Zamu ya Wananchi Kupasua Majipu Imewadia!

Queen V

JF-Expert Member
Jan 19, 2012
775
1,332
Je, una dondoo, taarifa au habari yoyote katika maeneo yafuatayo na ungependa imulikwe na vyombo vya habari?
➡Huduma mbovu katika ofisi mahususi ya umma
➡Ubadhirifu katika miradi au huduma za Jamii
➡Uzembe wa watoa huduma katika ofisi za umma
➡Biashara zisizo halali au michezo michafu katika huduma muhimu za umma (Afya, Maji, na Elimu)

Basi wasiliana nasi au tuma dondoo kwetu kupitia baruapepe: jielezehuru@gmail.com
 
Kwa nini nisianzishe uzi wangu niwape ninyi Taarifa, maana yangu ni kwamba mimi nitafaidika kivipi
Hii ni kwa wananchi wanaopenda kuona mabadiliko chanya kwenye jamii yao. Hii ndiyo faida kubwa ya jambo hili. Taarifa utakazotoa zitatumika kuleta mabadiliko katika sekta hizo kupitia tasnia ya habari.

Unaweza kuanzisha uzi wako, lakini naamini tukishirikiana tunaweza sababisha impact kubwa zaidi. Taarifa utakayotoa itafanyiwa uchunguzi wa kina kubaini chanzo halisi cha tatizo na wahusika.
 
Zifanyieni kazi kero mtakazoziona kwenye threads zetu huku huku JF , mutumulike huko mmmmm haya. Napita tu lakini
 
Hizo kazi sifanyi yaani Muhongo atume sms kwa meneja bandari kwamba Flowmeters zianze kufanya kazi halafu kesho yake waziri mkuu anaenda pale kumtumbua meneja ,Muhongo yupo mtaani anapeta tu

Wacha wale tu kama ni kula
 
Punguza hasira mkuu, nakumbuka maswali ya Majaliwa kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA kuhusu flow meters, alipotaja tu Muhongo/muongo alituma sms, Majaliwa akanywea, mama akaishia kutumbuliwa kwa sbb ya Muongo
 
Hawa ndio wale watu wa usalama nini?Mnataka kujua majina ya watu.
Hapana! Hii ni katika kusaidia kuyaleta majipu haya hadharani yakiwa yamefanyiwa uchunguzi na kuwasilishwa katika hali ambayo lazima italeta impact. Taarifa za mtoa hint zitakuwa salama kabisa.
 
na ninyi ni akina nani? tume/kitengo maalumu? bajeti yenu ya uendeshaji shughuli hizo inafadhiriwa na nani? mmeshafanikiwa kutumbua nini hadi sasa utuwekee hapa kama 'case study' tukuamini maana humu akina thomaso si kidogo! je malengo yenu yanamlika majukwaa ya mitandao tu? mna mkakati gani maana wenye kero zilizokubuhu hawana uwezo wa kusoma tangazo lako humu, pengine una vipeperushi, matangazo ya magazeti, luninga, mikutano ya hadhara, magari ya matangazo uliyokwishawahifanya? ni hayo tu mkuu.
 
Usije thubutu kutumia emeil zitaback fire na utakua held responsible under the law.. sheria ya mitandao ..yaan mmepitisha sheria ambayo haiwalindi wasema maovu motandaoni harafu mnarudi tena Acheni ufara na ujinga mkarekebishe kwanza ile sheria ya mitandao ndio irudi hapa kutuambia hiloo... Nawasii ndugu wanajf ukitumia email when it turns to bite you nothing shall stop you to held you responsible..
 
Back
Top Bottom