Zanziba haiwezi kuwa sawa TZ Bara-Pinda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zanziba haiwezi kuwa sawa TZ Bara-Pinda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by in and out, Jul 15, 2011.

 1. i

  in and out Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 69
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  akijibu swali la papo kwa papo siku ya alhamisi bungeni waziri mkuu mizengo kayanza pinda alisema znb ni nchi ina watu milioni 1 na tanzania bara ina watu zaidi ya milioni 42 kwa hiyo hata siku moja znb na tz bara hazitakuwa sawa ila pale ambapo yanapotokea matatizo tunakaa tunayazungumza kwa faida ya muungano wetu.
   
 2. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Pinda Acha dharau mheshimiwa,

  Zanzibar mliikuta nchi hatakama ilikuwa na watu 100,000 wanatakiwa kuheshimiwa kama nchi. Suala la population is irrelevant na hoja isiyo na msingi. Kauli kama hizi zinaudhi na kuvunja moyo mwishoe kuishia kuvunja muungano. Unasema unataka mazungumzo ila kwa kauli yako ni wazo mazungumzo hayo ni yale yanayokidhi mahitaji yako na hapo kwa ufupi hakuna mazungumzo. Wazanzibar ombeni mjadala wa muungano au ikishindikana vunjeni muungano muishie zenu this is too much bana!!!
   
 3. meddie

  meddie JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 413
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  sasa hapa hoja mbadala ni ipo zaidi kuwa ni maneno ya jasba tu!! yeye kasema jambo moja tu la population kwa maana kwamba huwezi kuwa na ratio ya 1:1. Ushaelewa yahke!!
   
 4. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Chafua hali ya hewa babaaaaa..........
   
 5. fikramakini

  fikramakini JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 27, 2010
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kwani swali hasa lilikua nini? Maana kwa jibu hilo mbona kweli? Hata ukubwa wa ardhi si TZ bara ndo kubwa? Pato kubwa zaidi si linatoka pia bara?

  Kutokana na swali aloulizwa ndo anaweza kua amekosea au la. Swali sijalijua bado ...
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Igaweni Zanzibar mara 2 iwe ni nyongeza ya mikoa tuue muungano tuachane na kelele za wavivu wale .
   
 7. mulambakao

  mulambakao Member

  #7
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata South Sudani imekuwa nchi juzi juzi tu, siyo nchi hiyo Unguja bana, au basi unge dedembua kwamba ni nchi inayo TAWALIWA majibu mnayo, marais tunawawekeeni sisi, muafaka unatoka kwetu nyiye mna nini? the PM was right even if magamba hayamtoshi!
   
 8. mulambakao

  mulambakao Member

  #8
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 13, 2011
  Messages: 28
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe ni kifaa Lunyungu, teh teh, wavivu wale kama kawaida tuwapeleke Sumbawanga wafundishwe kulima wavivu mpaka wamedidimia, let them go bwana they're of no match to us!
   
 9. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Pinda kaijbu vyema sana-zanzibar kamwe haiwezi kuwa kama tanganyika-kama hili litawauma-ni bora mjitoe kwenye muungano mapema-ninachoipendea tanganyika ni kwamba imeamaua kutawala zanzibar kwenye kila kitu-kwa hio na sisi watanganyika ni master wa wanzibar-ndo maana hata wakitaka maisha mazuri-eti inabid waje tanganyika-maana ndo kuna kila kitu-NGOJA NIANDAE BENDERA YANGU YA TANGANYIKA-SIKU YA SHEREHE ZA MIAKA HAMSINI NIIPEPERUSHE KWA NGUVU ZOTE
   
 10. T

  Tata JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2011
  Joined: Dec 3, 2009
  Messages: 4,740
  Likes Received: 658
  Trophy Points: 280
  Haya ni majibu ya kujipa moyo tu ya watanganyika. Mimi kwa mtazamo wangu wazanzibari wako juu zaidi kwenye huu muungano kuliko watanganyika na hizi kelele zao ni strategy ya kuendelea kufaidi kwani kila siku Tanganyika inaongeza upendeleo kwa wazanzibari. Yafuatayo kwa uchache ni mambo ninayotumia kujenga hoja yangu:-
  • Uwiano wa watu waliomaliza elimu ya msingi na sekondari na idadi ya watu wote nchini.
  • Uwiano wa watu wanaojua kusoma na kuandika
  • Uwiano wa viongozi wa kisiasa na kiserikali kwa idadi ya wananchi wote.
  • Uwiano wa barabara nzuri za lami kwa barabara zote za nchi
  • Uwiano wa watu wanaopata huduma za umeme na maji safi na salama
  • Hakuna mtanganyika anayeshika wadhifa wa waziri au naibu waziri kwenye serikali ya zanzibar wakati wazanzibari wanashika nyadhifa mbalimbali serikali ya Muungani ambayo ndiyo serikali ya Tanganyika.
  • Watu milioni moja wameshawahi kutoa rais wa kutawala watu milioni 40 wa Tanganyika na kuna uwezekano wa kutoa tena.
  • Hawana malaria ambayo bado inaua mamilioni ya watu Tanganyika
  • Wana bunge na serikaliambavyo vinasimamia maslahi yao ndani ya muungano kwa nguvu zote wakati Tanganyika haina serikali ambayo inasimamia maslahi yake pekee bila kushirikisha wazanzibari.
  • Wabunge wa Zanzibar wanashiriki kwenye kamati zinazosimamia mashirika ya umma wa watanganyika ambayo hata zanzibar hayapo.
  Kwa ufupi wazanzibari wako juu zaidi ya watanganyika kwenye huu muungano na wanazidi kwenda juu kadiri wanavyopiga hizo tunazoita kelele. Hizo siyo kelele bali ni maslahi yao ambayo wao wana mechanism ya kuyalinda na kuyasimamia. Watanganyika wamepiga usingizi tu na hivi kuna mgao wa umeme ndiyo hawaamki kabisaaa.
   
 11. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  nafikiri zaidi waziri mkuu alitakiwa kwenda mbali zaidi kwa kusema Zanzibar ni nchi huru na Doula iliyotimia na Tanganyika si nchi.
  Zanzibar ina Serikali, baraza la wawakilishi (Bunge),mahakama, bendera, rais lakini Tanganyika hakuna kitu.
  Kijumla zanzibar ni Utaifa wakati tanganyika hakuna utaifa. Lakini wote ni WaTanzania.

  Hivyo Zanzibar kwa vigezo hivyo haiwezi kufanana na Bara
   
 12. J

  JokaKuu Platinum Member

  #12
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,811
  Likes Received: 5,119
  Trophy Points: 280
  ..Pinda ame-validate point yake kwa kukumbusha kwamba Tanganyika kuna watu milioni[ 40+], na Zanzibar kuna watu milioni[ 1 +] .

  ..off course ukitulinganisha kwa idadi ya watu na eneo la ardhi, Tanganyika na Zanzibar siyo sawa hata kidogo.

  ..nakubaliana na Tata kwamba kinachoitwa " kero za muungano " ni mkakati wa Zanzibar kuinyonya Tanganyika. wamefikia mpaka kudai kwamba misaada toka nje igawanywe sawasawa baina ya Tanganyika na Zanzibar. hivi inaingia akilini kweli?

  ..halafu pamoja na miaka yote hii ya manun'guniko na vitimbi bado Zanzibar hawajitoi ktk muungano. hii inadhihirisha kwamba Zanzibar inafaidika na muungano, na wanataka kunyonya zaidi na zaidi.
   
 13. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Tumuulize Pinda, kwani tunashindana?

  Wanachotaka Wazanzibari ni Utaifa wao uliopotea kwa kuimeza Zanzibar na kudidimia kwa kila hali.

  Haya mambo ambayo mnadai kuwa Tanganyika inaifanyia Zanzibar kwani ni ya lazima au ni rushwa tu ya "kuulinda" huu "muungano" na kubakisha moja ya legacy ya fitna za Nyerere.

  Si ingekuwa vyema kuiwacha Zanzibar kama mnaona ni mzigo?

  Tena kwanini muulinde kwa majeshi ya kivamizi?

  Mnalo jambo lenu, hamjalisema tu.
   
 14. MWAGONA

  MWAGONA Member

  #14
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 14, 2011
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa kifupi mtoto wa wakulima feki hapo amekosea nimetanguliza mtoto feki kutokana na kauli yake aliyo wai kutoa bungeni kuwa posho za wabunge ni fedha kidogo saana wakati watoto wa wakulima haswa kuingiza kwa mwezi ni hiyo elfu 70 ni shughuli.Nikianza kwa hoja hapo juu ivi huyu mh hajui kuwa zanzibar ilikuwa nchi huru kabla ya muungano na kwa oja yake ya watu haina uzito wape wazanzibari haki yao mbona tukija kwa hoja ya ukubwa Burundi Ruanda ni sawa tu na mikoa baadhi ndani ya Tanganyika. kitu muhimu ili kudumisha na kumuenzi mwalimu Nyerere tutangaze serikali ya tanganyika tuwe na bendera yetu na kila kitu na Tanzania ibaki kama FEDERATION nazani hiyo ndiyo hoja muhimu kwani tukirudi nyuma wazanzibari wakikataa muungano kwa kuwa hata mkataba wenyewe haupo ambao walisain wazanzibari na watanganyika basi nchi ya zanzibari itakuwa nchi kama nchi. kwa maoni yangu pinda angesema kuwa katiba mpya ndiyo itakuwa suluisho ya yote hayaa inatosha.
   
 15. m

  matambo JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  leo anaiita zanzibar nchi, si alikataa huyu akisema zanzibar si nchi?
   
 16. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #16
  Jul 15, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,075
  Likes Received: 7,566
  Trophy Points: 280
  Hata mtaani kwetu kuna serikali ya mtaaa yenye mamlaka kamili kama ya Zanzibar..
   
 17. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Alichosema pinda ndo ukweli wenyewe.tatizo ni nani kasema...
   
 18. s

  sem2708 JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 3,094
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kauli za pinda sio za kisiasa ndo maana zinamletea matatizo sana mwisho anaishia kulia hadharani...watu wamezoea majibu ya kisiasa sasa yeye anaongea uhalisia zaidi.He is too honesty.Jifunze kupindisha vingnevyo utalia kila siku.lol!
   
 19. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,388
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  siwezi kuwa mnafiki siupendi muungano wa namna hii!
  binafsi naona ndio chanzo cha maisha yangu mabaya
  hebu fikiria working pemit fee kiasi gani tungepata kwa maduka tu ya wapemba!
  sisi tunapata nini kwao zaidi ya kupunguza nafasi zetu za ajira na maslahi ya taifa!
  naogopa tusije sikumoja tukawashitaki viongozi wetu kwa kutumia rasrimali zetu kunufaisha taifa lingine!
  mimi hasirani kwa muungano huu wa serikali mbili siutaki! lakini kama serikali moja au tatu nipo tayari lakini kwa hili ni sawa na kuvua samaki kwenye swiming pool.
   
 20. Makaimati

  Makaimati JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 4, 2011
  Messages: 462
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  Mkuu Musembi, Zanzibar ni Nchi kama alivyokiri Pinda na kuthibitisha kauli yake, hii ndio KATIBA ya Zanzibar:

  Katiba ya Zanzibar ya 1984 inasema;

  (9)(i) Zanzibar itakuwa ni NCHI ya kidemokrasia na haki za kijamii.

  (9)(2)(a) Mamlaka ya kuendesha NCHI ni ya wananchi wenyewe …

  (10) Kwa madhumuni ya kuendeleza umoja na maendeleo ya watu na ustawi wa jamii katika NCHI itakuwa ni wajibu wa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar:

  (10)(3) Itadhibiti uchumi wa NCHI kufuatana na misingi na madhumuni yaliyoelezwa na katiba hii.

  (12)(3) Haki za raia, wajibu na maslahi ya kila mtu yatalindwa na kuamuliwa na mahkama pamoja na vyombo vya NCHI na vinginevyo vilivyowekwa na sheria.

  (21)(i) Kila Mzanzibari anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa NCHI…

  (23)(2) Kila mtu ana wajibu wa kulinda maliasili ya Zanzibar, mali ya NCHI pamoja na mali yote inayomilikiwa kwa pamoja na wananchi

  Tuletee humu katiba ya serikali ya mtaa wowte huko kwenu ili tufaidike. Zanzibar ni Nchi kamili ndani ya "muungano" huu feki.


   
Loading...