Zantel arusha watia aibu kulangua moderm za internet

Gerad2008

JF-Expert Member
Jun 9, 2009
583
287
Wafanyakazi wa Zantel hapa Arusha wameanza biashara chafu ya kulangua moderm za internet kwa kuwatumia wafanyabiashara binafsi akiwemo mmiliki wa duka la SOUND and VISION au maarufu kama kwa Benson. Nilifika ofisi za Zantel kuuliza kama wana moderm za internet na kuniambia zimeisha ila ninaweza kuzipata katika duka la Benson kwa shilingi 75000/- badala ya shilingi 49000/- zinazouzwa na zantel kwa bei ya promosheni. Bila aibu akina dada waliokuwepo katika ofisi ya Zantel waliniambia kwa msisitizo tena kwamba zinapatikana kwa Benson na kwamba ofisini kwao hazitapatikana labda baada ya wiki mbili. hali hii kwa mtu mwelewa inaashiria bila wasiwasi kuwa kuna jinsi wafanyakazi wa Zantel wanachukuwa moderm za promosheni na kuzipeleka kwa Benson kwa makubaliano ya kujinufaisha binafsi badala ya kuwarahisishia wateja huduma. Jambo jili lifuatiliwe kwani kwetu sisi wateja hii haingii akilini eti mtu binafsi ana moderm ila dealers hawana. Hii inavuruga biashara na kuharibu sifa nzuri ya uaminifu ambayo ZANTEL imejijengea. wafanyakazi waroho na wenye tamaa ya kujinufaisha binafsi waondolewa la sivyo watairudisha nyuma zantel ambayo kwa hapa Arusha ndo ilikuwa inaanza ku stabilize
 
Piga simu makao makuu uwaelezee ilo tatizo. Au tembelea wavuti yao utaweza pata email za mabosi,then watumie na kuwataarifu habari iyo. Nina uhakika top guns hawafahamu kinachoendelea.
 
Nitajitahidi kuwatafuta mkuu kwani naona hapa Arusha hawa wafanyakazi wa zantel Hawathamini juhudi zilizofanywa na hii kampuni kuipromoti mpaka ilipofikia. kwa mtaji huu Zantel itapoteza imani kwa wateja
 
Kwani mnaishi nchi gani? Mbona hii ni kawaida kwao! Hata wakati zimeshushwa bei kutoka 99,900/- hadi 49,900/-walikuwa wakitembea mitaani kama hukujua bei imeshuka unapigwa bei ya zamani!Ndo tumefika huko kila sector ni udalali tu na kupenda cha juu kisichostahiki.
 
Hivi ofisi hiyo ina Meneja na sales team? Kama wapo hawajui kazi yao, na wanaidhalilisha kampuni. kwann wadada hao wakwambie straight kwmb uende kwa benson, maana yake n kwmb wamezipeleka huko.
Wapumbavu sana hawa!
 
kwanza wangejua moderm zenyewe za zantel ni vimeo, maana hazichakachuliki kama za voda na airtel ambazo huchakachuliwa na kuweza kutumia ktk mtandao wowote, watawauzia haohao wasiozijua.
 
Kwa hiyo unahitaji zinazochakachulika?
 
Vile vidada nyodo sana.kuna siku nlitaka kusajili line vikaniambia nikatafute mawakala huko mjini.hawana heshima kwa wateja kabisa.
 
Wafanyakazi wa Zantel hapa Arusha wameanza biashara chafu ya kulangua moderm za internet kwa kuwatumia wafanyabiashara binafsi akiwemo mmiliki wa duka la SOUND and VISION au maarufu kama kwa Benson. Nilifika ofisi za Zantel kuuliza kama wana moderm za internet na kuniambia zimeisha ila ninaweza kuzipata katika duka la Benson kwa shilingi 75000/- badala ya shilingi 49000/- zinazouzwa na zantel kwa bei ya promosheni. Bila aibu akina dada waliokuwepo katika ofisi ya Zantel waliniambia kwa msisitizo tena kwamba zinapatikana kwa Benson na kwamba ofisini kwao hazitapatikana labda baada ya wiki mbili. hali hii kwa mtu mwelewa inaashiria bila wasiwasi kuwa kuna jinsi wafanyakazi wa Zantel wanachukuwa moderm za promosheni na kuzipeleka kwa Benson kwa makubaliano ya kujinufaisha binafsi badala ya kuwarahisishia wateja huduma. Jambo jili lifuatiliwe kwani kwetu sisi wateja hii haingii akilini eti mtu binafsi ana moderm ila dealers hawana. Hii inavuruga biashara na kuharibu sifa nzuri ya uaminifu ambayo ZANTEL imejijengea. wafanyakazi waroho na wenye tamaa ya kujinufaisha binafsi waondolewa la sivyo watairudisha nyuma zantel ambayo kwa hapa Arusha ndo ilikuwa inaanza ku stabilize
Je ulijaribu kumuona meneja?au wote lao moja
 
Kwa hiyo unahitaji zinazochakachulika?

I dont agree with you guys, those guys are good and they give the best customer service, nimeenda hata mimi kununua modem pale na zilikuwa zimeisha they direct m to benson i bought the modem kwa hiyo 75 nikarudi office wakaniwekea highlife and wakawa wanajiuliza kwa nini apandishe bei , ladies ur gud keep up.
 
NAHISI ELIMU KWAO INAWEZA KUWA SHIDA,NDIO MAANA WAKIKALIA HUVYO VITI VYA KUZUNGUKA WANAONA NDIO WAMEFIKA.

Hakuna kitu kina kera kama,Hawa Dada zetu wanao fanya kwenye kampuni za simu,nikawa na wasiwasi kuhusu Elimu yao.
 
Back
Top Bottom