Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,682
- 149,884
Marudio ya Uchaguzi wa Zanzibar bila shaka yatatawaliwa na ushindi mkubwa wa CCM kwasababu ya CUF na vyama vingine kujitoa kwasababu walizozieleza kwa umma.
Hata hivyo,uamuzi wa CUF kujitoa ambao CCM hawakuutarajia,bila shaka umewakwaza sana CCM na utakuwa umewaathiri kisaikolojia kwani nafsi zao zitakuwa zinawasuta na hata kuona aibu kwa walichokifanya tofauti na kama CUF na vyama vingine vilivyokataa kushiriki uchaguzi huu wa marudia vingekubali kushiriki.
Kwa uchaguzi huu hata ukiona shamra shamra za ushindi jua wazi kuwa hazitoki moyoni bali ni shamra shamra tu kwasababu ni lazima ziwepo kuonyesha furaha lakini miyoni mwao ujue hali ni tofauti kabisa na wala hazitadumu hata kwa siku mbili.
Pia,kisaikolojia, CUF wamewaonyesha na kuwajengea imani watanzania kuwa wao si watu wa vurugu na fujo bali watu wa fujo na vurugu ni watu wa chama kingine kabisa ambao ndio chanzo cha yote haya.
Iwapo CUF wangeamua kuandamana na kukabiliana na Jeshi la Polisi na pengine kuleta madhara makubwa kwa jamii,ingepigwa propaganda kuwa CUF ni chama cha fujo na ghasia na hii ingekaa katika kumbukumbu za watu kwa muda mrefu na watu wangejenga mtazamo hasi kisaikolojia dhidi ya CUF.
Hivyo kwa uchaguzi huu kufanyika kwa amani bila vurugu wala ghasia za aina yoyote,mshindi kwa namba atakuwa ni CCM ila kisaikolojia (ushindi ambao ni muhimu zaidi) CUF ndio watakuwa wameshinda.
Hisia na fikra za watu juu ya ustaarabu na uvumilivu wa CUF katika uchaguzi huu, zitadumu kuliko hisia na fikra za ushindi wa CCM kwa idadi ya kura watakazopata kulinganisha na CUF pamoja na vyama vingine.
Uchaguzi huu wa marudio wa Zanzibar na ule wa kumpata Meya wa jiji la Dar-es-salaam,unatosha kabisa kutoa picha kwa mtanzania kuwa ni chama gani ni ni chama cha fujo na kisichoheshimu demokrasia na ni chama gani ni chama wa wastaarabu na wavumilivu.