Zanzibar: CUF walalamika kuporwa ofisi na ACT Wazalendo. ACT yawajibu waende kudai Mahakamani na sio kwenye press

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, amesema kuwa kama chama cha CUF wanadai kuwa ofisi zao zilizopo visiwani Zanzibar, zimechukuliwa na chama hicho, basi wapeleke malalamiko yao Mahakamani na siyo kwenye vyombo vya habari, na kutaja tarehe rasmi ya kuanza mchakato wa watia nia.

Hayo ameyabainisha leo Juni 19, 2020, wakati wa mazungumzo maalum na EATV&EA Radio Digital na kusema kuwa chama hicho kuanzia Juni 22, 2020, kitafungua rasmi mlango kwa watia nia wa kugombea nafasi za Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania na kwamba kimejipanga vilivyo na hakiendi kwa kufuata mkumbo bali wanaenda kwa kuwa wamefanya maandalizi muhimu.

"Mtu anasema ana ofisi mwambie aoneshe hati ya kiwanja, CUF hawana jengo wala gari hata moja, hizo ni mali za watu binafsi ambao walikiazima chama cha CUF wamekichoka, wamechukua mali zao, ingelikuwa mtu kachukua mali ya mtu, wangekamatwa na kuwekwa ndani kwa uvamizi, iweje sisi ambao tumechukua mali tuwe tunadunda barabarani na wengine wanazidai kwa Press conference, mali zinadaiwa Mahakamani waende" amesema Ado Shaibu.

Aidha Katibu Mkuu huyo ameongeza kuwa, "ACT ni chama ambacho kinaenda kuonesha kwamba ni mbadala wa uhakika kinachobeba maono na matumaini ya Watanzania na kesho sisi tutatoa mwelekeo mpya wa chama chetu tutaonesha sehemu ya nguvu zetu, Zitto na Maalim watazungumza na huo ndiyo utakuwa mshindo wa kwanza".
 
Back
Top Bottom