Zamani walikuwa wanaitwa "mama ntilie" ila sasa ni "mama lishe". Kwani hakuwezi kuwa na jina la Kiswahili lenye staha kwa hawa dada zetu "barmaids"?

Issue sio hadhi jina bali matendo. Hata ukiwapa jina lengine kama matendo ndio yale yale hilo jina pia litaonekana halina staha.
 
Kiswahili chake ni muhudumu wa baa. Umezungumzia jina lenye staha sasa kuitwa bar maid na ni kweli ni bar maid staha ipi wanaikosa?
Labda wanakosa staha, kutokana na mambo,na taratibu zao, kama ni hivyo, hata wakiitwa malaika, na neno malaika litakosa staha!
 
Habari za wakati huu jamiiforums.

Zamani walikuwa wanaitwa "mama ntilie" ila sasa ni "mama lishe". Kwani hakuwezi kuwa na jina la Kiswahili lenye staha kwa hawa dada zetu "barmaids"?

Binafsi ninaona kama wanasiasa wamewasahau sana hawa akina dada wanaotoa huduma kwa wateja kule bar. Neno mama lishe, kama sijakosea, lilianzishwa na mzalendo mwenzangu Hayati mzee B.W Mkapa (wahenga mtanisahihisha katika hili kama nitakuwa nimekosea) sasa mbona "barmaids" nyie wanasiasa mmewasahau?

SOMA PIA>>> Kuna haja ya Serikali kupitia wakuu wa wilaya na mikoa kuwabana wamiliki wa baa ili dada zetu wahudumu wapewe kadi za bima ya afya ya CHF?
Kwani barmaid ni jina baya? Au kwa sababu siyo lugha yako?

Kiswahili chake ni Mhudumu tu, shida yako nini? Acha kufikiri kichatochato
 
Bar maid...a woman who serves drinks in a bar. Kwani hili jina ambalo linaeleza kazi yao halina staha?

Labda anataka tutoe "Maids" na tuweke "attendants" japo sidhani kama itasaidia maana mtazamo hasi wa watu hausababishwi na jina ila wanavyoitazama kazi yenyewe
 
Huyu jamaa unapoteza muda kumuelewesha. Ni wale watu wanaodhani neno ''barmaid'' lina maana sawa na kahaba au changudoa. Ni watanzania wengi sana hawajui hili neno ni la kiingereza. Wanadhani linawakilisha au linaelezea sifa za ukahaba wanazokuwa nazo wahudumu wengi wa bar.
Nimefurahi sana kujua kuwa umetambua hilo neno linachukuliwa vibaya na watanzania wengi. Sasa ni jina lipo zuri la kiswahili litafaa?
 
Back
Top Bottom