Gerad2008
JF-Expert Member
- Jun 9, 2009
- 583
- 287
Wafanyakazi wa Zantel hapa Arusha wameanza biashara chafu ya kulangua moderm za internet kwa kuwatumia wafanyabiashara binafsi akiwemo mmiliki wa duka la SOUND and VISION au maarufu kama kwa Benson. Nilifika ofisi za Zantel kuuliza kama wana moderm za internet na kuniambia zimeisha ila ninaweza kuzipata katika duka la Benson kwa shilingi 75000/- badala ya shilingi 49000/- zinazouzwa na zantel kwa bei ya promosheni. Bila aibu akina dada waliokuwepo katika ofisi ya Zantel waliniambia kwa msisitizo tena kwamba zinapatikana kwa Benson na kwamba ofisini kwao hazitapatikana labda baada ya wiki mbili. hali hii kwa mtu mwelewa inaashiria bila wasiwasi kuwa kuna jinsi wafanyakazi wa Zantel wanachukuwa moderm za promosheni na kuzipeleka kwa Benson kwa makubaliano ya kujinufaisha binafsi badala ya kuwarahisishia wateja huduma. Jambo jili lifuatiliwe kwani kwetu sisi wateja hii haingii akilini eti mtu binafsi ana moderm ila dealers hawana. Hii inavuruga biashara na kuharibu sifa nzuri ya uaminifu ambayo ZANTEL imejijengea. wafanyakazi waroho na wenye tamaa ya kujinufaisha binafsi waondolewa la sivyo watairudisha nyuma zantel ambayo kwa hapa Arusha ndo ilikuwa inaanza ku stabilize