Zanzibar: Aingia matatani baada ya kukutwa kapika mchana kwenye baa yake

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,241
2,000
Mfanyabiashara aliyejulikana kwa jina la Kasian ameingia matatani baada ya chakula kunaswa kwenye baa yake muda wa mchana na anatarajiwa kupandishwa mahakamani
Zanzibar serikali imekataza kwa mfanyabiashara yoyote kuuza chakula wakati wa mchana kwa vyovyote vile na usiku inaruhusiwa kwa waliopewa vibali tu
Mfanyabiashara huyo amedai chakula hicho kilikuwa kwa ajili ya mafundi kwenye baa yake na sio kwa ajili ya biashara

The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
15,471
2,000
Nafikiri pombe inapingwa na mafundisho ya dini nyingi ikiwemo uislam, licha ya kuwa mwezi mtukufu, muislam anatafuta nini baa? Hasa huu mwezi mtukufu, huko kunajulikana kabisa kwa waovu kwanini wasiachwe wale? Muislam ataenda kutafuta nini huko hadi ashawishike kula wakati hatakiwi kabisa kuwa hayo maeneo?

Hii inanikumbusha zamani kuna jamaa alikamatwa anauza kitimoto kwenye kilabu cha pombe kijijini, alipopelekwa mahakamani akasema mie najua pombe wanakunywa wapagani, na hawakatazwi kula mnyama, nimeleta huku kwa sababu waumini wasiokula nguruwe hawaji kilabuni kunywa pombe, alipewa onyo na kuachiliwa bila kesi.
 
makumbire

New Member
Jun 15, 2017
4
45
Mfungo Wa kuvutiwa NA chakula au kuudhika wakati wengine wanapika ni Wa kimwili sio Wa MUNGU.KILA MTU ANA IMANI YAKE KWA NINI UZUIE MTU KUPIKA WAKATI SI IMANI YAKO ETI NI RAMADHANI ,KWANI HI NI NCHI YA WAISLAMU? BIG NOOO TO THIS NA HII TABIA INAENDELEA SANA SIKU HIZI SERUKALI INATAKIWA KULIZUIA.MBONA WAKRISTO WAKIFUNGA HATUWASUMBUI WAO TUNAISHI NAO HATA KAMA WANAPIKA.NA WAKRISTO NCHI NI WENGI KULIKO WAO.NDUGU NZANGU WAISLAMU TUFIKE MAHALI TUHESHIMU IMANI ZA KILA MTU.NA NDUGU ZANGU WAKRISTO TUESHIMU IMANI ZA WENGINE KWA UNYENYEKEVU.TANZANIA NI NCHI YA AMANI ISIYO NA DINI, WANANCHI WAKE NDO WANA DINI.TUENDELEZE AMANI ILIYOPO.MUNGU AWABARIKI WOTE
 
mojave

JF-Expert Member
Apr 30, 2016
5,543
2,000
Nafikiri pombe inapingwa na mafundisho ya dini nyingi ikiwemo uislam, licha ya kuwa mwezi mtukufu, muislam anatafuta nini baa? Hasa huu mwezi mtukufu, huko kunajulikana kabisa kwa waovu kwanini wasiachwe wale? Muislam ataenda kutafuta nini huko hadi ashawishike kula wakati hatakiwi kabisa kuwa hayo maeneo?

Hii inanikumbusha zamani kuna jamaa alikamatwa anauza kitimoto kwenye kilabu cha pombe kijijini, alipopelekwa mahakamani akasema mie najua pombe wanakunywa wapagani, na hawakatazwi kula mnyama, nimeleta huku kwa sababu waumini wasiokula nguruwe hawaji kilabuni kunywa pombe, alipewa onyo na kuachiliwa bila kesi.
Hawa wanapenda kulazimishana kufunga sijui shida yao nini.

Usikute wanaozini hawawafatilii kama wanavyofatilia chakula.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom