Zambia: Rais Hakainde Hichilema awafuta kazi IGP, CDF na DPP. Aahidi kumaliza utawala kandamizi wa mtangulizi wake

pasi padinde

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
282
299
RAIS MPYA WA ZAMBIA AMFURUSHA OFISINI MKUU WA POLISI (IGP), MKUU WA MAJESHI (CDF) na DPP, AAHIDI KUMALIZA UTAWALA KANDAMIZI WA MTANGULIZI WAKE

RAIS mpya wa Zambia Hakainde Hichilema jana Jumapili August 29,2021 ameteua wakuu wapya wa jeshi na kuwaondoa wakuu wote wa polisi akiwemo IGP na Mkurugenzi wa Mashtaka na Makosa ya jinai huku akiahidi kumaliza utawala kandamizi wa mtangulizi wake.

Akitoa hotuba yake Rais amesema wakuu hawa wa vyombo vya dola walitupilia mbali weledi na kuikanyaga Sheria ili kumkandamiza mwananchi kwa manufaa ya Viongozi wachache huku wakijua wazi kuwa ni kinyume cha Sheria.

Rais ameongeza kuwa katika utawala wa mtangulizi wake IGP na wakuu wengine wa Polisi walitumia madaraka yao vibaya kula rushwa, kubambikia raia wasio na hatia kesi, kupora mali za raia, kutesa, na hata kuua raia wasio na hatia.

"Mimi mwenyewe nimepitia mateso makali ya polisi, wamenikamata mara kadhaa, wamenibambikia kesi na kunishitaki kwa UONGO mara kadhaa, nimetupwa gerezani kwa kesi ya kubambikiwa kuwa Mimi ni mhaini niliyetaka kumuua mtangulizi wangu Rais Edgar Lungu. Kwa haya yote nitakuwa MNAFIKI nikisema namuamini IGP na wakuu wengine wa vyombo vya usalama na ndio maana nimeamua kuwafuta kazi wote huku Sheria ikisubiri kufuata mkondo wake" amesema Rais Hakainde Hichilema.

"Sitaki kurithi na kufanya kazi na Viongozi ambao mikono yao inanuka damu, MATUMBO yao yameshibishwa na rushwa, watu ambao wanadhani kuwa unapokuwa na cheo sasa una fursa ya kutesa na kunyanyasa wananchi. Nataka kufanya kazi na watu ambao wana HOFU ya Mungu, watu wanaojua kuwa cheo ni dhamana ya kuwatumikia wananchi na sio dhamana ya kutesa wananchi. Watu wanaojua kuwa nje ya madaraka na vyeo vyao wao ni binadamu tu kama binadamu wengine." aliongeza Rais Hakainde.

IGP wa Polisi Nchini Zambia Afande Kakoma Kanganja tarehe 25.11-2019 aliwaonya wanachama wa Chama cha Upinzani nchini Zambia(UPND) kuwa wakijaribu kuandamana polisi wake WATAWAKUNG'UTA sawasawa pamoja na kiongozi wao Hakainde Hichilema watamvunja miguu kwa risasi. IGP huyo alienda mbali na kusema hawezi kukubali kuona vibaraka wa magharibi wakiiharibu Zambia au wakimharibia kibarua chake.

Katika uteuzi huo Rais Hakainde amewateua wafuatao kuchukua nafasi za waliofutwa kazi:

1. Rais amemteua Lieutenant General Dennis Alibuzwi kuwa Mkuu Mpya wa majeshi yote ya Zambia (CDF) na Naibu wake ni Major General Geoffrey Zyeele, ambaye pia kwa nafasi yake yeye ndiye mnadhimu Mkuu wa Jeshi "Chief of Staff."

2.Rais amemteua Lieutenant General Collins Barry mwenye asili ya Scotland kuwa Mkuu Mpya wa Jeshi la Anga la Zambia "Zambia Air Force ZAF". Naibu wake ni Major General Oscar Nyoni.

3. Rais pia amemteua Remmy Kajoba kuwa Mkuu Mpya wa Polisi (IGP).

Wengine walioteuliwa ni Mkuu Mpya wa Jeshi la kujenga Taifa na jeshi la ardhini. Mkuu wa Jeshi la wana maji akihifadhi kiti chake

Aidha Rais Hakainde amewashukuru maafisa aliowafuta kazi kwa kipindi walichoitumikia Zambia katika nafasi zao.

Rais pia amewaonya wakuu wapya wa vyombo vya ulinzi na usalama akiwaambia kuwa " na ninyi niliowateua nataka niwaambie lazima muwatumikie watu kwa weledi na uadilifu usiotiliwa shaka, muwatumikie watu kwa HAKI na usawa kwa moyo wenu wote huku mkihakikisha kuwa HAKI za binadamu, UHURU wa watu vinaheshimiwa. Siku zote mkumbuke kuwa hakuna cheo wala madaraka vinavyokupa uhalali wa kumuonea mtu yeyote, ishikeni, Sheria, iishini Sheria na msimamie Sheria kwa HAKI bila kumkandamiza mwananchi. Polisi kataeni maagizo yanayoenda kinyume na kiapo chenu, kinyume na weledi na kinyume cha Sheria za Zambia" amesema Rais Hakainde.

Haki huinua Taifa cheo ni dhamana
 
Zambia sasa kuna DEMOCRACY ya kweli.
Hakuna Mungumtu.
Rais sasa aweke mazingira ya kuimarisha katiba ya nchi, ili wasirudi nyuma, bali wazidi kukua.
 
hii salamu tosha kwa IGP ziro IQ
 
Rais Samia afuate nyayo za Hichilema awafute kazi wale waliokuwa wanaamini wao wanamtumikia Magufuli sio Tanzania ateuwe watakaoitumikia Tanzania na Watanzania.
 
USIKU WA SAFISHA SAFISHA KTK VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA, SAFU MPYA YATEULIWA
29 August 2021
Lusaka, Zambia

In a night announcement, President Hichilema drops Commanders of Zambia Army, Air Force, National Service and Inspector General of Police​

In a night announcement, President Hichilema drops Commanders of Zambia Army, Air...

Video courtesy of Makvan HD

President Hakainde Hichilema has dropped Commanders of Zambia Army, Air Force, National Service, and Inspector General of Police and appointed new Service Chiefs in their place.

In a night announcement from his residency in new Kasama, President Hakainde thanked those that served and has called on citizens to respect them as they have served the country with diligence, and urged that they be not demonized.

President Hakainde Hichilema made various changes in the defence and security wings of the country. President Hichilema has appointed Zambia Army Deputy Commander Dennis Alibuzwi as Army Commander and consequently promoted him to the rank of Lieutenant General with immediate effect.

Lieutenant General Alibuzwi replaces Lieutenant General William Sikazwe who served as Zambia Army Commander for two years and eight months since his appointment in 2018.

The President has recalled Brigadier General Geoffrey Zyeele and appointed him as the new Deputy Army Commander and Chief of Staff, and has consequently elevated him to the rank of Major General.

At the Zambia Air Force (ZAF), Mr. Hichilema has retired Air Commander, Lieutenant General David Muma and replaced him with Brigadier General Collins Barry, who he has subsequently promoted to the rank of Lieutenant General.

Further, Brigadier General Oscar Nyoni has been appointed as ZAF Deputy Commander, and has been promoted to the rank of Major General.

President Hichilema has also made changes at the Zambia National Service (ZNS) by relieving ZNS Commandant Lieutenant General Nathan Mulenga of his duties and replacing him with Brigadier General Patrick Solochi, who has since been promoted to the rank of Lieutenant General.
Lieutenant General Patrick Solochi will be deputised by now Major General Reuben Mwewa who was before this appointment and subsequent promotion, at the rank of Brigadier General.

Meanwhile, the President has recalled and appointed Remmy Kajoba as new Inspector General of Police, replacing Mr. Kakoma Kanganja.

Mr. Hichilema has appointed Mr. Milner Muyambango to the position of Deputy Inspector General of Police in charge of operations and also appointed Mrs. Doris Chibombe as Deputy Inspector General in charge of administration.

President Hichilema has meanwhile relieved all Provincial Commissioners of Police of their duties with immediate effect, pending normalisation of the appointment process to the said portfolios.

The President stated that there will be re-organisation in the appointment of Provincial Commissioners of Police.

He explained that the current system is that the Provincial Commissioners of Police and the Inspector General of Police (IG), together with the two deputies, are appointed and sworn-in by the President, a situation he said creates a problem in the command structure.

“To the new office bearers, we want to state that you must have the interest of the people at heart and serve the country diligently while ensuring that human rights, freedoms and liberties are respected,” President Hichilema said.

The President has meanwhile thanked all the officers that have been relieved of their duties whom he said will be re-assigned to other duties later.

“We are grateful for their support when they served the country in these portfolios,” he said.
Source : Zambia : In a night announcement, President Hichilema drops Commanders of Zambia Army, Air Force, National Service and Inspector General of Police
 
Kwa haya yote nitakuwa MNAFIKI nikisema namuamini IGP na wakuu wengine wa vyombo vya usalama na ndio maana nimeamua kuwafuta kazi wote huku Sheria ikisubiri kufuata mkondo wake" amesema Rais Hakainde Hichilema.

Nukuu ya maneno mazito yaliyosemwa na Mkuu wa nchi na Amiri Jeshi Mkuu wa vyombo vya ulinzi na usalama wa Zambia, Mh. Rais Hakainde Hichilema.
 
Lusaka, Zambia

PRESIDENTIAL ADDRESS | NEW ZAMBIA POLICE

H.E PRESIDENT HAKAINDE HICHILEMA
 
Hatuna lA kujifunza
Tuta jifunzaje wakati hatukubali kukosolewa? Mmoja wetu kasema hatukatwi kodi tu imekuwa balaa kubwa Nchi inasimama kumshughulikia, Bungeni imekuwa ajenda kuu, wakati tuliwatuma wakatutetee? TZ acha kabisa bonge la mfano bora wa Demokrasia Afrika 🤣 🤣 🤣
 
Wakati huohuo huku Tanzania yule IGP wa Bwana Chato ndiye Rais wa nchi.
 
Back
Top Bottom