Zamani nilikuwa namshangaa mtu aliyefanikiwa kimaisha na hasaidii ndugu zake, Leo mimi natamani hata kuwapiga Risasi

huwajui tu ndugu
Tuume na kupulizia, hakuna ajuaye kesho yake ndio maana tunaishi kwa kujihami. Tunaweka akiba ya fedha na kumheshimu kila mtu kwasababu hatujui nani atakuwa nani kesho na wewe utakuwa nani kesho.

Binafsi huwa napenda sana "opposite" ya aya hii kutoka kwenye msahafu isemayo, "usilotaka kutendewa usimtendee mtu mwingine". Sijui imenifahamu mantiki ya usemi huo.
 
Muda mwingine kutumia hekima kwenye changamoto hizi za kifamilia ni kujimaliza mwenyewe, unaonesha upendo kwa watu ambao wao hawana upendo na wewe. Wanakuchekea kinafiki ukiwapa msaada, wakitoka wanapanga mipango ya kukudhuru na kukuombea uharibikiwe.

Binadamu wana Roho mbaya sana, hata Yesu hakuwa na kosa lakini walimsulubu msalabani japo aliwapa chakula wakiwa hoi na njaa walivokula na kushiba wakaanza kumtesa. Wanaonesha kukupenda lakini mioyo yao imejawa chuki. Naandika haya nikiwa na Jazba siku kadhaa zilizopita ningekuwa niko karibu na viumbe hawa waliofanya niandike hapa basi leo maiti kadhaa zingekuwa mochwari au zishazikwa na mimi ningekuwa nyuma ya nondo.

Ndugu zangu kwa sasa ni ndugu wa damu tu wadogo zangu na mama zangu. Hawa wanaojiita ndugu za baba huu ushenzi wanaoniletea kwenye familia yangu na mimi binafsi pamoja na kujishusha sana kwao Imefika mahali imetosha, naona ni kama nakumbatia kundi la wachawi huku nikijifanya nawapenda. Huku wao wakiwa na mipango yao binafsi.

Nimesaidia sana kifedha na kila aina ya msaada lakini hawa watu nia yao sio njema Lakini majibu niliyowapa nadhani washanifahamu kwamba mimi sasa ni mtu wa namna gani, siwezi kukumbatia nyoka tena.

Nilipofikia ukinipiga kofi, nakurushia bomu huu upuuzi wa kumuachia Mungu aamue sina tena. Tutajibu dhambi zetu tukiwa kwenye kiti cha enzi.
Achana na ndugu, kula bata na malayer
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom