VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,136
- 17,871
Nipo hapa Unguja, Zanzibar.Nimefika jana na kesho nitaelekea Pemba. Nawaona wazanzibari na maisha yao. Bado wako pamoja. Bado wamoja. Wanapendana na kusaidiana. Wanasikilizana na kutaniana. Wanaishi pamoja kwa amani na utulivu.
Wananchi walichagua viongozi wao. Matokeo yakafutwa na Jecha. Wananchi wamestahimili hayo. Wako pamoja wakijikongoja kimaisha. Wanasonga mbele. Mambo yanaendelea. Wananchi wako tayari kurudia uchaguzi. Wako tayari kuwachagua tena wale wale waliofutwa kiutata.
Wananchi wanaimani kwa CCM na CUF. Wanaviamini vyama hivi kuliko kisiasa. Wanaviamini na kuviishi. Wanaviamini na kuviishi. Ni kama Simba na Yanga katika soka. Upinzani huwepo lakini maisha ndiyo ya maana zaidi. Wazanzibari hawa si wale. Hawa wengine na wanataka mambo mengine.
CUF, shirikini uchaguzini hapo Machi 20 mwaka huu. Mnapendwa kuliko kupondwa. Mnaungwa mkono kuliko kufika kikomo. Mnasemwa kwa mazuri kuliko yale ya kiburi. Mnasifiwa kuliko kukashfiwa. Nipo hapa, ingawa ni mgeni, lakini nayaona ninayoyaandika.
Natoa rai kwa ZEC. Uchaguzi uwe huru na wa haki. Si uchaguzi wa Zanzibar, ni uchaguzi wa watanzania. Kila la kheri CUF katika kufika katika ninachowashauri. Shirikini uchaguzini. Kama ipo, ipo tu!
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Unguja, Zanzibar)