Zanzibar 2020 Zanzibar: Hafla ya kuapishwa Rais mteule Awamu ya Nane, Dkt. Hussein Mwinyi Uwanja wa Amaan

Asante, tunafuatilia kwa makini, na haswa hotuba yake ya leo, itaponya vidonda vyote vilivyosababishwa na uchaguzi huu, japo makovu yataendelea kubaki.
P
Vidonda tena...... !!!!?? Mbona anasema anamshukuru rais wa JMT mh. JPM kwa kufanikisha uchaguzi kwa "salama". Uchaguzi ulioisha kwa salama unakua na vidonda tena.
 
KWA wenye macho na akili nzima ni vizuri kumsoma GHASSANY....KWA HERI UKOLONI,KWAHERI UHURU.Ni utafiti bora wa siasa na mustakhabhali wa Zanzibar ikitizamwa kihistoria
 
Kwa yanayoendelea Maalim Seif kwa sasa hawezi tena kukataa cheo cha Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

Funzo alilipata mwaka 2015 baada ya kugomea uchaguzi wa marudio akitegemea serikali ya Mapinduzi Zanzibar itakwama.

Yaani kwa sasa atawatosa ACT-Wazalendo kama watamshinikiza asiwe sehemu ya serikali ya Dkt. Mwinyi.
Hivi kwani Maalim Seifu ni Mpinzani? Mpinzani ambaye anapokea mshahara wa serikali kwa cheo kikubwa alichokuwa nacho enzi hizo akiwa CCM. Poleni Upinzani wa kweli.
 
Uzi umedoda kuliko kiporo cha wali dagaa wa Mwanza. Hata kapicha hakuna. Yaani mbona mko kisimanzisimanzi sana. Nilikuwa mitaa yenye Watu wa Kisiwani wengi leo ila utafikiri hakuna kinachotokea huko Kisiwani.
 
Asante, tunafuatilia kwa makini, na haswa hotuba yake ya leo, itaponya vidonda vyote vilivyosababishwa na uchaguzi huu, japo makovu yataendelea kubaki.
P
Huyu bwana anatawala katika dhulma na dhambi kubwa sana. Hatapata baraka .
Muulizeni Shein nafsi inavyomsuta na jinsi alivyochakaa. Vidonda haviponi kwa maneno bali haki
Muafaka 1 ,2 n.k vimeshindikana seuse maneno uwanjani.

Shamsi Vuai aliyeifia CCM na kuhalalisha dhulma, akiwasaliti wenzake yamemkuta
Jina lake ndilo lilikuwa chaguo at least la Wazanzibar, lililpofika machanjioni Dodoma, tupa kule. Analipa dhambi

Sasa huyu bwana wa Mkuranga(Mbunge) ndiye bosi.
 
Hongera sana Rais Mwinyi,tunategemea mambo makubwa kutoka kwako.


Uchaguzi umeisha sasa tujenge nchi.

URT- JPM
SMZ- Mwinyi
 
Kuna rais Fulani wa Zanzibar aliitwaga komandoo enzi zile. Juzi kwenye uapishi alikuwepo! I mean Salmin Amour Juma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom