Zanzibar: Ajali yaua Watu watatu papo hapo na sita wamejeruhiwa KIBUTENI

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,484
54,854
Watu watatu wamefariki dunia papo hapo na wengine sita wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea Kibuteni Wilaya ya Kusini.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema ajali hiyo iliyohusisha gari aina ya Noha iliyokuwa ikitokea mjini kwenda makunduchi harusini iliacha njia na kupinduka katika kilima cha kibuteni.

Kamanda Suleiman amewataja waliofariki dunia ni Suleiman Abdalla Ussi(23),Francis Andrea(20),na Bi Kibena Antony Paulo (25) wote waakazi wa Ndagaa wilaya ya Kati.
.
Amesema majeruhi watano akiwemo dereva wa gari hiyo Abdalla Ali Choum wameelezwa katika hospital ya Mnazi Mmoja na Mmoja anaendelea na matibabu katika hospital ya makunduchi.

Credit: Rauhiya Mussa Shaaban
 
Noah mpaka sasa zimeshaua watu wengi kuliko Vita ya Kagera. May these innocent souls rest in peace.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom