Zanzibar: Askari wanne wa SMZ na maofisa 3 wa Idara ya Misitu mbaroni kwa mauaji ya Katibu wa ACT-Wazalendo tawi la Mwembemakumbu

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
873
1,000
ACT.JPG

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia askari wanne wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na maofisa watatu wa Idara ya misitu kwa tuhuma za mauaji ya Katibu wa ACT Wazalendo tawi la Mwembemakumbu, Said Salum Suleiman.


Video hii inamuonyesh SAID MMANGA SULEIMAN, Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, tawi la Mwembe Makumbi, aliyepigwa risasi na polisi na kufariki baada ya muda, kwa kosa lakukamatwa na mchanga katika maeneo ya Muembe Makumbi Mkoa wa Mjini Magharib

----
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia watu saba kwa tuhuma za mauaji ya Said Salum Suleiman (32) mkazi wa Mwembemakumbi mjini Unguja.

Wanaoshikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya Suleiman ambaye alikuwa katibu wa ACT-Wazalendo tawi la Mwembemakumbu ni askari wanne wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na maofisa watatu wa idara ya misitu.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 12, 2020 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Awadh Juma Haji amesema tukio hilo limetokea jana saa 8 mchana ikidaiwa kuwa alipigwa risasi na maofisa hao eneo la Mwembemakumbi.

Amesema askari hao wakiwa wameambatana na maofisa wa idara ya misitu walikuwa katika doria maalumu kuwabaini wanaojihusisha na uhalifu wa mazao ya misitu na uharibifu wa mazingira.

Amesema wakiwa wanatokea katikati ya mji wakiwa na gari lenye namba za usajili SMZ 451B aina ya Mitsubishi walimkuta Suleiman akiwa na mkokoteni uliopakiwa mchanga.

Amesema mkokoteni huo ulikuwa ukivutwa na punda na alikuwa akitokea eneo la bondeni kuingia barabarani lakini alipowaona alikimbia na kuacha mkokoteni huo.

Amebainisha kuwa askari hao walichukua mkokoteni huo kwa lengo la kuupeleka katika ofisi zao zilizopo Maruhubi lakini muda mfupi baadaye walivamiwa na kundi la vijana wakiwa na mapanga na silaha mbalimbali, akidai kuwa walitaka kuwazuia polisi na maofisa hao kutoondoka na gari walilokuwa wamepanda.

Amesema katika kile alichokiita mapambano watu hao walivunja kioo cha nyuma cha gari na kusababisha askari kufyatua risasi iliyompata Suleiman.

“Baada ya kutokea kwa tukio hilo maofisa hao waliondoka mara moja katika eneo hilo na kuwaachia wananchi wakitoa msaada kwa Suleiman ikiwa ni pamoja na kumpakia kwenye gari kwa lengo la kumpeleka hospitali,” amesema.

Chanzo: Mwananchi
 

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,275
2,000
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja linawashikilia askari wanne wa vikosi vya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na maofisa watatu wa Idara ya misitu kwa tuhuma za mauaji ya Katibu wa ACT Wazalendo tawi la Mwembemakumbu, Said Salum Suleiman.
Kwa nini unataja nafasi yake ya kisiasa ktk taarifa ya maafa kama haya! Je, mauaji yake ni ya kisiasa? Kama ni ya kisiasa, maafisa misitu wanahusikaje? Kama siyo ya kisiasa, inatosha kuandika jina lake tu maana naamini alikuwa anayo kazi nyingine ya kuendesha maisha yake.
 

THE LOST

JF-Expert Member
Jul 3, 2017
1,149
2,000
Ndo yaleyale ya mdogo wetu Akwilina, hatima ya sheria zetu IPO mikononi mwa Jiwe the godfather.
 

mugah di mathew

JF-Expert Member
Jul 28, 2018
3,717
2,000
NAshindwa kuelewa ni kwa nini unataja nad´fasi yake ya kisiasa ktk taarifa ya maafa kama haya! Je, mauaji yake ni ya kisiasa? Kama ni ya kisiasa, maafisa misitu wanáhusikaje? Kama siyo ya kisiasa, inatosha kuandika jina lake tu maana naamini alikuwa nayo kazi nyingine ya kuendesha maisha yake.
Hapana,ni vigumu kumtenga mwanasiasa na siasa hasa siku ya uchaguzi

Ikumbukwe aliuawa wiki ya uchaguzi
 

chabuso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
6,144
2,000
Habari njema,..

Vile vile wawajibishe na wale wotewalio uwa na kuwatesa raia wasiokuwa na hatia wakati wa Uchaguzi..

Nchi inaendeshwa na Sheria ndio inaoongoza Nchi
 

Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
5,275
2,000
Hapana,ni vigumu kumtenga mwanasiasa na siasa hasa siku ya uchaguzi

Ikumbukwe aliuawa wiki ya uchaguzi
Nami nasema hapana! Tumeifanya nafasi ya kisiasa kuwa jambo muhimu sana ktk nchi kiasi kwamba, sasa kila mpuuzi anataka kuwa mwanasiasa. Hata diwani akifumaniwa tunaona ni sahihi sana kumzomea kwa kutumia nafasi yake ya kisiasa. Tunakoelekea ni kama sasa maisha ni siasa tu!

Kila siku watu wanauwa wake zao lakini hatusikii wakitaja kazi zao za maisha, badala yake akiwa nafasi ya kisiasa ndo inatajwa. Huu ni udhaifu tunaoulea kwa lengo la kuamini chama cha siasa ndo kila kitu.
 

Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,093
2,000
Nami nasema hapana! Tumeifanya nafasi ya kisiasa kuwa jambo muhimu sana ktk nchi kiasi kwamba, sasa kila m,puuzi anataka kuwa mwanasiasa. Hata diwani akifumaniwa tunaona ni sahihi sana kumzomea kwa kutumia nafasi yake ya kisiasa. Tunakoelekea ni kama sasa maisha ni siasa tu!..
Kwahiyo yule aliyechomwa moto na wajukuu zake haikupaswa kusema Diwani wa CCM?Badala yake wangesema mtu mmoja achomwa moto na wajukuu zake?

Wakati huu ambapo kuna malalamiko kuwa wazanzibar 13 wameuwawa kwa kupigwa risasi toka tarehe 27,ni vigumu kutohusisha na siasa!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom