Zanzibar: Akutana na kipigo baada ya kuonekana akila mchana!

Nilichokiona kikifanyika ni ujinga wa hali ya juu na ukosefu wa akili pia...kufunga ni siri kati yako na mungu wako kukiri kile ulichomkosea mungu wako...

na si kila mtu ajue kuwa umefunga ..wenzetu wanaona kufunga ni kula , mbona hawawaambii ukweli wale wanaopiga picha futari zao na kutupia kwenye mitandao wakijikweza mapochopocho , hali ya kwamba kuna baadhi ya waislamu hata hiyo futari yenyewe wanaisikia kwenye bomba shauri ya umaskin wao ....

hiki ni kipindi cha upendo yawezekana huyu mtu anaumwa au matatizo tu ya kibinadamu hadi kula sehemu public, lakini je vipi kuhusu waislamu wanaofuturu maeneo ya wazi hasa kipindi cha jioni ..ndo tuseme wale ambao hatujafunga hatutamani wao kula njiani au na sisi tungewaambia wakale vyumbani ??

Halafu hapo ikifika siku ya sikukuu mungu wangu kinachifanyika ndo aibu tupu ..sasa unasema huyu kafunga nini sasa ikiwa sikukuu anaenda club, beach kufanya ushenzi , ulevi , ufuska na matendo ambayo hayaendani na misingi ya kiislamu..
 
Ni ujinga tuu.....
Huko ni kushinda njaa na Cyo kufunga
Waislam wengi wa Leo wanashinda njaa na cyo kufunga....
Huyo mungu anayelazimisha watu wasile ni mungu yupi?
Unaweza ukafunga kumbe moyoni kufunga kwako ni kwaajili ya kuogopa viboko
Kuwa mpole mkuu
 
Jamani hatuheshimu za wengine tutachochea vurugu za kidini..... Mnaukumbuka kesi ya dibagula?.... Kisheria imani yake ilikuwa inamruhusu Lakini alifungwa jela kwa kuandika kwamba Yesu si mungu... Pamoja na mahakama kuu baadaye ilimuiona hana hatia alikuwa ameshasota jela. Je waliomfunga hawakujua sheria? Huyu alikutana na yaliyomkuta kutokana na uchochezi wa kidini. Na huyu alokwenda kula hadharani (kosa sio kutofunga) mwezi Ramadhan Zanzibar nae pia ni Mchochezi. Hawa ni watu hatari na hawafai kuungwa mkono.
 
Back
Top Bottom