Zanzibar Baada Ya Uchaguzi wa Kesho

Jenerali Ambamba

JF-Expert Member
Sep 8, 2014
3,344
2,534
Kama tujuavyo sote, kesho ndiyo uchaguzi ule wa marudio utafanyika Zanzibar, sasa yafuatayo yatatokea.

1: Rais Dr. Ali Mohamed Shein kama ilivyo ada na kama inavyotarajiwa atatangazwa mshindi wa uchaguzi huo hata bila kushinda au kwa mazingira yaliyokwishaandaliwa barabara, baada ya kutangazwa mshindi, kwa katiba iliyopo ya Zanzibar makamu wa kwanza wa Rais tayari "Amishaandaliwa"

yafuatayo yatajiri...

Maalim Seif Sharrif Hamad, anaweza kutangazwa kuwa mshindi wa pili baada ya Shein, hivyo mazungumzo yakaanza ya namna ya kumshawishi Shein na Chama chake waingie Serikalini.

Au...

Mojawapo ya vyama shiriki katika uchaguzi huo ukiondoa CUF tayari kimeandaliwa "Ushindi wa Mezani" kwa nafasi ya pili ili kiweze kutwaa nafasi ya umakamu wa kwanza wa Rais.

Katika Baraza la wawakilishi, mwelekeo ni huo huo kwamba, Wagombea wa CUF watatangazwa kushinda nafasi zao za Ubunge wa Baraza ili mazungumzo ya kuwalainisha wakubali yaanze maramoja.


Au

CCM na ZEC itawagawia na kuwatangaza wagombea wa vyama vidogo vidogo sio CUF nafasi za Uwakilishi ili kwendana na matakwa ya kikatiba ikiwemo uundwaji wa serikali.

Lakini vile vile, CCM wanajua kwamba ikiwa watatumia njia ya kwanza ya kuwatangaza Maalim Seif kuwa mshindi wa pili na Wagombea wa CUF kuwa washindi katika Baraza LA wawakilishi, CUF wanaweza kuendelea kugomea matokeo hayo au ushindi huo kwa kutoyatambua kabisa hivyo "Mgogoro wa kisiasa na kikatiba kuendelea" kufukuta hivyo sidhani kama watakubali hili litokee, ni suala la kusubiri na kuona.

Sasa kuna kituko kingine hiki hapa.

Yawezekana lengo la CCM na Serikali siyo wao kushinda ila ni namna ya kutaka kujisafisha mbele ya macho ya jumuia ya kimataifa na kwa wananchi, hivyo hesabu zao za "Tutoke vipi" hapa ni Uchaguzi, wameona kwamba ili wajisafishe kwa makosa yao waliyoyatenda ni bora warudie uchaguzi ili Maalim Seif atangazwe rasmi, lengo hapa ni kutaka kujitakasa mbele ya wananchi na macho ya jumuia ya kimataifa. ( hii ni dhana tu, ambayo si rahisi sana kutokea ila ngoja tuone baada ya kesho).
 
Hata sitaki kutabiri zanzibar baada ya kwesho. Namwachia Mungu. Maana hata ccm hawaelewi hatma ya zanzibar mdio maana wanahaha kuhakikisha jesh na police wanakua wengi kitaa kama kuna sherehe ya police
 
Hamad Rashid nimemsikia jana BBC anasema bado siku kidogo,atakuwa Makamu wa Pili wa rais. Sasa huu utabiri kwamba CUF itashinda Hamad Rashid hajasikia bado.
 
Kwa.vile mwandishi wa DW ametekwa nyara,kwenda kung'olewa kucha bila shaka,hakuna maana kutoa maoni. Tusubiri tu kuona jambo gani litatokea kesho.

POLISI WALIO PELEKWA ZANZIBAR KWA AJILI YA KULINDA AMANI WAKATI WA UCHAGUZI, WAAITE WAKEE, WATOTO NA FAMILIA ZAO MAANA BAADA YA KESHO ITABIDI WAHAMIE HUKO, NA NI MWANZO TU WA UCHUMI WA ZANZIBAR KUPOROMOKA HASWA KWA KUKALIA POLITICA ISIYO NA MWISHA MAANA AMANI YA KWELI HAITAKUWEPO TENA HATA KAMA HAMNA VITA, ILA WASIWASI UTADUMU.
 
Kwa.vile mwandishi wa DW ametekwa nyara,kwenda kung'olewa kucha bila shaka,hakuna maana kutoa maoni. Tusubiri tu kuona jambo gani litatokea kesho.

Kumbe Msukule unaweza kuishi miaka zaid ya 17 tangu mwenyewe atangulie mbele ya haki!
 
Back
Top Bottom