Zambia: Azirai baada ya kugundua mkewe ni mmiliki wa nyumba waliyopanga

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Jul 1, 2017
3,032
4,028
Mwanaume mmoja raia wa Zambia aliyetambulika kwa jina la Martin Stampa, anadaiwa kuanguka na kuzirai baada ya kugundua kuwa mke wake ndiye “mwenye nyumba” wake.

Kulingana na taarifa za mitandao ya kijamii nchini humo, imesema, Stampa (37), aliishi katika nyumba hiyo kwa miaka 15, na alikuwa akilipa kwacha 3500 kila mwezi ambazo mkewe alidai kuzipeleka kwa mwenye nyumba wao.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa ugomvi ulizuka baada ya bibi huyo aliyetambulika kwa jina la Lombo Lushomo (27), kugundua kuwa mumewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa.

Mitandao hiyo, inaarifu kuwa Martin Stampa alimwambia mke wake kuwa alipata kimada kwa sababu alitaka mtu mwenye akili na anayejihusisha na mazungumzo mahiri ikiwemo kujituma katika utafutaji.

Inadaiwa kuwa, jambo hilo lilimkasirisha Bi. Lushomo, ambaye alimtaka kuhama na kumpisha na kumwambia kuwa hana akili za kutosha kwani amekuwa akimlipa kodi ya kila mwezi kwa sababu nyumba wanayoishi ni yake.

Mara baada ya kuoneshwa hati, ya nyumba hiyo, inasemekana Martin alipoteza fahamu na kuzimia kitu ambacho kilisababisha Wananchi kumpa msaada wa kumwagia maji ili kumzindua kisha kumuwahisha Hospitalini.

Attachments

  • Coma.JPG
    Coma.JPG
    13.6 KB · Views: 6
Ndio maana wanaitwa Hawa, tuishi nao kwa akili. Nilishaona mke amempangia Mchepuko wake kwenye nyumba ya mume wake na kuishi kwa kupewa chakula kinacholetwa na Mume wake bila mume kujua, Hawa watu tuishi nao tu, unaishi na mtu bila kujua analowaza, Mungu ametuwekea Siri kubwa kwenye mioyo yetu.
 
hahhahhahaha habari ya uongo sanaaaaa yani mwanamke ana miaka 27 na wameishi katika nyumba kwa muda wa miaka 15 hahahhaha labda zipunguzwe namba za miaka ya nyumba kutoka 15 had 3 sawa unataka nambia uyo mke aliolew akiwa na miaka 12 na alimiliki nyumba akiwa na miaka iyo au pungufu ya iyo na ata kama alirithi kwa miaka 12 nyumba lazima isimamiwe na ndugu.
 
Wabongo kwa ubishi hajambo 😄
 
Ushuzi mtupu uongo mtupu. Bora umeshtukia
 
Mwanaume mmoja raia wa Zambia aliyetambulika kwa jina la Martin Stampa, anadaiwa kuanguka na kuzirai baada ya kugundua kuwa mke wake ndiye “mwenye nyumba” wake.

Kulingana na taarifa za mitandao ya kijamii nchini humo, imesema, Stampa (37), aliishi katika nyumba hiyo kwa miaka 15, na alikuwa akilipa kwacha 3500 kila mwezi ambazo mkewe alidai kuzipeleka kwa mwenye nyumba wao.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa ugomvi ulizuka baada ya bibi huyo aliyetambulika kwa jina la Lombo Lushomo (27), kugundua kuwa mumewe alikuwa na uhusiano wa kimapenzi nje ya ndoa.

Mitandao hiyo, inaarifu kuwa Martin Stampa alimwambia mke wake kuwa alipata kimada kwa sababu alitaka mtu mwenye akili na anayejihusisha na mazungumzo mahiri ikiwemo kujituma katika utafutaji.

Inadaiwa kuwa, jambo hilo lilimkasirisha Bi. Lushomo, ambaye alimtaka kuhama na kumpisha na kumwambia kuwa hana akili za kutosha kwani amekuwa akimlipa kodi ya kila mwezi kwa sababu nyumba wanayoishi ni yake.

Mara baada ya kuoneshwa hati, ya nyumba hiyo, inasemekana Martin alipoteza fahamu na kuzimia kitu ambacho kilisababisha Wananchi kumpa msaada wa kumwagia maji ili kumzindua kisha kumuwahisha Hospitalini.

Sijaendelea kuisoma hii tamthilia.
Mtu amekaa kwenye nyumba miaka 15.
Mke ana miaka 27.
27 toa 15 ni 12.
Sasa Jamaa ana miaka 37, 37 toa 15 ni 22.
Kwa hiyo jamaa alioa mtoto wa miaka 12 na yeye 22, na wakakaa humo miaka 15!

Ngumu kumesa!!
 
Hii hibari ya uongo. Huyo alizimia kwa sababu tofauti kabisa. Nilisoma sehemu.
Hukusoma pia umri wa mwanamke?

maana hapa kaandikwa ana miaka 27, na kaishi kwenye ndoa miaka 15.

Je aliolewa akiwa na miaka 12? (yaweza kuwa sahihi)

lakini Je, hio nyumba aliijenga akiwa na hio miaka 12?
 
Back
Top Bottom