Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

Sio tu ndugu ila kwenye maisha hasa ya watu weusi aka WaAfrica jaribu sana kuwaweka watu mbali na wewe...uwe na urafiki wa kawaida tu na watu, haya mambo yakujifanya sijui rafiki yangu wa karibu na kujuana kiundani ni hatari, ndugu zako ni watoto zako na mkeo ( if she is good for you) wengine wote waweke mbali kidogo...
 
Lakini ukifa watakuzika tu utake usitake na watoto wako watatunzwa na wao.
Kwahiyo unachukua perceived future catastrophes kuji-hold hostage kwa hawa watu?

Its funny,maana na wao si watakufa like anybody else au wao wana tiketi ya kutokufa?

Kuzikwa is not an issue here....

Zote ni fear impacted by the society on you and u will never be free ukiwa hivi!
 
Ndugu wana mambo ya ajabu sana..
Mimi wakati nipo mdogo nilikuwa namshangaa baba yangu kwa kuwakwepa ndugu zake nikamuona kama katili na ana roho mbaya..wakati nasoma hakuna alienisumbua kabisa..
Nilivyopata mahali pa kujishikiza tu.. nikafungua na kiduka mahali.. basi wanaona kama mimi mo sasa...
Kila siku matatizo yao tu.. mara mtoto anaumwa mara wao wanaumwa.. sa hv nimekubali dhambi tu..
 
Mtu ambaye hajakutana na ushenzi wa watu kama hawa atakupinga.

Ukweli ndio huo, ndugu - Baba wadogo, kaka, shemeji, dada, wifi, shangazi, wajomba, wake, waume, wadogo zetu nk. Ni watu tuishi nao kwa akili za kujiongeza usidhani kwa kuwa unawapenda wanakupenda pia.
Kweli kabisa
 
Mda mwingine kutumia hekima kwenye changamoto hizi za kifamilia ni kujimaliza mwenyewe, Unaonesha upendo kwa watu ambao wao hawana upendo na wewe. Wanakuchekea kinafiki ukiwapa msaada, wakitoka wanapanga mipango ya kukudhuru na kukuombea uharibikiwe.

Binadamu wana Roho mbaya sana, hata Yesu hakuwa na kosa lakini walimsulubu msalabani japo aliwapa chakula wakiwa hoi na njaa walivokula na kushiba wakaanza kumtesa. Wanaonesha kukupenda lakini mioyo yao imejawa chuki. Naandika haya nikiwa na Jazba siku kadhaa zilizopita ningekuwa niko karibu na viumbe hawa waliofanya niandike hapa basi leo maiti kadhaa zingekuwa mochwari au zishazikwa na mimi ningekuwa nyuma ya nondo.

Ndugu zangu kwa sasa ni ndugu wa damu tu wadogo zangu na mama zangu. Hawa wanaojiita ndugu za baba huu ushenzi wanaoniletea kwenye familia yangu na mimi binafsi pamoja na kujishusha sana kwao Imefika mahali imetosha, naona ni kama nakumbatia kundi la wachawi huku nikijifanya nawapenda. Huku wao wakiwa na mipango yao binafsi

Nimesaidia sana kifedha na kila aina ya msaada lakini hawa watu nia yao sio njema Lakini majibu niliyowapa nadhani washanifahamu kwamba mimi sasa ni mtu wa namna gani, siwezi kukumbatia nyoka tena.

Nilipofikia ukinipiga kofi, nakurushia bomu huu upuuzi wa kumuachia mungu aamue sina tena.Tutajibu dhambi zetu tukiwa kwenye kiti cha enzi
😄😄😄😄😄😄 Undugu lawama.
 
Hivi ndugu ukimpa mfano 50k utamaliza shida zake.?

Jibu ni hapana, na wala hatokushukuru kiviiile atasema si 50k tu na atarudi tena baada ya muda mfupi... lakini ukiwapa ndugu 10 tayari hiyo ni 500k ila wao hawajui wanaona 50k tu.

Siku ummyime sasa, we mnyime tu utaona!

Haya maisha tusaidiane kwa mawazo tu, haya hayana hasara... kwa pesa na vitu labda kwa nyakati za lazima tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom