Zamani tulikuwa tunakula Maisha hasa si kama sasa.Siku tu hazigandi ila nakumbuka sana

GuDume

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
6,652
14,247
Miaka ile is ndo tuliishi maisha bwana asikwambie mtu. nakumbuka miaka hiyo mzee amerudi toka ng'ambo alituletea raba mtoni.... aaahh...... hiz mabinti walikoma nazo sana... maana walikuwa wananiona mtoto wa kidosi hasa. tulikuwa tunapiga jeans za LEE original kabisa kabla mchina hajaanza kutengeneza madude due yake ya kuleta kizungu zungu.

unapika pekosi na shati la juliana au eagle... kijana maridadi chini umevaa teremka tuzoze. kama umebarikiwa kuw ana afro umezichana kwa kichanio cha chuma ambacho kiliwekwa kwenye moto kwanza ili nywele zinyooke. halafu zikikaa sawa unachomeka kitana au kichanio kingine kuonesha wewe una afro limekubali.

ilikuwa ni ngumu kumkuta kijana amevaa mlegezo maana hiyo ingeonesha ishara mbaya sana kwa jamii... ilikuwa mwanaume mwanaume kweli na mwanamke mwanamke kweli.siku hizi mna akina delicious... inaumiza sana. ukienda disco kama upo lege lege wababe wanakuchukulia demu wako hivi hivi. hii ilitujenga tuwe mashababy hasa.... na pia mnaenda na wenzio kadhaa... ilikuwa hukuti mwanaume nyoro nyoro... ilikuwa wanaume wanaume hasa.

kuna mashati yalikuja ya bahama na suruali za mchelemchele miaka ya 70 mpaka 80s. ilikuwa shida...kitambaa kama cha uji uji hivi.. unapiga ile na kiatu chako teremka tuzoze... linakuwa puto hivi na suruali inabana juu chini fundi anakuelegezea.

sisi tulikuwa na mabitozi. huyu bitozi anatembea ana kitambaa cheupe mfuko wa nyuma wa suruali kinanin'ginia hivi. ukimkuta kavaa na raba mtoni anadunda hivi anatembea kama chini pamoto... au anatembea kisigino hakigusi chini ananesa hivi utadhani amekanyaga mwiba haujachomolewa bado kisiginoni. unamwambia nini bitozi? ana sigara mdomoni inafuka moshi tu anaweza akawa hata ule moshi havuti basi tu swaga za kimamtoni.

tulikuwa na utamaduni wa kwenda kuangali sinema. majumba kama AVALON,EMPIRE, STARLIGHT n.k yalikuwa yanatutoa sana siku za Jumatano, Ijumaa, Jumamosi na Jumapili. na pia tulikuwa tunakuja New Africa kucheck Videos za wanamuzi mbalimbali wakiwemo wa kikongo na Afrique... majengo mengine nimeshayasahau kwa sasa yamebadilishwa kuwa nini...

mademu wetu

walikuwa ni rahisi sana. hawana gharama... ukimpa pesa ni za kusukia au ataweka curly. basi hana makuu chini amevaa mkuki moyoni au naye ana teremka tuzoze. blauz ya kung'aa ng'aa hivi ya stay away from fire. huyu ukimnunulia tu beer ya ndovu au safari basi anapata amani kabisa. tena hanywi nyiiiiiing.. hapana. mbili tatu tu.

tulikuwa tunakula mademu bila wasiwasi wa kupata ngoma miaka ya nyuma ya 70. kabla hu ugonjwa SIDA au Ugonjwa wa Kisasa haujaja hapa nchini. matatizo yetu yalikuwa ni kaswende,gonorea na kisonono... hayo tu. ingawa nayo yalitutesa sana. dawa yetu kubwa ilikuw arangi mbili. upande red upande black. ndo dawa ya vidonda hiyo na magonjwa mbalimbali.

ukiwa huna pesa disco vumbi kiingilio chako ni kumwagia maji ule ukumbi wa disco kwa siku hiyo.. kuondoa vumbi. then jioni wanakuja watu wamepaka mafuta ya RAYS AU SHANTA wana meremeta ile mbaya.... yaani hata mbu au inzi akitua ana nasa. wenye pesa tulikuwa tunapakaa mafuta ya kunukia ya AYU/ YU. kwenye kimkebe hivi. mpaka miaka ya 90 zilipokuja lotion mbalimbali ikiwemo maarufu sana ya ZANA sijui kama ipo.

wadada walikuwa wanatengeneza mikorogo toka miaka hiyo. sabuni kama JARIBU/MEKO zilitumika sana kutengenezea mkorogo. hizi walizikwangua kupata unga unga ambao ulichanganywa na lotion ya COCOA BUTTER na GLYCERIN halafu wadada wangejipaka usiku wakati wa kulala na kuja kunawa asubuhi.

maisha yalikuwa rahisi sana..... kwa kweli siku hazigandi nasi wazee wa zamani tulikula maisha na wengine mpaka sasa katika kizazi hiki cha Dot Com tunaendelea.. na wewe mzee mwenzangu unaweza kuwa na kumbu kumbu zako.
 
Bugaloo maarufu juu pima chini kadiria na raizon yako ngazi tatu kitaa lazima wakukome duh ama kweli ya kale ni dhahabu acha nizeeke mimi
 
enzi za kibisa. soda zilikuwa mirinda, fahari, vimto , kipindi hicho cha mumiani, ukipisha na londo jekundu ni mbio tuu, wanyonya damu, kipindi ambacho tulikuwa tukisikiliza vituko vya juma na uledi, pwagu na pwaguzi, ndicho kipindi magazeti kama heko na mzalendo yalikuwa ktk chati, shilingi ilikuwa na thamani japo niliikuta mwisho mwisho, lakini niliitumia kwa kununua, kande, viazi na mseto shuleni, viatu vya chachacha na vile vya mataili ya magari, huku mpira wetu ukiwa ni sodo, sasa uwe na bahati mbaya ile kufuri ya V.I.P ikakatika kimkanda wakati mnagombea kupiga kona...sisi tulikuwa madogo na mara nyingi papuchi tulizipata kwa wadada waliotuzidi umri, huko, kwenye mabwawa, mtoni ama kisimani.
 
Inaonesha ulikua wakishua sana mkuu, hilo life style lenu ndio lilifanya washua wetu watulazimize kukariri kitabu wakiamini maisha ni 22/7 (pie) wasijue kusoma alama za nyakati

kweli Yajayo ..................,
 
enzi za kibisa. soda zilikuwa mirinda, fahari, vimto , kipindi hicho cha mumiani, ukipisha na londo jekundu ni mbio tuu, wanyonya damu, kipindi ambacho tulikuwa tukisikiliza vituko vya juma na uledi, pwagu na pwaguzi, ndicho kipindi magazeti kama heko na mzalendo yalikuwa ktk chati, shilingi ilikuwa na thamani japo niliikuta mwisho mwisho, lakini niliitumia kwa kununua, kande, viazi na mseto shuleni, viatu vya chachacha na vile vya mataili ya magari, huku mpira wetu ukiwa ni sodo, sasa uwe na bahati mbaya ile kufuri ya V.I.P ikakatika kimkanda wakati mnagombea kupiga kona...sisi tulikuwa madogo na mara nyingi papuchi tulizipata kwa wadada waliotuzidi umri, huko, kwenye mabwawa, mtoni ama kisimani.

Ya kale ni dhahabu.... TULIKOTOKA NI AFADHALI TUNAKOENDA TUJIADHALI.
 
Back
Top Bottom