Zanzibar: Ahukumiwa kwenda kutumikia kwenye Chuo cha Mafunzo (Gerezani) kwa kubaka msichana wa miaka 17

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,491
9,261
Hatimae Mahakama ya Mkoa Wete imemuhukumu kwenda kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka kumi (10) pamoja na kulipa fidia ya shilingi laki mbili mshitakiwa Khalifa Khalfan Mwaveso mwenye umri wa miaka 25 mkaazi wa Micheweni Pemba, aliepatikana na kosa la kumbaka msichana mwenye umri wa miaka 17.

Baada ya mahakama kufanya uchambuzi wa Sheria juu ya ushahidi uliwasilishwa na upande wa mashitaka, mahakama imeweza kuthibitisha kosa pasi na chembe ya shaka ya maana.

Ndipo hakimu wa mahakama hiyo Abdalla Yahya Shamhun alipotoa hukumu hiyo chini ya kifungu cha 210 cha Sheria nambari 7 ya mwaka 2018, baada ya kumkuta na hatia mshitakiwa huyo

Hakimu Shamhuni alimuamuru mshitakiwa huyo kwenda kutumikia chuo cha mafunzo kwa muda wa miaka kumi (10) pamoja na kulipa fidia ya shilingi laki mbili ndani ya siku 14

Kabla ya hukumu hiyo, mwendesha mashitaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa mashitaka Pemba, Juma Mussa Omar alidai kuwa, hawana kumbu kumbu za awali kwa mshitakiwa huyo, ingawa aliiomba mahakama kutoa adhabu kali, ili iwe fundisho kwa wengine.

“Muheshimiwa hakimu kutokana na kosa hili mtuhumiwa apewe adhabu kali na kumlipa fidia muathiriwa chini ya kigungu cha 109 (1) cha Sheria nambari ya mwaka 2018, Sheria ya Zanzibar, ili iwe funzo kwa wengine wenye tabia kama hiyo”, alidai mwendesha mashitaka huyo.

Kwa upande wake mshitakiwa huyo aliiomba mahakama impunguzie adhabu angalau, impatie adhabu ya kwenda kuitumikia jamii.

Awali ilidaiwa mahakamani hapo kuwa, mtuhumiwa huyo alitenda kosa siku na tarehe isiyojukana mwezi Octoba mwaka 2019 saa 3:00 usiku huko Pandani Masipa Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba. Ilidaiwa kuwa, bila ya halali alimbaka msichana mwenye umri wa miaka 17, jambo ambalo ni kosa kisheria.

Kufanya hivyo ni kosa kinyume na kifungu cha 108 (1) (2) (e) na kifungu cha 109 (1) vya Sheria namba 6 ya mwaka 2018 Sheria ya Zanzibar.
Kesi hiyo yenye namba RM 04/2020 kwa mara ya kwanza ilianza kusikilizwa katika Mahakama ya Mkoa Wete Januari 1 mwaka huu.
 
Mbona hakimu hajatafsiri kama binti alikuwa bikira au mzoefu! Kama alivyofanya kwa yule mwingine juzi
Kweli Dunia watu.. hapa zaidi nikua kuumiza watoto kiafya na kiakili,.
Lazima wadhibitiwe hawa waaribifu.
Achana na habari za "bikira Maria"
 
JELA MIAKA 30 KWA UBAKAJI: Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kijana aliyefahamika kwa jina la Halawa Tabu mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti mwenye umri wa miaka 19.

Kijana huyo anadaiwa kuwa alijifanya ni mganga wa tiba za jadi na kumbaka binti huyo wakati akimfanyia tiba ya dawa ya kumuosha mwili kwa kutumia maji yanayodaiwa kuondoa mikosi mwilini.

Awali katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora, Wakili wa Jamhuri, Miraji Kajiru aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo la ubakaji mwezi Julai mwaka huu Kinyume na Kifungu cha 130 kidogo cha kwanza na cha pili (a) na kifungu cha 131 kidogo cha kwanza sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Mshtakiwa Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Julai 19 aliitwa nyumbani kwa binti aliyembaka na baba mzazi wa binti huyo kwa lengo la kuzindika nyumba yao ndipo ilipofika usiku kijana huyo Tabu akaomba amchukue binti huyo ambaye jina linahifadhi kwenda naye porini ili akamuoshe dawa za kuondoa mikosi mwilini na akafanikiwa kufanya tukio hilo alilokusudia.

Shauri hilo la ubakaji namba 66 la mwaka 2020 upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi saba huku upande wa mshtakiwa Halawa Tabu alikuwa akijisimamia mwenyewe.

Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora Jocktan Rushwela baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili alijiridhisha pasipo shaka yoyote ndipo akamuhukumu adhabu yenye ukomo kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.

#kesi #hukumu #ubakaji #Tabora #mganga
 
Zanzibar bwana..
Yani sheria zao ziko laini laini sana.
Waletwe huku Bara wakione chamtema kuni.
Na huyo kimemuangusha ubini wake tu anaonekana katokea bara angekuwa wale wale wapemba bint angetetea nampenda bwana'angu msimfunge kesi ingefutwa familia zingerudi nyumbani kufanya harusi maisha yaendelee.
 
JELA MIAKA 30 KWA UBAKAJI: Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kijana aliyefahamika kwa jina la Halawa Tabu mwenye umri wa miaka 25 mkazi wa Wilaya ya Uyui mkoani Tabora baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka binti mwenye umri wa miaka 19.

Kijana huyo anadaiwa kuwa alijifanya ni mganga wa tiba za jadi na kumbaka binti huyo wakati akimfanyia tiba ya dawa ya kumuosha mwili kwa kutumia maji yanayodaiwa kuondoa mikosi mwilini.

Awali katika Mahakama ya Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora, Wakili wa Jamhuri, Miraji Kajiru aliiambia mahakama kuwa mshtakiwa huyo alitenda kosa hilo la ubakaji mwezi Julai mwaka huu Kinyume na Kifungu cha 130 kidogo cha kwanza na cha pili (a) na kifungu cha 131 kidogo cha kwanza sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2019.

Mshtakiwa Ilidaiwa mahakamani hapo kuwa Julai 19 aliitwa nyumbani kwa binti aliyembaka na baba mzazi wa binti huyo kwa lengo la kuzindika nyumba yao ndipo ilipofika usiku kijana huyo Tabu akaomba amchukue binti huyo ambaye jina linahifadhi kwenda naye porini ili akamuoshe dawa za kuondoa mikosi mwilini na akafanikiwa kufanya tukio hilo alilokusudia.

Shauri hilo la ubakaji namba 66 la mwaka 2020 upande wa mashtaka ulikuwa na mashahidi saba huku upande wa mshtakiwa Halawa Tabu alikuwa akijisimamia mwenyewe.

Hakimu mkazi Mkoa wa Tabora Jocktan Rushwela baada ya kupitia ushahidi wa pande zote mbili alijiridhisha pasipo shaka yoyote ndipo akamuhukumu adhabu yenye ukomo kutumikia kifungo cha miaka 30 jela.

#kesi #hukumu #ubakaji #Tabora #mganga
,kwahio hayo maji ya kumuoshea mikosi yapo ndani ya mwili wa mganga?
 
Mbona hakimu hajatafsiri kama binti alikuwa bikira au mzoefu! Kama alivyofanya kwa yule mwingine juzi
Nina wasiwasi na hizo Sheria ambazo yaelekea zina macho. Sheria ambazo huchagua nani apewe adhabu ipi, Nani afungwe na nani aachiwe kwa kosa la aina hiyohiyo moja.
 
Back
Top Bottom