

4. Fisadi: libertine - Mpotezaji

5. Fisadi: seducer - Mshawishi; Mtongozaji

Je Serikali ya Zanzibar ambayo inaendeshwa na Wanadamu ni kweli wote ni safi?

Na kisha aelezee baadhi ya malalamiko ya muda mrefu kuhusu Zanzibar yakiwemo yale ya Vigogo kudai asilimia mpaka 30% kutoka wazabuni mbalimbali na pia ukweli kuwa Mtoto wa Muungwana wa huko amekuwa akipendelewa na kupewa tender hata pale ambapo haja-qualify na pale ambapo ameshindwa basi tender hizo huitishwa tena mpaka ashinde.
 
kwani wale ndio mafisadi wote Tanzania? mafisadi wa PPF, EPA, Richmonduli, TICTS, ATCL to name a few wote wako kwenye list ya kina Slaa?

Kwa definition ya fisadi iliyotolewa hapo juu, Karume naye ni fisadi
 
kwani wale ndio mafisadi wote Tanzania? mafisadi wa PPF, EPA, Richmonduli, TICTS, ATCL to name a few wote wako kwenye list ya kina Slaa? Kwa definition ya fisadi iliyotolewa hapo juu, Karume naye ni fisadi

Kwa mujibu wa Mbunge wa bunge la jamhuri ya Tanzania. Mwizi mpaka avunje nyumba, hivyo na mimi nafuata mfano wake fisadi lazima awepo kwenye list ya Slaa. kwi kwi kwi.
 
Ufisadi uko in a form of complex food web, kuna masters wao ambao ndio wanapigiwa kelele nyingi-baadhi wamo kwenye list ya Slaa. Sasa kuna mafisadi viwembe wenyewe, hawa ndio ambao hatuwajui lkn ndio wamehusika kwa kiasi ila hawana majina makubwa. Hawa ndio wabaya zaidi.
 
wape muda tu, hata bara miaka 3 iliopita tulisema hivyo hivyo! hakuna ufisadi na wala hatukuujua ufisadi. I promise wao watakuja na kali kuliko hii ya ufisadi wa bara. Ukiona mwenzio ananyolewa ...........! ni ushauri tu kwa wazenj.
 
Mafisadi wengi wa bara wanajinufaisha kwa pesa, kwa kupindisha mikataba. Mafisadi wa Zanzibar wanajinufisha zaidi kwa madaraka hata wanaposhindwa chaguzi, kwa kupindisha matokeo ya uchaguzi.
 
wape muda tu, hata bara miaka 3 iliopita tulisema hivyo hivyo! hakuna ufisadi na wala hatukuujua ufisadi. I promise wao watakuja na kali kuliko hii ya ufisadi wa bara. Ukiona mwenzio ananyolewa ...........! ni ushauri tu kwa wazenj.

Zanzibar bajeti yake ni bilioni 178 za kibongo. Ukiangalia kwa makini hiyo ni kashfa moja tu ya Richmond, sawa na bajeti ya mwaka mzima ya Zanzibar. Kama ufisadi wao unaweza kuwa mkali zaidi ya Bongo, then....
 

``Mambo ya EPA na ufisadi tusiyalete hapa. Sisi tupo safi na matunda tunayaona. Tusiyachukuwe mambo hayo (ya Tanzania Bara) na kuyaleta hapa.``

Hili tamko ni anti-union.

Lina maana matatizo ya Bara wao hayawahusu, na hayawanyimi usingizi.

Pia, hata kama hayawahusu, hakutakiwa kutupiga dongo nje nje hivyo na matatizo yetu.

Sidhani kama huyu Kiongozi ni Haini anaetaka kuvunja Muungano, japo unaweza kusema kwa sentensi hiyo moja tu ya kichochezi, mtu wa Bara anaweza kuwa justified kudai tuvunje na Muungano wenyewe. Ila ni uwezo mfupi tu wa kufikiri. Hawana idea nini cha kusema hadharani hawa watu.

By the way: Huu Muungano nao usiwe tabu!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom