Zamu ya Zanzibar Urais 2015?

I see the series in a different way: NYERERE, mwinyi, MKAPA, KiKwEtE.
Aliyeharibu ni KiKwEtE. Hapo ilikuwa nafasi ya Zanzibar. Na siajabu akaharibu tena 2015 kwa kumuweka mzanzibar. Swala la wakristu kukubali sijui watatumia njia gani maana wadanganyika wengi udini kwao sio issue na ukizingatia tume yenyewe ndo hii ya Kiravua na Ukame, hatari kwelikweli. Na spika mwenyewe ndo Makinda ya ndege, hata kanuni wasiwasi.

Mie nakubaliana na Rutashubanyuma with one caution, NGUVU YA UMMA ipunguzwe makali. Kwa upande wa pili nasema "Adui muombee njaa". Wakigawanyika ndo furaha yetu wapigania uhuru wa Tanganyika, sababu huko Zenj, wenzetu wameshapata Uhuru japo ni nusunusu
 
I see the series in a different way: NYERERE, mwinyi, MKAPA, KiKwEtE.
Aliyeharibu ni KiKwEtE. Hapo ilikuwa nafasi ya Zanzibar. Na siajabu akaharibu tena 2015 kwa kumuweka mzanzibar. Swala la wakristu kukubali sijui watatumia njia gani maana wadanganyika wengi udini kwao sio issue na ukizingatia tume yenyewe ndo hii ya Kiravua na Ukame, hatari kwelikweli. Na spika mwenyewe ndo Makinda ya ndege, hata kanuni wasiwasi.

Mie nakubaliana na Rutashubanyuma with one caution, NGUVU YA UMMA ipunguzwe makali. Kwa upande wa pili nasema "Adui muombee njaa". Wakigawanyika ndo furaha yetu wapigania uhuru wa Tanganyika, sababu huko Zenj, wenzetu wameshapata Uhuru japo ni nusunusu

Nzitunga umelonga hapo...........................Tupo wote.............................
 
Kwani Zanzibar kuna mkristo, Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete ...................nafikiri nimeeleweka.

Sasa ukichanganya sequence hii na mambo ya zanzibar na ubara naona kama watakuwa katika wakati mgumu sana.Halafu mkumbuke bila CC kusimamisha majina ya wazanzibar peke yao si rahisi kupita kwani wapiga kura wengi wako bara.Na kwa vile ZNZ ni sehemu ya zanzibar kwa nin tusiachane na mambo hayo tukaangalia zaidi ubora wa sifa za kiongozi(Ya dini au anakotoka tuyaache) Tanzania ni nchi moja,tukiendekeza haya mambo ya zamu zamu yatatutokea puani huko mbele na hatutakuwa salama.
 
Sasa ukichanganya sequence hii na mambo ya zanzibar na ubara naona kama watakuwa katika wakati mgumu sana.Halafu mkumbuke bila CC kusimamisha majina ya wazanzibar peke yao si rahisi kupita kwani wapiga kura wengi wako bara.Na kwa vile ZNZ ni sehemu ya zanzibar kwa nin tusiachane na mambo hayo tukaangalia zaidi ubora wa sifa za kiongozi(Ya dini au anakotoka tuyaache) Tanzania ni nchi moja,tukiendekeza haya mambo ya zamu zamu yatatutokea puani huko mbele na hatutakuwa salama.

Ninaafiki mtazamo huu hasa kwenye eneo nililoliwekea rangi nyekundu...........
 
Hahahahahahahaaaaa Land of great thinkers...tell me again.... is that true? Mi sijui, but hope u've got jawabu ijapokuwa litakuwa shubiri?Hivi nailiza hiv Tz kuna dini mbili tu?Vp wahindu? vp wale wanaamini dini za jadi? vp wale wasio na dini? kwa kutokana na maelezo yenu nilivyoyafuatilia wao pia wana haki?kwa sababu ni watanzania na wana haki sawa na wewe!na kitu chengine kutokana na maelezo ya wengi sana inaonyesha kama mgombea wa ccm 2015 ndiyo raisi na ninavyojua mimi wengi waliochangia ni hawaipendi CCM.. kwa hivyo inaoneka mnajua kama CCM itashinda mwaka huo?mbona mapema mno kuja na conclusion hiyo! tuchukulie Chadema au chama chengine kitashinda sasa zongo jingi sana na mgombea wa CCM 2015 yeyote atakaekuwa hatokuwa rais kwani mwaka huo chadema ndiyo mshindi na hope mtamueka mkiristo?nashaa sana... hebu tuje upande mwengine hivi chadema mgombea wake ameshawahi kuwa muislam kwa nini hamjafikiria kama 2015 ni lazima apewe muislamu kugombea kwa nafasi ya chadema au mgombea wa CCM asiwe muislamu mwaka huu... mtaniambia pengine hiyo ni sera ya CCM lakini kutokana na mnavyoiongelea yinyi ni sawa na sera ya jamuhuri ya muungano wa TZ ya kupokezana baina mkiristo na muislamu? na chadema iko ndani ya jamuhuri hii? hivvi kwa mfano ikatokea Zitto ndiyo mgombea wa uraisi wa Chadema mwaka 2015 na CCM wamemueka mzanzibar(muislamu) na CUF wakasimamisha mkiristo je mnataka kuniambia mwenye kuwa na haki ya kuwa raisi ni mgombea wa CUF kwa sababu ni mkiristo?hebu fikirieni mauala hayo. hope mtatanabahi ya kuwa mnapoteza wakati wengu....Either you are too bright or too dumb......sorry
 
Hilo lipo wazi kwa yeyote mwenye upeo wa kutafakari ameshaligundua liko hivi, Bara then Visiwani, Bara then Visiwani,..mikoba ndo inakabidhiwa kwa staili hiyo, kwahiyo ndugu zanguni, JK na chama chake mikoba wanakabidhisha Visiwani in 2015 na huyu si mwingine ni...........Shamsi,.......nafikiri nimeeleweka. Na hili limewekwa wazi kwa uteuzi wake kama mbunge wa kuteuliwa, ndo anaandaliwa hivyo!! Msishangae akikabidhiwa wizara nyeti, sawa sawa??:whoo:
 
Kumbe mpaka sasa ngoma draw! Mkapa /Nyerere alafu Mwinyi /Kikwete
Naona kwa hizi sequence tulizoweka naona ajaye anajulikana
 
Relief.... Una uhakika kama sequence imeenda hivyo bara..visiwani.. bara... visiwani? wacheni na siasa zenu za kutisha watu... mwanzo mnasema hivyo baadae mkiristo .. muislamu mbona hamueleweki? na hii sequence ni Lazima Urais wa Jamuhuri ya Muungano upokezane hivyo au just ni kwa mgobea wa CCM tu?
 
Zanzibar kutoa rais wa muungano wasubiri labda hadi 2025 kama bado kutakuwa na muungano vinginevyo ndiyo imetoka hawatatoa milele quote my words.


mzanzibar ambaye kidogo kwa wakati wa karibuni alikuwa amejijenga bara kiasi cha kuaminika kupewa urais wa muungano ni SALIM AHMED SALIM .....labda na kwa kiasi DR SHEIN....sioni nani mwingine anaweza kuwashinda hao kwa wakati huu tuliyonayo.....zanzibar walipoteza wenyewe fursa ya kumtoa rais mwaka 2010.

Sasa naona kikwete amemleta NAHODHA ili apate kujijenga kuja kuwa rais wa muungano ...lakini bado ni mweepesi mno na sana sana mwaka 2010 aataishia kuwa waziri wa mazingira na muungano na GHARIB BILAL[makamu wa rais]...huku bara kwa sasa ni wazi kuwa PINDA anauzito kimamlaka [japo si kikatiba ] kuliko BILAL....
 
Kuna mambo manne ambayo yananifanya nitofautiane na wengi ambao wamewatabiria akinamama wa bara Uraisi 2015 au hata mmbara mwingineyo yeyote yule. Kwa mtazamo wangu hili kamwe halitatokea. kwa maono yafuatayo.....

Matukio haya ndiyo yanayoniongoza kusema hivyo;-

a) Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi masuala ya Muungano, Mheshimiwa Seif Khatibu alikuwa wa kwanza kulipiga hili baragumu kuwa hii sasa ni zamu ya Mzanzibari kuwa Raisi baada ya Kikwete...............Khatibu ni mtu ambaye yupo karibu sana na JK na kwa hiyo ni rahisi sana kujua kauli hiyo ilitokea wapi...............Kwa maoni yangu Khatibu alitumiwa na JK kupima upepo wa kisiasa unavuma vipi.............

b) Maamuzi ya makusudi ya kupendelea makundi maalumu yaliyofanywa na Kamati Kuu ya CCM chini ya uongozi wa JK ndani ya CCM katika kipindi cha miaka mitano iliyopita..................Haya ni pamoja na kuwazibia wabara kugombea uenyekiti wa UVCCM na kumnufaisha mzenji....Masauni.ambaye hata hivyo alikwenda kuwadhalilisha kwa kukosa sifa za kuwa kijana wa miaka 35 au chini ya hapo na kuwa na vyeti vya kughushi vya umri wake wa kuzaliwa............................

Vile vile uteuzi wa wanawake watatu kugombea nafasi ya uspika na kuyaondoa majina yote ya wanaumme kwa visingizio vya gender-balance...........Matukio haya mawili yaashiria udikteta ndani ya CCM kuchukua sura ifuatayo mwaka 2015:-

Pamoja na kuwa CC ya CCM itaruhusu wagombea wote kutoka kila kona ya nchi kugombea Uraisi lakini majina yatakayorudi ni matatu tu kutoka visiwani kwa minajili ya kile ambacho JK atasema ni kuwaenzi wazanzibari..................na ya kuwa bila ya kuchukua hatua za makusudi hawatakuwa na nafasi za kutoa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania....................

Usishangae kama nyuso mpya za visiwani zitaingizwa kwenye baraza la mawaziri litakalotangazwa hivi karibuni kwa minajili ya kuwajenga wazanzibari fulani fulani........kwa lengo la kuwaongezea sifa za kuukwaa uraisi.........na wengi wao watakuwa ni vijana ili huko mbele waseme tena hawa mbona ni vijana haswa na wengi tutakubali hizo ghiliba na kushangilia bila ya kujua malengo haswa nini............

Hivyo mkakati wa JK katika ni nani kumkabidhi nchi wabara andikeni mmeumia..................labda kura zisichakachuliwe na mmbara atatokea upinzani kuliongoza taifa hili..................

Lakini hilo nalo JK atahakikisha kamwe halitokei kwa sababu atakwamisha mabadiliko yoyote katika muundo wa NEC hadi baada ya uchaguzi wa 2015 ili kujenga mazingira ya mzanzibara aweze kutumia idara ya usalama wa taifa na NEC kutwaa madaraka isivyo halali na kinyume na sheria..............kama ambavyo yeye kajisimika madarakani bila ridhaa ya wapigakura na hivyo kuvunja katiba ya nchi hii.............

Habari njema ni kuwa CCM itagawanyika vipande vitatu vya kupinga maamuzi ya CC na upinzani utanufaika sana na wageni kutoka CCM.........na hapo kauli ya Baba wa taifa itakuwa imetimia ya kuwa ili CCM ishindwe kutwaa madaraka ni lazima ivunjike vipande vipande yenyewe.............................

Hivyo ukombozi wa kweli wa mtanzania unategemea sana JK afanye makosa haya comes 2015...................Eeeeeeeeeeeeeeehh mwenyezi Mungu mwongoze huko gizani nasi tupate unafuu wa kiuchumi na shida hizi zipungue za kudhulumiwa na mafisadi wa CCM......................

Haya ni maono yangu na ya kwako je..................waonaje mustakabali wa Taifa in 2015?

Mambo ya CCM tuwaachie CCM wenyewe, hapa tunatakiwa kujadili mgombea wa CHADEMA 2015 wana JF
 
Jamani kama mnakumbuka article of association inasema wazi lazima kuwe na mbadilishano wa marais kipindi akitoka bara basi kingine inabidi atoke visiwani
na possible presidential candidates wake kutoka visiwani ni:

Salim a. Salim
dr h mwinyi
shamsi vuai nahodha


na wengine mwaweza ongezea
 
Si kweli, hiyo thread yako imekosa data. Kwanza hakuna kitu kama article of association badala yake kuna article of union.

Na article hiyo imekuwa ikiongezewa vipengele kadhaa mara kwa mara. Kwa mfano, Aticle ya kwanza kbs ya mwaka 1964 iliainisha mambo 11 tu kama UNION MATTERs. Lakini kwa sasa mambo hayo yameongezwa na kufikia 33.

Cha msingi unachopaswa kujua ni kuwa Article of union halisi ya mwaka 1964 ni siri sana na haijawahi kuonekana hadharani.

Na hii inatokana na mambo makubwa mawili. Kwanza haijaainisha kimsingi masuala ya muungano, pili ambalo ni kubwa zaidi iliweka ukomo wa muunganno ni mwaka 1974.

Kwa mujibu wa makubaliano ya Mwalimu na Karume, ni kuwa muungano uwe wa miaka kumi na baada ya miaka hiyo kumi kama kila upande utaridhia basi waongeze mingine kumi.

Hivyohivyo waendelee kurenew kulingana na makubaliano ya vioogozi wetu na maridhiano ya wananchi wa pande znte.

Lakini ilipofika mwaka 1972 mzee Karume alionekana kuchoshwa na muungano hali iliyomfanya aonekane kuwa ikifika mwaka 74 hatakubali kurenew mkataba.

So inadaiwa zikapikwa njama za kumuua. Ndio maana hadi leo kifo chake ni utata mtupu.
 
WaZanzibari au Mzanzibari mzalendo hahitaji Uraisi wa Tanganyika au tuseme Tanzania mambo ya kuvishana vilemba vya ukoka yamepitwa ,kwani Uraisi wa nchi hiyo Tanganyika au Tanzania kwa sasa ni mzigo uliojaa lawama. ,kazi mnayo kujipapatua.
 
Jamani kama mnakumbuka article of association inasema wazi lazima kuwe na mbadilishano wa marais kipindi akitoka bara basi kingine inabidi atoke visiwani
na possible presidential candidates wake kutoka visiwani ni:

Salim a. Salim
dr h mwinyi
shamsi vuai nahodha


na wengine mwaweza ongezea

Ndoto mchana kweupe! Umesahau kama Mkapa na JK wote sio Wazanzibar na wameongoza kwa kufuatana. Ndio maana tunawaambia katiba ina matatizo na kero za Muungano kibao watu hawaelewi
 
Hicho kipengele kilifutwa mwaka 1992 wakati tunaanzisha mfumo wa vyama vingi.
Hata mswala ya makamu wa rais kutoka zbar kwa sasa siyo lazima just wanafanya hivyo ili kuupa muungano nguvu.
 
Hiki kipengere kinachosemekana kinaweka ukomo wa miaka kumi kumi, kwa uhai wa muungano, ndiyo kwanza nakisikia; hivyo, naomba kama kuna yeyote anayeweza kudhibitisha uwepo wa kipengere hicho.
 
Back
Top Bottom