Zambia wameweza (hongera Satta), zamu yetu ni mpaka tuing'oe CCM madarakani

Sisi tuna laana, na mpaka iondoke ndipo tutafanya lolote. Laana yenyewe ni JK. Unajua unapoingia madarakani kwa nguvu na ujanja ujanja Mungu anaiacha nchi. Tunashindwa kila mahali, Afya hoi, Elimu ni balaa, umeme siuji nini, maji ndiyo usiseme, sasa michezo, bado ni 'kichwa cha mwenda wazimu'.
 
Wachezaji wa lizee limoja linaitwa Sunday Kayuni hao,wachezaji hawana nidhamu wala uzalendo unawang'ang'ania wawemo kwenye team ya taifa
Hiyo nayo shida. Serikali imewekeza ikamleta na kocha lakini uongozi wa mpira. Kuna watu hapa tz wanaitwa watu wa mpira, hta rais wa TFF analijua hilo. Usipowajua hao hupati uongozi kwenye soka. Hadi hao watu wa mpira watakapodhibitiwa ndio tutaona matunda. Sunday Kayuni naye ni hao hao watu wa mpira. Wachezaji wanachaguliwa kwa kuwa wana uhusiano na nani ama wwmehonga kiasi gani. RUSHWA KILA MAHALA
 


MMENIONA SINKALA ?


attachment.php
 
Zambia wameweza, sisi tunasubiri nini?
Tukiendelea na CCM tutabaki kua wasindikizaji katika soka. Hongera SATTA hayo ni mafanikio ktk mwaka wako wa kwanza wa uongozi

Hongera kwanza ziwaendee waZambia kwa kufanya maamuzi magumu
 
Tatizo letu watanzania ni kulifanya kila jambo kuwa la kisiasa.... hatuwezi hata kuipongeza serikali na Rais KIKWETE angalau kwa kutuletea kocha ambaye kiukweli alijitahidi kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kisoka? je hatujui kuwa ni serikali ya CCM ndiyo iliyotujengea uwanja wa kisasa chini ya mzee MKAPA? hata haya nayo mnasema CHADEMA ndiyo itakayofanya vizuri?
 
Neema huja wakati mkiwa na viongozi wasafi, wenye kutumikia watu wao siyo viongozi wasiopenda kuwatumikia wananchi!!

Absolutely true! Siku zote HAKI huliinua taifa.

Imagine these scenarios:

(i) Mchezaji anaingia uwanjani mfukoni hana kitu na nyumbani pia hajaacha kitu cha maana na wala hakuna ahadi yoyote kutoka kokote ikiwapo serikalini ya motisha wowote. Si kwamba serikali haitaki wachezaji wake wapate, la hasha bali hali halisi ya serikali ndivyo ilivyo na kila mtu na wachezaji wanajua hivyo na ndivyo ilivyo na hata kiongozi mkuu na viongozi wote wa serikali wanaishi hivyo. Pamoja na umasikini wetu, HAKI imetamalaki. Naamini kwa mazingira haya hata mtoto mdogo atafanya kazi kufa na kupona ili kuitetea nchi yake. Ni lazima atajituma kwa bidii akitanguliza uzalendo mbele kukiwa na matumaini ya "one day yes".

(ii) Kama ilivyo kwa (i) hapo juu, mchezaji pia anaingia uwanjani akiwa "hohehahe" na hakuna ahadi yoyote ile hata kama kutakuwa na ushindi. Lakini, akiwa uwanjani, wazo linamjia kwamba huku nyuma kuna kundi fulani, pamoja na umaskini wa taifa letu, kundi hilo limejipa jukumu maalumu la kulitafuna taifa kadiri ianvyowezekana yaani kula kuku kwa mrija. Tena kundi hili limejitungia hadi sheria za kulilinda dhidi ya "uhalifu" wao huu. Mchezaji anakumbuka posho kubwa kubwa wanazojilipa huko serikalini, posho kubwa kubwa za wabunge na bado wanadai kuongezewa, n.k. Ni lazima ataathirika kisaikolojia ambayo itashusha kabisa performance yake.

Zambia wanaangukia katika kundi la kwanza na sisi tunaangukia kundi la pili. TAFAKARI.
 
Tatizo letu watanzania ni kulifanya kila jambo kuwa la kisiasa.... hatuwezi hata kuipongeza serikali na Rais KIKWETE angalau kwa kutuletea kocha ambaye kiukweli alijitahidi kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kisoka? je hatujui kuwa ni serikali ya CCM ndiyo iliyotujengea uwanja wa kisasa chini ya mzee MKAPA? hata haya nayo mnasema CHADEMA ndiyo itakayofanya vizuri?


Sasa kama ni kweli Maximo alikuwa anakaribia kutuweka kwenye ramani ya dunia kama unavyotaka tuamini ilikuwaje basi wakamtoa??


Na huo uwanja mmoja kwa miaka 50 ya Uhuru ndiyo unataka tuamini kuwa CCM wanamikakati sahii ya michezo nchini?? Subiri London Olympics tuone hata kama wataweza kupeleka wanamichezo watano!!!
 
Kuna yule beki aliyetoka mwanzoni kabisa mwa game uku analia kwa uchungu alio nao kwa nchi yake.
 
hii ni results ya project yao ambayo waliianza miaka ya tisini.... baba zao walikufa mwaka 1993 wakati hawa walioshinda jana walikuwa na miaka miwili mpaka mitano tu; sisi tunapenda zima moto hakuna mpango wowote wa kitaifa kuhusu mpira, leo hii nenda TFF omba mpango mkakati wa kukuza kandanda kwa miaka 10 ijayo - utapewa mikaratasi kibao ya madesa matupu lakini practically ni sifuri. mimi nimeshaamua niangalie kandanda ya wenzetu tu maana hili la kwetu ni maumivu matupu.
 
Siyo kwa mpira tu,nadhani ameweza hata kutimua Waziri wake mmoja ambaye alikuwa mpigaji debe wake wakati wa kampeni zake kwa hongo ya $2000.Sasa sijui kama kwetu twaweza hili!
 
Zambia wameweza, sisi tunasubiri nini?
Tukiendelea na CCM tutabaki kua wasindikizaji katika soka. Hongera SATTA hayo ni mafanikio ktk mwaka wako wa kwanza wa uongozi:smash: :shock:​

Hamuwezi...... Ng'oooo
 
Back
Top Bottom