Sajenti
JF-Expert Member
- Apr 24, 2008
- 3,651
- 412
Raisi mpya wa Zambia Michael Satta a.k.a King Cobra amesema kuwa utawala wake utaendesha serikali ya nchi hiyo kwa mujibu wa amri 10 za mungu. Katika kutekeleza amri hizo amesisitiza zaidi katika amri ya kutoiba na kwamba hategemei katika kipindi cha utawala wake kuna raia wa Zambia atakayejaribu kufanya wizi.
Haikufafanuliwa zaidi ni wizi wa aina gani ambao Raisi Satta alikuwa akiuzungumzia kwani yawezekana pia hata wizi wa kuku, bata na vitu vingine vidogo vidigi ukawa unafanyika. Raisi Satta ambaye ni muumini wa dhehebu la Roman Catholic amesema pia serikali yake itafanya kazi kwa karibu na kanisa la dhehebu hilo katika kile anachoamini kuwa kuifanya Zambia moja ya nchi yenye wacha mungu.
Hakueleza kwa wale watakaobainika kuiba watafanya nini, lakini inasemekana kuw Raisi Satta ni miongoni mwa viongozi wachache katika taifa hilo la kusini mwa bara la afrika wenye misimamo mikali na wasioogopa kufanya maamuzi magumu. Jina la utani la King Cobra alipewa na wananchi wa Zambia kutokana na ujasiri wake wa kutoa matamko makali sana dhidi ya serikali zilizopita na hasa zilipokuwa zikifumbia macho ufisadi katika tawala hizo.
Source: VOA news..