Zambia: Watu 21 wafa kwa ajali za Barabarani kipindi cha Krismasi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Watu wapatao 21 wamepoteza maisha na wengine 22 kujeruhiwa kutokana na ajali za barabara nchini Zambia katika kipindi cha Krismasi mwaka huu.

Taarifa hiyo ni kwa mujibu wa msemaji wa naibu wa polisi nchini humo Rae Hamoonga aliyoitoa hapo jana mbele ya wanahabari.

Kwa mujibu wa Rae, idadi ya watu waliofariki na kujeruhiwa imeongezeka kutoka 13 hadi 22 kuzidi idadi ya mwaka uliopita wa 2018. Idadi ya ajali za barabarani wakati huu wa Krismasi pia imeongezeka kutoka 125 mnamo mwaka 2018 hadi 139 kwa mwaka huu.

======

LUSAKA, Dec. 27 (Xinhua) -- At least 21 people were killed in road accidents in Zambia during this year's Christmas period, the police said on Friday.

Zambia Police Deputy Spokesperson Rae Hamoonga said the toll was a major jump from last year's 13, and the number of injured also rose, from 22 of the previous year to 31 this time around.

The number of road accidents this Christmas, at 139, also surged, from 125 recorded last year, the spokesperson said.
 
Hongera kwa Tanzania misimu ya sikukuu kama hivi tulizoea kuona matukio mengi ya ajali
Lakini sasa hali ni tofauti sana
Pongezi nyingi kwa taasisi zote xinazohusika na usimamiaji wa sharia za usafiri nchini
Na hapa naomba niwatambue wachache kati ya hao
Mh Rais kupitia taasisi zake kama
Jeshi la polisi kikosi cha Usalama barabarani
SUMATRA(LATRA) kwa ubunifu mkubwa wa ufungaji wa mabasi yote vifaa vya kuratibu mwendo(VTS)
RSA taasisi za mabalozi wa Usalama barabarani
TANROAD (Mfagale na timu yako kwa ukarabati mkubwa wa miundo mbinu )
Wizara ya afya (Hospitali zetu kitoa huduma kwa haraka kwa wahanga wa ajali zinapojitokeza na kuokoa maisha ya majeruhi)
CHAKUA (chama cha kutetea abiria Tanzania
Watanzania wote kwa ujumla yaani abiria kwa kubadili tabia za kushabikia mwendo kasi
Hakika tumepiga hatua kubwa sana licha ya changamoto ndogondogo ambazo bado zinajitokeza
KWA PAMOJA TUNAWEZA MUNGU IBARIKI TANZANIA

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom